Askari wa kikosi cha zima moto wakijaribu kuzima moto kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mwandishi wa habari wa Star Tv,Bw. Enos Masanja iliyokuwa ikiteketea kwa moto maeneo ya Soweto,mjini Moshi.
Baadhi ya wapangaji katika nyumba ya jirani wakijaribu kuokoa mali zao.
Hawa zimamoto wetu naona bado wananchangamoto ya vitendea kazi.
Mmoja wa wapangaji katika nyumba hiyo Bw Yusuph akijaribu kuokoa mali zake.
Mwandishi Enos Masanja akitazama nyumba aliyokuwa akiishi ikiteketea.
Kikosi cha zima moto wakijaribu kudhibiti moto usishike nyumba za jirani.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kwa uzimaji moto huo bado tuko nyuma sana kwani hatuna vifaa na wazimaji wenyewe sio...au hawana taaluma hii, ukiiangalia hio picha tu utapata jibu

    tumuombe mungu tu ila wapelekwe sehemu wakasomee hii kazi

    ReplyDelete
  2. Wakasomee wapi?Hapo ndiyo tayari wamehitimu ndugu yangu.Vitendea kazi duni kabisa.Sasa matukio kama hayo yakitokea sehemu mbili au tatu tofautisi mpaka vifaa vyao(zima moto)vitaungua? Inasikitisha sana

    ReplyDelete
  3. nyie kazi kupepeta midomo tuuuuu nafasi zenyewe za kazi ndio hizi muje mufungue vyuo na maofisi binafsi ya zima moto.

    ReplyDelete
  4. sasa hata air mask hawana na helmet za kazi wala hawana hata vifaa vya kuingilia ndani chumba cha moto na horse zinavuja maji kiasi hicho yaani bado sana lakini msikatike moyo wabongo mtafika tu huko muendako ,
    Keith New York

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...