Hello Michuzi,

whereby one of the Kenyan politicians said "For example Tanzania; they eat rats! But in this country (Kenya) if you tell people to eat rats, they will not eat. Therefore ppl will die of hunger and there are rats here"

Ningependa kuuliza eti ni kweli wananchi wenzangu wanakula wapanya? Sijawahi kuisikia hiyo before.

Mdau,
UK.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Watani wa Jadi, Ndezi siyo Panya??

    ReplyDelete
  2. Ndio, nenda kaolee huko Uyaoni utembee juu ya viuno vya watu, na baada ya hapo- kitu 'chamaki nchanga'.

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu mdau wa UK, kwanza naomba kukuuliza wewe mtanzania kweli? Maana hakuna mtanzania anaweza kusema wapanya. Sasa kuhusu kula panya wewe ndugu yangu unanishangaza sana, je unajua kuwa nchi zilizoendelea kama Ufaransa wanakula chura tena ni moja ya vyakula vya gharama sana. Unashangaa sisi kula panya. Basi kwa taarifa yako tunachokula sio panya hawa majumbani bali ni wanyama wanaofanana na panya wanaishi porini
    Kwa taarifa yako ni watamu sana, mimi ni mmmojawapo ninaekula.
    Achana na hizo, huko Marekani tunaona kwenye program za luninga wanaonyesha mashindano mbali mbali ambapo washindani wanatakiwa kula funza na vidudu aina mbali mbali.

    ReplyDelete
  4. Vipi kuhusu wamakonde? Ila kwa kusema Tanzania kwa ujumla hapo alitokosea na pia wamakonde walikuwa wanakula enzi zile sijui kama hadi leo wana hayo maswala ila hata sisi huwa tunawatania Samaki Nnchang'a

    ReplyDelete
  5. afadhali sisi tunakula panya,kuliko wao wnakula jasho la maskini wenzao(Rushwa iliyokisiri duniani).Hawa jamaa wanajisikia sana na hawana lolote.

    ReplyDelete
  6. NI KWELI KABISA PANYA NA WADUDU WOTE WASIOFAA WANALIWA TANZANI, hajakosea huyo bwana sasa nini mnakataa wa bongo HUKO mTwara chakula kikuu ni panya

    ReplyDelete
  7. Jamani ukweli ni kwamba wala panya tupo wengi sana ila basi tu hamtaki kukubali. Ukienda Sumbawanga panya ni kitu cha kawaida kabisa, tena ngoja nikupe bei, panya wa kawaida ni sh 500, akiwa mkubwamkubwa sh 700 mpaka 1000, achen mchezo bhana. Afu kule kwetu Swanga, mgen ukiandaliwa panya basi umeheshimika kwelkwel.
    Kama hayaamini haya basi aende Swanga, nauli ni 54000/= bila chenji.

    ReplyDelete
  8. Jamani msitokwe na povu la mdomo kwa jazba,kitu chochote kinasemwa pimia msemaji kalenga nini? kashfa,kashangaa au ni nini hasa kusudio lake? na mwisho wa yote kila watu na utamaduni wao panya kweli analiwa sio Bongo hata India wanakula panya.

    ReplyDelete
  9. Ndio maana sitaki shirikisho na hawa jamaa wana dharau nyingi sana,wamesahau kama Mahindi wanayokula yanatoka Tanzania nchi yao ni nusu jangwa.......hawa jamaa wananikera sana !

    ReplyDelete
  10. Rats are cream of southern coast,guys

    ReplyDelete
  11. Tunakula panya na ni watamu sana kama kuku vile.

    ReplyDelete
  12. Ndio Panya wanaliwa TZ, hasa kule kusini tena wanaitwa CHAMAKI NCHANGA hahahahahaha

    ReplyDelete
  13. Kwa taarifa yako Panya wanaliwa sehemu kibao Duniani si Tanzania tu. Marekani wanakula vyura, wanakula Alligator ambao ni jamii ya mamba pia wanakula kobe, possum, vicheche, squirrels. Hadi Farasi analiwa Marekani.
    Vyakula vinaendana na utamaduni wa sehemu. Kila unapokwenda utashangaa vyakula wanavyokula, na wakija kwako watashangaa unachokula.
    Hata hao wakenya utakuta baadhi yao wanakula panya.Wabongo msipandwe na jazba za kingese.

    ReplyDelete
  14. KUSHIBA SI NENO. HATA KULE KWETU KENYA TWALA INZI. INGAWA SI KILA INZI ULIWA. SISI TWACHAGUA WALE TU WAKUBWA WAKUBWA WA KIJANI.

