Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama katika Uwanja wa Ndege wa Sir Serese Khama jijini Gaborone, Botswana,wakati Rais Kikwete alipowasiri nchini humo leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pia atahudhuria sherehe za miaka 50 tangu kuzaliwa kwa chama tawala cha nchini huko cha BOTSWANA DEMOCRATIC PARTY.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Sir Seretse Khama jijini Gaborone, Botswana, leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pia atahudhuria sherehe za miaka 50 tangu kuzaliwa kwa chama tawala cha nchini huko cha BOTSWANA DEMOCRATIC PARTY.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama wakiangalia ngoma mashuhuri ya makhirikhiri.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua paredi ya Majeshi ya nchi hiyo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa shangwe baada ya kuwsili Gaborone.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Michuzi, mimi nimechoka na mwandishi wako. yaani siku hizi mnakosea sana spelling kwenye habari zenu....... karibu kila habari ninayosoma imekosewa vitu fulani, inakatisha moyo kusoma. Awe anasoma mtu zaidi ya mmoja kabla ya kupost.
    Asante

    ReplyDelete
  2. Jamani na wewe mbeya kweli. Mimi mbona naona limekosewa neno moja tu. Ukileta mambo ya sarufi, kasome vitabu tu. Habari za mtandaoni tegemea makosa madogo madogo. Mdau-Mhariri wa Kujitegemea.

    ReplyDelete
  3. Mdau namba moja unalalamika kuwa umechoka kusoma habari zinazokosewa spelling. Kumbuka kuwa Tulipata uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita. kwahiyo tumia uhuru huo kusoma blog zingine kama unajisisikia kichswa na spelling mistake za mwandishi wa michuzi. Hakuna anayekushikia bunduki kukulazimisha usome michuzi blog. badala ya kulalamika tumia muda wako kujiletea maendeleo yako binafsi na wanaokuzunguka.

    ReplyDelete
  4. 100% confidence levelFebruary 24, 2012

    Anonymous Fri Feb 24, 05:57:00 PM 2012,Suala la makosa ya kimaandishi siyo wewe tu linayekukera katika hii blogu ya jamii,kimsingi tupo wengi hususani tunaojua matumizi sahihi ya lugha mbalimbali,mathalani Kiswahili,Kiingeleza,Kifaransa nk.
    Hii ni dalili ya kuelemewa na habari ama kutokuwa makini wakati wa kuhakiki na kuzinakirisha mtandaoni.La sivyo basi mdau anayezinakirisha habari hizo ndiye hoi.Ankala fuatilia hili kwa makini kwani blogu hii hata Ban-Ki-Moon huwa anaipitia.

    ReplyDelete
  5. MIchui, jana nimepost kwako kero yangu ya umeme , nimekatia uimeme na tanesco kwa kuletewa bili ta millioni 19 ya mwezi huu, Ajabu ya Mungu, biashara yangu ni mgahawa hapa Magomeni na bili zote za mwaka mzima ninazo na nimelipa kila mwezi, sasa jamani waungwana ,hii bili ya millioni 19 ni ya wapi ?? hivi wamekwisha kata umeme wao na imenibidi nitupe kuku na nyama kutoka kwenye friza ,maana zimeharibika , naomba msaada wa hali na mali kwa yeyeote anayezijua sheria za nchi yetu. email yangu ndefu ya jana sijaiona kutoka ndiyo maana nazidi kukulia ,nipositie hii ulimwengu ujua kero na shida mazalendo anavyofanyiwa nchini kwake, mchinaa aaa!! anapeta tu. meneja Kipara

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Fri Feb 24, 07:36:00 PM 2012, nilikwishawahi kumkosoa JK kwenye blog hii kwa kuchangia sh. mil. 10 kwenye mfuko wa wamachinga mara ya mwisho alipokuwa Mwanza. Nilisema kuwa siku zote suluhisho au msaada si pesa tu, na nilishambuliwa sana kwa kutouthamini mchango huo.

    Leo hii wewe umekuwa mfano mzuri wa wafanyabiashara ndogo ndogo wengi hapa nchini. Mnakumbwa na mabalaa na vikwazo vingi kibiashara, ila waliosoma wanachojua ni kuwapa pesa tu.

    Nilikuwa kijijini mkoani Mbeya nafanya utafiti mwaka 2008. Mwanamama mmoja akanimbia ameahirisha kuchukua mkopo wa pili kwa sababu barabara si nzuri, hivyo hata akizalisha kwa wingi anaingia harasa kubwa kwani wenye malori hawataki kufika shambani kwake kumsaidia kufikisha mazao sokoni kwa sababu ya ubovu wa barabara.

    Leo hii wewe ukilalamika, wasomi wetu hawa wanaona unachohitaji ni pesa tu! Viongozi wetu wanapaswa kusikiliza na sio kusikia, wanapaswa kutatua tatizo kama lilivyo na sio kama wanavyolifikiria wao, wanapaswa kuwa viongozi na si watawala!

    ReplyDelete
  7. Machadema hadi huko!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...