Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Mhandisi John Msemo (wa tatu kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kuangalia mipaka ya barabara kabla ya kukabidhi rasmi mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa kampuni ya CRJE uliofanyika Kurasini jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mhandisi, Lumeya M. Kasambaganya, Mhandisi wa Kampuni ya Norplan, Mussa Nyamsingwa na Kushoto ni Mhandisi Mkuu wa Kampuni inayojenga daraja hilo ya CRJE, Zhou Zejun.
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Mhandisi John Msemo (wa tatu kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kuangalia mipaka ya barabara kabla ya kukabidhi rasmi mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa kampuni ya CRJE uliofanyika Kurasini jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mhandisi Mkuu wa Kampuni inayojenga daraja hilo ya CRJE, Zhou Zejun.Picha na Francis Dande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ankal
    Daraja hili linajengwa Kurasini wapi hasa, hebu tuwekee hapa mchoro wa ramani yaani location. Tunaachwa hewani kuambiwa tu Kurasini!!!!

    ReplyDelete
  2. Nyie NSSF kwanza Asante kwa huo mradi.Lakini hakikisha mnawambia mapema hao Wajenzi kiwango cha hilo Daraja..Siyo baada ya muda linaanza kubomoka tunaanza kupiga kelele hooo hawakukidhi viwango...ooh mara hivi.Barabara ya kutoka Chato nadhani hadi Kimwani(Kagera) haina miaka mitatu imejaa viraka kibao,hizi barabara zetu kuu mpya ni aibu tupu ikiwemo na hii ya Kilwa.Hao jamaa ni 'wasanii"wanahitaji ukaguzi wa kweli kweli.Kazi wanachapa sana hilo sipingi ila.....

    David V

    ReplyDelete
  3. haya ndio maendeleo yanayotakiwa.
    sio tuu maslahi binafsi,na wengine kulalamika ohh serikali haifanyi kitu chochote!!!kazinzuri saisdieni kukwamua nchi yetu.

    mdau washington

    ReplyDelete
  4. Afadhali NSSF mmeamua kusimamia wenyewe badala ya kuwachia watu wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...