OFISI YA RAIS IKULU-UTAWALA BORA
TAARIFA KWA UMMA
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP - OGP)
Tanzania imeridhia kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership – OGP).
Mpango huu ni juhudi za kimatifa katika kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji wa huduma bora.
Vigezo vya nchi kuwa mwanachama wa Mapango huu ni pamoja na kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa (Country Action Plan) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na wananchi.
Kwa kuanzia, uandaaji wa utekelezaji wa Mpango huo utahusisha vipaumbele katika sekta tatu za Afya, Elimu na Maji ili kuimarisha uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika utoaji wa huduma.
Mpango huu sasa unaboreshwa kwa kupokea maoni na ushauri kutoka kwa Wananchi na Wadau mbalimbali. Njia za kukusanya maoni pamoja na Tovuti ya Wananchi (www.wananchi.go.tz), barua kupitia Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, S.L.P. 9120, Dar es Salaam, ujumbe bila malipo kupitia simu ya mkononi (SMS) namba 0658-999222, barua pepe: ogp@ikulu.go.tz.
Mpango Kazi wa OGP Tanzania unapatikana kwenye Tovuti ya Wananchi – www.wananchi.go.tz . Wananchi na Wadau wengine wanaimizwa kushiri kikamilifu kutoa maoni yao katika kuboresha Mpango Kazi wa OGP Tanzania. Mwisho wa kupokea maoni/ushauri au mapendekezo ni tarehe 30/03/2012.
IMETOLEWA NA OFISI YA RAIS
IKULU – DAR ES SALAAM
1,tupunguzieni rushwa pale uwanja wa ndege wa dar es salaam.
ReplyDelete2,tupunguzieni unyanyasaji na usumbufu sehemu za huduma za serikali zikiwepo wizara ya mambo ya ndani.
3,tupunguzieni shida za msongamano wa barabarani mjini dar es salaam
4,tupunguzieni ghalama za ushuru bandarini ili watu wasiweze kutumia rushwa ili kukwepa kodi ya serikali.
ni mengi kwa kweli ila nimechoka kuandika
na nimetanguliza kusema tupunguzieni kutokana ni shida kuondoa kabisa hizo adha sasa basi tupunguzieni japo kidogo yani kama rushwa punguzeni msichukue nyingi.
mdau niliechoka na serikali mbovu iliyojaa rushwa kila kona na uwajibikaji mmbaya.
Angalau muheshimiwa Raisi wa awamu hii anaonyesha ushirikiano na wananchi.Lazima tumshukuru kwa hili maana anajua kama wananchi wanapata shida.Na bila kusahau unyanyasaji kutoka kwa wafanyakazi wa serikalini maana wanakebehi sana hasa utakapoenda mapokezi uone dharau iliyokuwepo.
ReplyDeleteThe government should try implement ISO 9001:2008 and/or Six Sigma on all of it's ministries and their corresponding departments. That's one approach of driving down the rampant corruption while greatly improving efficiency.
ReplyDeleteWekeni madini na nishati kwenye list yenu!
ReplyDeleteNinakubaliana na Mdau wa kwanza kwakweli vtu alivyovitaja nivyakwanza haswa Bandarini(TRA)na Airport!
ReplyDeleteAnkal unaweza kuweka facebook link kwa most of news ili tuweze kuzipost kwenye facebook kama hii habari kabla ya wewe kuipost tulikuwa tunashauriana na wadau kwamba, kwa kupitia mitandao hii ya jamii tueleze matatizo katika sekta mbalimbali kisha tuishauri seriakli ni jinsi gani ya kuyatatua matatizo hayo. Kwani inavyoonekana viongozi wengi wamekaa madarakani kwa miaka mingi na bado fikra zao ni zilezile za miaka 30 iliyopita wanakuwa aidha hawaendani na mabadiliko au hawataki kubadilika kwa kujisahau kwamba dunia imebadilika na watu wanazidi kuwa waelewa zaidi huwezi kuwapiga siasa wakati kiongozi hana uwezo wa kumaliza kero za wananchi wake. Serikali isipokuwa makini siku za mbele itasumbuliwa sana na wananchi wake, hasa itakapoanza kuwa wazi kwani hapa inataka kujitia kitanzi lazima iwe imejiandaa kuwa wazi, kulingana na mkaguzi mkuu wa mahesabu inaonekana serikali ni wafujaji wakubwa sana wa fedha za walipa kodi na hata wakigundua watumishi wanofuja rasilimali za nchi hawachukuliwi hatua zozote za kisheria! Tunamba tuwekee links za tweet na fb na hii itasaidia zaidi kwa blog yetu kusomwa kila wakati na kujulikana zaidi. Asante
ReplyDeleteAhsante kwa KUFIKIKA na USIKIVU!
ReplyDeleteHii ni ishara ya kuwa sasa pana mchagizo wa kufikiana kati ya Mtawala na Mtawaliwa.
Katika nchi zilizoendelea suala hili limepiga hatua zaidi na sisi pia tumepata fursa muhimu kama hii.
Mfano mpango huu ukidumishwa na kuboreshwa zaidi tutapata faida nyingi ikiwemo:
1. Kuwa na E-Government portal, kuanzia ngazi ya chini kwa Serikali za Mitaa kurahisisha na kuwezesha majukumu ya Kiutawala.
2.Kupunguza ubadhirifu na Urasimu kwa vile inawezekano mambo kutawanywa (de centralization) badala kila kitu hadi Makao Makuu.
3.Kutoa msongamano (Foleni za Magari mabara barani na ,Ahadi za miadi ya Kuonana na Viongozi Maofisini kwa Huduma mbali mbali za Kiserikali.)
4.Itasaidia kubana matumizi ya Serikali kwa ujumla na kutupatia kasi ya Maendeleo.