    ReplyDelete
  15. Huyo MKENYA aende zake kule,! toka zako hapaaa!

    Kenya na Tanzania wapi kuna ukame na njaa?

    KENYA INA NJAA HADI KWENYE MISHIPA YA DAMU NA MAJI NI MGOGORO, PANA SEHEMU KAMA GARISSA MTU ANAOGA KWA MWEZI MARA MOJA!

    KENYA AIRWAYS (Shirika la ndege la Kenya) limerusha ndege miezi kadhaa mwaka jana 2011 bila (inflight meals) chakula cha kwenye ndege, ilikuwa kusafiri nao ufunge fuko la maandazi kabla ya kufunga mkanda tayari ndege kuruka kwa Safari!

    Jamaa wana njaa sana na wanategemea wizi wa chakula chetu kwa njia za magendo mpakani!

    KWANZA CHAKULA YAO YA MAANA NI ''SIMA KWA NYAMA'' yaani Ugali kwa nyama wakati kwetu Ugali ni chakula cha Kuli,mfyatua matofali au mbeba zege!

    WANASHANGAA NINI KULIWA PANYA ?,,,SI MIFUGO YA KAWAIDA TU?,,,HAWAJAENDA CHINA?,,,CHINA WANAKULA HADI KONOKONO WACHA PANYA TU!

    ReplyDelete
  16. Proteins rich, and I tell you once you try it you will never dare to miss it. Mmmm.. denda lanitoka nikikumbukia!

    ReplyDelete
  17. Ndugu panya au chamaki nchanga pale Lindi wanaliwa kwa sana tu ila ni panya wa porini kama kungekuwa na nafasi ya kuattach ningeattach picha ujionee, niliipiga mwaka jana maeneo ya kijiji cha Ntene wilaya ya Lindi

    ReplyDelete
  18. Mnashangaa panya, mbona baadhi ya nchi za Asia wanakula nyoka.

    ReplyDelete
  19. Huyo jamaa hajaiweka sawa hii taarifa, panya wanaliwa Tanzania hasa maeneno ya Kusini. Mimi kwetu Masasi, Mtwara na panya wanaliwa lakini siyo chakula kikuu kama anavyoeleza huyo jamaa wa Kenya. Hakuna jambo la ajabu hapo lakini kukuzwa kwa jambo ndiyo tatizo. Mbona wangoni wanakula mbwa?

    ReplyDelete
  20. YES PANYA WANA PROTEIN YA HALI JUU KULIKO KITU CHOCHOTE SUMBAWANGA NA MTWARA WANAKULA.PANYA WANAOLIWA NI WALE WA MASHAMBANI WANAOKULA MAZAO SI WANDANI.TENA MI NIMEKULA NI WATAMU SANA HUWA WANABANIKWA,PANYA NI WATAMU KULIKO SENENE,DAGAA,KUMBIKUKUMBI,CATTERPILA NK

    ReplyDelete
  21. Vyote vimeumbwa kuliwa ukiona wewe huli hiki lakini una unachokula mbacho mwenzio hali kwa hiyo hamna sababu ya kutoleana macho! kuna wanaokula chura ,wengine mbwa, wengine panya ,wengine nyoka, wengine mchwa, wengine konokono, wengine mijusi,wengine kobe nk,nk lakini wote ni watoto wa baba mmoja na alikuwa na malengo na makusudi yake kutuumba hivyo alivyotuumba.

    Hamna haja ya hasira wala nini, kwa nini ujipe adhabu bila sababu?
    Wewe endelea na maisha yako nao na ya kwao!

    ReplyDelete
  22. panya wanaliwa wala sio kwamba wanadharau huko ntwara tunaita samaki nchanga.....................

    ReplyDelete
  23. For me personally it doesn't matter since no one has ever died from eating rat meat. Many nationals eat weird foods not to say delicatessens. Foods like snails,crabs, cockroaches and other funny bugs, monkeys, snakes just to mention a few are consumed and yet no one utters a word about them.Eat if you can, provided you don't tumble a bucket and if you can't don't eat. SURVIVAL IS THE POINT HERE!

    ReplyDelete
  24. Panya Nation! lol!

    ReplyDelete
  25. Yes ni kitoweo haswa mikoa ya kusini, wenyeji wa mikoa hiyo wanatumia kwa samna haswa panya wa mashambani si wale wa majumbani.

    ReplyDelete
  26. Basi wew sio Mtanzania,huku panya wanaliwa tena watamu samaki nchanga

    ReplyDelete
  27. Cha kunumbila mung ni cha kugegeda kasoro dijanga! tena kumpata pungo kwa nchele baaa!!! panya kwetu ntwara ndio kumwita kizungu PRAWNS!

