Na Mery Ayo,Arusha

MTOTO mdogo ajulikanae kwa jina la Tatu Ally mwenye umri wa miezi tisa mkazi wa sombetini katika halimashauri ya Arusha amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa amelala kuteketea kwa moto.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Tobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo limetokea mnamo february 18 majira ya saa moja na nusu usiku.

Alisema kuwa ajali hiyo ya moto iliunguza nyumba ya mtu aitwae Stephano Masawe (85)ambaye ni mstaafu wa mamlaka ya maji taka na safi (AUWSA )na hatimaye kuweza kusababisha kifo cha mtoto huyo.

Aidha kamanda alileza kuwachanzo cha moto huo kinasadikika kilitokana na mlipuko wa jiko lamafuta ambao ulienea kwenye chumba na hatimye kusababisha ajali hiyo.

Aliongeza kuwa moto huo ulianza kuwaka katika chumba cha mpangaji aitwae Neema Ally na ndipo baadhi ya mashuhuda walipiga kelele za kuomba msaada ambapo kwa bahati nzuri haukuweza kuenea kwenye vyumba vingine.

Aliongeza kuwa kujulikana kwa kifo cha mtotohuyo kulitokana mama huyo aitwae neema ally kueleza kuwa kabala ya ajali hiyo alikwenda dukani na kumwacha mtoto wake ndani na ndipo aliporudi alikuta moto umekwisha enea chumba kizima.

Mara baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi ambapo askri waliokuwa doria katika maeno hayo walifika katika eneo hilo na kukuta mwili wa marehemu ukiwa kitandani mwa chumba hicho ambapo waliuchukua na kwenda kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mount meru

Kamanda alisema kuwa bado Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. 100% confidence levelFebruary 20, 2012

    Mnapokua mnatoa taarifa za huzuni na simanzi,jaribuni kuweka picha zenye kuendana na ujumbe husika.Nalisema hili kwa kusoma ujumbe wa kuungua kwa mtoto huyu halafu picha ya RPC akitabasamu.

    ReplyDelete
  2. hakuna sababu ya kuweka picha ya kamanda wa polisi wa mkoa. Halafu anatabasamu.

    ReplyDelete
  3. Sio tu anatabasamu, kaweka na posi haswaa!

    ReplyDelete
  4. nawaunga mkono wadau hapo juu. Picha ya kamanda ya nini.
    nadhani bro michu yuko likizo hii isingetokea.

    ReplyDelete
  5. RIP mtoto, huyu mmwela shoga au vipi, unakenua nini wakatati mtoto kapoteza maisha wajameni!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...