Wahenga walisema usipoziba ufa utajenga ukuta. Hii inajidhihirisha katika ukingo wa Ziwa Victoria sehemu za bustani mwanana ya jiji la Mwanza ambapo pametengenezwa na kupandwa nyasi nzuri ili wakaazi wa Rock City wapumzike na kupunga upepo. Tatizo ni kwamba ukuta uliojengwa kwenye kingo za mto huo zimeanza kumomonyoka, na hatua za haraka zisipochuliwa kurekebisha hali hiyo madhara makubwa yatatokea. Isitoshe Globu ya Jamii imeshuhudia watu wakitupa taka kwenye sehemu zilizibomoka!
Pamoja na mandhari ya kuvutia lakini Hali si shwari kama inavyojionesha...
sehemu ya uzio nayo imeanza kumeguka. Hii huenda inasababishwa na watu kutumia njia ya mkato baada ya kukosekana pa kuingilia kwa upande huu
Vibati vya uzinduzi wa bustani hii inasemekana vimeshafanywa chuma chakavu na wajuaji
Huduma ya maji ya ziwa inapatikana kwa urahisi, hivyo wazee wa jiji la Mwanza shime itunzeni sehemu hii
Huyu mama bila shaka anasikitikia hali ilivyoanza kuwa mbaya sehemu hii mwanana








Ziwa Mwanza:
ReplyDelete(JINA LIMEKAA VIZURI NA LIMEPENDEZA SAAANA)
Ahsante kwa utangulizi wa kuliita Ziwa kwa jina lake halisi ambalo ndilo linastahili kuitwa badala ya kuendeleza kuudumisha Ukoloni Mamboleo sijui ni kwa faida ya nani?
Hivi tukiamua kukataa kuendelea kuliita ziwa kwa jina la kitwana na la Kikoloni tuseme:
1.Tutanyimwa Misaada?,,,(kwa Dhana ya utegemezi wa Misaada tumekuwa kama Punda aliyefungwa kamba ya pua na kuwa hawezi kujitegemea kwenda mpaka akokotwe),,,au
2.Tutatengwa Kimataifa?,,,au
3.Masoko ya Utalii kama ni kigezo kuogopa kuyapoteza kwa nini tusitafute njia mbadala sahihi na kufikia lengo na tusiwe Jasiri na kufanya Uamuzi?
???????????????????????????????????
Hebu rekebisha hiyo title.. hili linaitwa Ziwa Mwanza?
ReplyDeleteNice pics...
ReplyDeletehttp://tembeatz.blogspot.com/
Kwa mmomonyoko huu wa ardhi, ni salaamu kwa ndugu zetu Zanzibar wanaotaka kuvunja Muungano. Kwa mabadiliko ya tabia nchi, hakuna kisiwa kitakachobaki. Hata Ukerewe wakae mkao wa kuhama. Z'bar waache jeuri maana siku si nyingi hawatakuwa na hiyo wanayoiita "nchi".
ReplyDeleteDu! eneo nzuri sana hilo limekaa utamu utafikiri Uchagani!
ReplyDeleteNdg yangu nataka kukuambia kuwa nyie waandishi ni watu ambao mnapotosha jamii zetu kila kukicha.Tangu nizaliwe sijawahi kusikia kuwa kuna ziwa Mwanza.Kwa mara ya kwanza ndo nasikia kwako.Upo tayari kubadilisha kichwa cha hii habari na kuomba radhi kwa wsomaji wako?Tafadhari fanya hivyo mapema iwezekanavyo.
ReplyDeleteHapo mitaa ya KAMANGA nini?
ReplyDeletePicha ya chini kabisa kwenye 'background' naona kama mjengo wa Meli za TRL
Wahusika watakuwa 'wamesikia'
David V
pazuri sana pakitunzwa patapendeza zaidi.
ReplyDeleteHaya ziwa Bukoba basi, furahi, najuwa wewe nshomile kila kitu wewe tu.
ReplyDeleteYes, hiyo picha ya mwisho Kamanga bwana, unayeya kuelekea busisi, hapo,lazima ununuwe vitumbuwa vya nguvu na sato makubwa makubwa wa kumimina walokaangwa na mama Mabhina, teh!teh! teh!
ReplyDeleteBeatiful scene.
ReplyDelete