Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue akiagana rasmi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki Moon baada ya kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Ban Ki Moon na Balozi Sefue wakiwa wameshika picha iliyochorwa na kijana wa kitanzania, Davis Michael Kilawilla, sahemu ya maelezo ya picha hiyo inasema "Mama ni Mama hata akiwa katika mazingira magumu namna gani, hata akiwa jela mapenzi yake kwa watoto wake hayana kifani anatafanya kila awezalo kwaajili ya watoto wake" kijana Davis amempatia mchoro huo Ban Ki Moon kutambua mchango wake katika kuwasaidia wanawake. Ban Ki Moon ambaye alionyesha kufurahishwa sana na zawadi hiyo ameahidi kumwandikia mwanafunzi huyo ili kutoa shukrani zake.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki Moon, akifurahia jambo na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Ombeni Sefue wakati Balozi Sefue alipokwenda kumwanga, katika mazungumzo yao ambayo yaligusia masuala mbalimbali, Ban Ki Moon alishindwa kabisa kuzuia kuelezea hisia zake na mapenzi yake kwa Tanzania,Ukaribu wake na Rais Jakaya Kiwete na pia akaelezea masikitiko yake makubwa ya kuondoka msaidizi wake wa Karibu Naibu Katibu Mkuu Asha- Rozi Migiro. akadokeza kwamba Naibu Katibu Mkuu ajaye hatatoka Afrika.
Balozi Ombeni Sefue akimwelezea Ban Ki Moon kuhusu mchoro uliopo kwenye picha iliyochorwa na mwanafunzi wa Kitanzania, Davis Michael Kilawilli anayesoma nchini Malaysia, kijana huyo ambaye ni mshabiki mkubwa wa Ban Ki Moon aliichora picha hiyo kufuatia juhudi kubwa anazozifanya katibu mkuu katika kutetea na kuendeleza maslahi ya wanawake. Mwanafunzi huyo aliomba Mhe. Balozi amfikishie picha hiyo kwa Ban Ki Moon na bila ajizi Balozi alimkabidhi Ban ki Moon.
Na Mwandishi Maalum
New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete imekuwa mstari wa mbele katika kusukuma mbele ajenda za Umoja wa Mataifa zikiwamo za Maendeleo na Ulinzi wa Amani.
Na kwa sababu hiyo, Mkuu huyo wa UM, anasema anaridhishwa na kufurahishwa sana na uhusiano wa karibu ulipo baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Ameyaeleza hayo siku ya jumanne wiki hii, wakati alipokuwa akiagana na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue aliyekwenda kumuaga rasmi baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Katika mazungumzo hayo, Ban Ki Moon, alishindwa kujizuia kuelezea hisia zake na mapenzi makubwa aliyonayo kwa Rais Jakaya Kikwete na Watanzania kwa ujumla.
“ Ninahisia za pekee kuhusu Tanzania, uhusiano wangu na Rais Kikwete ni wa aina yake, ninasikitika kwamba imekulazimu uondoke baada ya kukaa hapa kwa muda mfupi, lakini napenda niliweke hili wazi, kwamba ninafurahishwa sana na mchango wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa” akasema Ban Ki Moon
Na kuongeza, ninajua unakwenda kushika wadhifa mkubwa sana wa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, ambeye amejijenga heshima kubwa Barani Afrika na katika Jumuia ya Kimataifa. Nimekuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara, amenisaidia sana katika masuala mengi likiwamo hili la mpango wa kimataifa kuhusu Afya ya Mama na Mtoto”.
Akasema ni matumaini yake kwamba, Balozi Sefue katika wadhifa wake mpya bado ataendelea kufuatilia kwa karibu masuala ya Umoja wa Mataifa kwa namna moja ama nyingine, na kwamba asisite wakati wowote kuwasiliana naye, ama kwa niaba ya Rais au katika nafasi yake ya Ukatibu Mkuu kiongozi. Na kwamba kwa upande wake bado ataendelea kuitegema Tanzania.
“ Katika muda mfupi uliokaa hapa, umepata fursa ya kufahamu mambo mengi ambayo nina hakika utayafuatilia na pengine utaendelea kutusaidia katika wadhifa wako mpya. Nipigie simu wakati wowote iwe kwa niaba ya Rais Kikwete au wewe mwenyewe nitafurahi sana kuwasiliana nawe” akasisitiza Ban Ki Moon.
Pamoja na kuelezea kuridhishwa kwake na mchango wa Rais Jakaya Kikwete na Tanzania kwa ujumla katika masuala ya Umoja wa Mataifa. Ban Ki Moon alitumia pia fursa hiyo kumshukuru Msaidizi wake wa karibu, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro.
Ban Ki Moon amemuelezea Asha- Rozi Migiro kama kiongozi mchapakazi sana na ambaye amekuwa msaada mkubwa wake, na anasikitika kwamba anaondoka .
Akadokeza pia kwamba amekwisha kufanya majadiliano ya karibu sana na ya kina na Naibu Katibu Mkuu wake kuhusu nani atakaye jaza nafasi yake na kwamba safari hii hatatoka Afrika.
Kwa upande wake, Balozi Ombeni Sefue ameshukuru Katibu Mkuu kwa ushirikiano mkubwa aliompatia wakati akiwa hapa Umoja wa Mataifa, na kwamba ingawa anaondoka lakini ataendelea kufuatilia masuala ya Umoja wa Mataifa, na kuangalia namna gani Tanzania itakavyoendelea kuchangia.
Akaongeza kuwa baadhi ya changamoto atakazofuatilia kwa karibu ni matatizo ya ajira kwa vijana na kuongezeka kwa pengo kati ya walionacho na wasionacho na kwamba masuala hayo mawili yasipotafutiwa ufumbuzi yataendelea kusababisha uvunjifu wa amani kwa kuwa ni masuala yanayozigusa nchi zote duniani.
Balozi Sefue will surely be missed at the mission and the UN in general.
ReplyDeletethis is not true brother. huyo jamaa ni agent wa fake friends of africa. will never have true love with Tanzania and Africa.
ReplyDelete