Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania,Sylvester Manyara akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza uzinduzi wa kampeni yake kubwa ya kipindi cha Valentine ambapo wateja watakaonunua bidhaa aina ya Samsung Galaxy watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali iliyofanyika leo kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.Kulia ni Ofisa wa Samsung,Josheph Safari
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania,Sylvester Manyara akionyesha moja ya simu za Samsung.

Kampuni ya SAMSUNG Tanzania leo imezindua rasmi kampeni yake kubwa ya kipindi cha Valentine ambapo wateja watakaonunua bidhaa aina ya Samsung Galaxy watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Meneja Mauzo na Usambazaji wa kitengo cha Samsung Mobile kwa Tanzania Bwana Sylvester Manyara alisema mwaka huu Samsung imeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwazawadia wateja wake katika kipindi hiki cha kuadhimisha siku ya wapendao kwa kuwapa zawadi ambazo zinaendana na msimu huu.

Alisema maduka yanayohusika na kampeni hii ni yale tu ya mawakala wa Samsung Mobile waliothibitishwa. Wateja watakaonunua moja kati ya bidhaa za Samung Galaxy ambazo ni Galaxy Tab 10.1, Galaxy Tab 7.0 Plus, Galaxy Y Pro, na Galaxy Mini, kuanzia Ijumaa Tarehe 10/02/2012 hadi Jumapili tarehe 19/02/2012 watapata nafasi ya kuingia katika bahati nasibu itakayowawezesha kujishindia moja kati ya zawadi tatu kubwa.

Alizitaja zawadi hizo na kuongeza kwamba zote zitatoa fursa kwa mshindi kuja na mwenza wake. Mshindi wa kwanza atalipiwa gharama za usafiri na malazi kwenda Cape Town kwa mapumziko ya siku mbili, yeye na mwenza wake. Mshindi wa pili atapata nafasi na mwenza wake kutembelea mji mkongwe wa Zanzibar kwa siku mbili, gharama za usafiri na malazi zitalipiwa. Mshindi wa tatu na mwenza wake watapata zawadi ya kula chakula cha jioni katika hoteli yoyote ya hadhi ya nyota tano hapa Dar Es Salaam.

Ili kuleta haki na usawa, Droo ya kuwapata washindi hawa itashuhudiwa na kiongozi kutoka bodi ya kusimamia michezo ya kubahatisha Tanzania na itafanyika jumapili tarehe 19/02/2012 katika duka la Samsung Mlimani City. Washindi watakaopatikana watatangazwa katika vyombo vya habari, watatakiwa kupanga tarehe ya safari yao iwe siku yoyote katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia siku watakapotangazwa.

Bwana Manyara alisema lengo kuu la kampeni hii ni kuwazawadia wateja wake ambao wanatumia bidhaa za Samsung Mobile siku hadi siku. Mbali na wateja kufurahia bidhaa hizi bora kabisa, Samsung inawajali na inaonyesha upendo wake kwao katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya wapendanao duniani, yaani Valentine Day!.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Anachoonyesha siyo simu. Ni "Tembe" kwa kiingereza "Tablet"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...