Mhandisi Mshauri wa Kampuni ENV Ltd ya Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Fredrick Mtoga (kulia) akitoa maelezo mafupi namna walivyoweza kuuchepusha mto wa Mkondoa wakati wa ujenzi wa Bwawa la Kidete, Wilaya ya Kilosa, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (mwenye kaunda suti ) alipotembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo hivi karibuni.
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ENV Ltd ya Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Fredrick Mtoga (anayechora ardhini) akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa Bwawa la Kidete, Wilaya ya Kilosa, kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( mwenye Kaunda suti ) wakati alipotembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (mwenye Kaunda suti) akiongozana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mgeni Baruani ,(wapili mstari wa pili kutoka mbele) alipofanya ziara ya kuangalia mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidete , Wilaya ya Kilosa hivi karibuni.
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ENV Ltd ya Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Fredrick Mtoga (anayenyoosha mkono ) akionesha eneo ambapo mto wa zamani ulipokuwa ukipita kabla ya kuchepusha mto huo ili kutoa nafasi ya ujenzi wa Bwawa la Kidete, Wilaya ya Kilosa, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( mwenye Kaunda suti ) wakati alipotembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo hivi karibuni.Picha na John Nditi wa Blobu ya Jamii.


.jpg)
.jpg)
Mungeimarisha yaliyopo kabla hamjaanza kujenga mengine.
ReplyDeleteMhandisi anaye toa maelekezo[Fredrick Mtoga] kwa kuchora chini kimsingi amepotoka maadili ya uandisi.
ReplyDeleteKatika kuelezea usahii wa ramani ya bwawa la Kidete,alitakiwa awe na takwimu na taarifa sahihi ya maandishi ikiwemo michoro,ramani,na maelezo ya kina baada ya feasibility study kufanyika.Inashangaza anaueleza umati kwa kuchora chini-kweli? kweli? ningekuwa mkuu wa mkoa ningemwambia afute mamichoro yake hapo chini na kuniletea taarifa sahihi ndani ya siku mbili.
Kiukweli ni kwamba nimeguswa sana na habari hii ya bwawa la kidete. Kama unakumbuka ni bwawa hili la kidete ambalo lilisababisha vifo na upotevu mkubwa wa mali mwaka 2009. Mpaka sasa waathirika wa mafuriko bado hatujarudi katika hali zetu za kimaisha tulizokuwa nazo kabla ya mafuriko. Kwa kupitia mtandao wenu huu, tunaomba mumtafute huyo muhandisi ( Fredrick Mtoga) aliyepewa dhamana ya maisha yetu atueleze hatua waliyofikia.
ReplyDeleteTunashukuru kwa ziara hiyo ya Bendera ila tunaomba mtupatie taarifa ya mradi kwani kutuonyesha picha tu haitoshi.
ReplyDeleteKuchora chini kunatokana na aina ya taarifa ambayo muelezwa alikua anahitaji kwa wakati huo. Si kila kitu kinaweza kuonekana kwenye mchoro na si kila mtu anaweza kuelewa mchoro. Lazima wewe kama mwalimu uwe na uwezo wa kumuelimisha mtu kwa njia mbalimbali kuliko kung`ang`ania njia moja ambayo kimsingi haiwezi kuleta matokeo mazuri ya uelewa.By the way, umefanya vizuri kuchangia maoni yako kwani hii inaonyesha ni jinsi gani ulivyoguswa na habari hii.
ReplyDelete