Tanzania kila siku ya pili ya mwezi wa pili wa kila mwaka huadhimisha siku ya ardhioevu duniani (World Wetland day). Katika kila mwaka kuna kaulimbiu ambayo hutumika kuhamasisha uhifadhi wa Ardhioevu. Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni Ardhioevu na utalii. Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika Mkoani Arusha katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara ikiwashirikisha shule za msingi, sekondari za Makuyuni, Manyara Ranch, Edward Lowasa pamoja na Jumuiya ya kuhifadhi mazingira ya mto wa Mbu ya MUKUMU. Idar ya Wanyama pori kupitia Kisehemu cha Ardhioevu ilishiriki kwa kuwa na Maafisa wawili Bw. Lotha Laisser na Imani Nkuwi na kutoa mada za Ikolojia ya Ziwa Manyara pamoja na ardhioevu na Utalii. Pia maafisa kutoka Malhai clubs of Tanzania (MCT) walishiriki.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za mkoa wa Arusha wakisikiliza kwa makini elimu juu ya uhifadhi wa ardhioevu.
Wanafunzi wa Manyara ranch sekondari wakitoa ujumbe kwa njia ya Shairi juu ya Ardhi oevu na Utalii.
Mtaalamu wa Masuala ya Ardhioevu Kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Idara ya Wanyamapori Bw. Lotha S. Laisser akitoa mada juu ya ikolojia ya ardhioevu ya Ziwa Manyara kwa Wanafunzi na baadhi ya wananchi walioshiriki katika maadhimisho ya Siku ya ardhioevu Tanzania Mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...