Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kwanza la Africa kuhusu Uendeshaji, Changamoto na Fursa katika Uhifadhi wa Mbuga za Wanyamapori na Maeneo yaliyohifadhiwa (The 1st Pan-African Conference on Sustainable Tourism Management In National Parks and Protected Areas: Challenges and Opportunities).

Kongamano hilo la siku Tano limepangwa kufanyika katika Kituo ya cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 15 hadi 19 Oktoba 2012. Washiriki wapatao 300 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kuhudhuria.

Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kufuatia mkutano wake (UNWTO General Assembly) ambao ulifanyika nchini Korea 2011. Katika Mkutano huo Tanzania pia ilichaguliwa kuwa mjumbe katika Baraza la Utendaji (Executive Council) la Shirika hilo, nafasi ambayo itakuwa nayo hadi mwaka 2015.

Kongamano hilo la Oktoba 2012 ni la kwanza na la aina yake litawakuwakutanisha wahifadhi na wadau wa sekta ya Utalii ili wajadili namna ya kufanikisha uhifadhi na utalii duniani. Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo kutokanana na sifa nzuri na uzoefu ilio nao katika kuanzisha na kuendeleza hifadhi za Taifa.

Tanzania inategemea kupata manufaa kutokana na Kongamano hilo kwani washiriki watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini na hivyo kuvitangaza warudipo makwao. Pia watanzania watapata fursa ya kuuza huduma mbalimbali kwa wageni watakaohudhuria Kongamano hilo, kama vile malazi, chakula, burudani na usafiri.

Faida nyingine ni kuwa, washiriki kutoka Tanzania watapata fursa ya kubadilishana ujuzi na ueledi na wenzao watakaotoka nchi mbalimbali duniani.

Wizara inatoa wito kwa wanachi, wafanyabiashara na wadau wote kujiandaa ipasavyo ili kunufaika na ujio huo wa Kongamano hilo la kimataifa nchini.

Taarifa mbalimbali zitaendelea kutolewa kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Kongamano hilo.

George Matiko
MSEMAJI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
23 Februari 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...