Mtoto Cesilia Edward (pichani) amefariki dunia jana saa tano usiku wa tarehe 08 katika hospitali ya Regency ya hapa jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa siku mbili kwaajili ya matibabu

Marehemu Cesilia alikuwa na umri wa miaka 14 alikuwa na tatizo la moyo na figo kushindwa kufanya kazi na kusababisha tumbo kujaa maji na kuvimba.

aligundulika na tatizo hilo tangu alipozaliwa.

Kampuni ya Africa media Group wamiliki wa Channel ten Kupitia kipindi mimi na Tanzania ilifanikiwa kumpeleka mtoto Cesilia nchini India kwa matibabu mwaka 2011 mwezi Oktoba lakini hakufanikiwa kupata matibabu (operation) baada ya madaktari kuthibitisha kuwa alikuwa amechelewa kwa matibabu.

Cesilia alikuwa mtoto yatima na kulelewa na familia ya Bw. Peter Nyarugembe mkazi wa Mbagara kuu ambaye alikuwa akimlea baada ya kukuta akilelewa na dada yake wilayani Kisarawe na alimkuta na tatizo hilo ila kutokana na hali ya uchumi aliyo nayo hakuweza kumsaidia kupona ugonjwa alio nao na kuamua kuomba msaada kwa wasamalia wema kupitia Kipindi cha mimi na Tanzania.

Marehemu alifikishwa hospitali jumatatu ya tarehe 6 mwezi huu akiwa na hali mbaya iliopelekea kupoteza fahamu na kumbukumbu kila wakati hali iliendelea hivyo mpaka umauti ulipo mkuta.

Mungu ailaze roho ya marehemu Cesilia mahala pema peponi.

-Amen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Pole sana mlezi pamoja na Dada wa Cesilia. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu Cesilia, ipumzike kwa amani, Amen.

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  3. RIP - inauma lakini wanadamu tuna kikomo, tumwachie Mungu,

    ReplyDelete
  4. R.I.P CECILIA.

    UNCLE NAOMBA, PICHA HII IBADILISHWE AU IONDOLEWE KABISA.
    USHAURI WANGU.

    ReplyDelete
  5. Cecilia kapumzike kwa amani kwani umeteseka sana hapa duniani.

    Mungu akupe neema nyingi huko unakokwenda. Amin

    ReplyDelete
  6. Maskini, inauma sana, lakini yote ni mapenzi ya Mungu, inabidi tumshukuru. Ameteseka sana binti wa watu kwa kweli, Mungu ampumzishe katika amani yake sasa. RIP Cecilia.

    Watanzania na wapendwa wote mliojitokeza kumsaidia binti huyu Mungu awalipe maradufu. Mzee uliyechukua jukumu la kumlea mtoto huyu na Dada Hoyce Temu, kazi yenu si bure mtalipwa na Mungu, mbarikiwe sana!

    ReplyDelete
  7. Mungu akuweke mahali pema na pumzika salama baada ya mateso ulikuwa ukiyapata mtoto Cecila Edward. Emin

    ReplyDelete
  8. Poleni sana wafiwa ni kipindi kigumu kwenu na mungu atawaongoza na kuwapa nguvu kwa kipind hiki

    ReplyDelete
  9. R.I.P We will remember you always.

    ReplyDelete
  10. Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

    ReplyDelete
  11. mungu akupe nguve Cecilia pumzika kwa amani,good night dear,kimeniuma sana nilipofungua hii blog kuona picha yako hoooooooooooooo yesu nalia mie,sikujui lakini wewe kama mtoto wangu.

    ReplyDelete
  12. CECILIA ULIPANGIWA NA MUUMBA WAKO MAISHA YAKO NA MUDA WAKO WA KUISHI HAPA DUNIANI, KWA HIYO SISI SOTE TUWAPITA NJIA HAPA DUNIANI, TUNAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA MAPENZI YAKE YOTE! BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LITUKUZWE MILELE YOTE AMINA!MUNGU BABA ULIYE KIMBILIO LETU NA ULIYEMUWEZA WA YOTE UMPE CECILIA PUMZIKO LA MILELE AMINA.

    ReplyDelete
  13. inna lilah waina ilah rajiun.

    ReplyDelete
  14. MLEZI WA HUYU MTOTO ANASUBIRI KUVIKWA TAJI MBINGUNI. NANI ANGEKUBALI MATATIZO YA KUUGUZA MTU ASIYEKUHUSU? MUNGU AKUTIE NGUVU.

    ReplyDelete
  15. PUMZIKA KWA AMANI CECILIA

    ReplyDelete
  16. Inna Lilah Waina Ilah Rajiun.

    ReplyDelete
  17. Mungu awajaze nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu familia yote na ailaze roho ya Cecilia mahali pema peponi amen. So sad jamani

    ReplyDelete
  18. Mungu ailaze roho ya Cecilia mahala pema peponi

    ReplyDelete
  19. MZEE WA BUNJUFebruary 10, 2012

    Inna lillahi waina ilaihi rajiuun, hana dhambi anaenda janna tu,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...