Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa Wataalamu uliofanyika tarehe 1 na kufuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 2 na hatimaye leo Mawaziri. Mkutano ulijadili maandalizi ya mkutano wa kilele wa umoja wa mataifa wa mazingira, katika ngazi ya Jumuiya. Waziri aliyeongoza Tanzania katika majadiliano hayo ni Mheshimiwa Fatma Abdulhabib Ferej, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Katika ngazi ya Makatibu Wakuu, aliyeongoza ni Ndugu Sazi Salula, Katibu Mkuu katika ofisi ya Makamu wa Rais, wengine ni Ndugu Maimuna Kibenga Tarishi -katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii, Ndugu Uledi Mussa -naibu katibu mkuu wizara ya ushirikiano wa afrika mashariki na dkt Islam Salum, Naibu Katibu Mkuu wa Mazingira Zanzibar. Ngazi ya wataalam.iliongozwa na Dkt Abdullah Makame wa Wizara ya Afrika Mashariki akisaidiwa na Bertha Nyange Wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Wataalam mbali mbali walishirika kutoka sekta za umma na binafsi.
Home
Unlabelled
Mkutano maalum wa kwanza wa Baraza la Mawaziri wa Sekta za Mazingira na Maliasili wa Afrika Mashariki wakamilika Arusha Leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mitego hiyo ankarrr!! unaona enhe?
ReplyDelete