    ReplyDelete
  28. Mnashangaa panya mbona kuna watu wanakula nyoka.

    ReplyDelete
  29. Ni kweli panya wanaliwa ila Wakenya wasijifanye wako special sanaaaa, hata wao wanakula

    ReplyDelete
  30. your excellency Tanzanians don't eat Rats because we are starved no,we eat them because they are delicacy.You Kenyans your are starved and rats will be so expensive for you aren't they?

    ReplyDelete
  31. HAHAH ILO NDIO TATIZO LETU KWENYE UKWELI TUNAKUWA NA JAZBA SI WOTE WANAKULA PANYA AU TUNAKULA PANYA ILA NI KWELI WAPO NCHINI KWETU TZ WATU WANAKULA PANYA, KAMA KENYA WAPO WANAOKULA WADUDU PIA AMBAO KWETU HATULI NI KITU CHA KAWAIDA NIGERIA KONOKONO, UFARANSA WANAKULA CHURA. NA WAPO WANAOSHANGAA WATU KULA NJIWA VILEVILE.

    SEMA KENYA SASA HIVI NJAA TUPU LABDA YEYE ALICHOKUWA ANASEMA KWENYE NJAA WAJITAHIDI KULA KITU CHOCHOTE KAMA NYAMA KAMA VINYAMA NA MAZAO YAMETOWEKA.

    ReplyDelete
  32. Tena ukute katupiwa Nazi na Karoti kwa mbali.. wee.. una chapati zako 2, wacha kabisa.

    Mdau,
    ITC - Holland

    ReplyDelete
  33. Panya ni panya tu, hakuna wa shambani au wa mjini.

    Tunakula panya na mbwa, vyote ni shwari kabisa.

    ReplyDelete
  34. jamani kiingiacho siyo haramu. ila nimempenda huyo mama kasema wanaume wakishindwa kazi wanawake wataikalia. duh wakenya!!!!

    ReplyDelete
  35. MKENYA amelewa Gongo la Kikenya ''CHANG'AA'' anashangaa nini Mtanzania kula panya?

    WAO KENYA NDIO WENYE NJAA KALI!!!

    Mbona hashangai mu Italiano kula (Alligator) au mamba?

    Mbona hashangai Mmarekani kula (Wolf cat) au paka wa porini?

    Mbona hashangai M Korea na Mu Italiano kula mbwa?

    Kenya wajadili jinsi kukabiliana na njaa yao na kuwapiga Al Shabaab Somalia kwanza ndio waangalie wengine wanakula nini?

    ReplyDelete
  36. jamani hao ni watani zetu. katoa utani nyie mwafura kama nyoka. hamuwezi kuona hata huyo mama anasema akikamatwa "ATATOA" baadaye kasema wanaume wakishindwa wakishindwa "ATAWAKALIA". mimi nahamia Kenya kama mambo ndo haya.

    ReplyDelete
  37. Kula Panya kwa Tanzania ndio ushahidi kuwa tuna rasilimali nyingi sana za CHAKULA ikiwemo panya!

    LICHA YA MAGHALA YA MAHINDI KUVUNJIKA KWA MAVUNO(Chakula ambacho kwetu ni cha chini ila kwao Kenya ni sawa na 'biriani'), PANYA PIA TUNAPELEKA ''YOMBO'' KAMA KAWA! HIYO NDIYO DALILI YA SHIBE YA MTANZANIA!

    Sasa wao Kenya ni njaa kali hawana aina nyingi za vyakula na wingi wa chakula hadi maghala kuvunjika kwa mavuno lumbesa kama sisi!

    ReplyDelete
  38. Ahhh wapi Wakenya waendelee kula Makande yao yaliyokorogwa mchanganyiko na Kabechi "Githeri"

    WAO NDIO INABIDI TUWAFUNDISHE KULA PANYA WAWEZE KUMUDU MAISHA KWA NJAA INAYOWAPIGA MARA KWA MARA!

    ReplyDelete
  39. KENYA:

    ''Ugali kwa nyama'' ni chakula cha kifahari sana ndio sawa na (Biriani la kupaka kwa kuku) huku Tanzania!

    NCHI YA NJAA KALI AFRIKA MASHARIKI!

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 28, 2012

    kenya tena ndo kuna njaa iliyokithiri huyo waziri anaongea kama mpumbavu amefanya tafiti gani kusema watanzania wana kula panya kwa sababu ya njaa wakati kenya kwa njaa ndo usiseme

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...