Habari za leo kaka Michuzi

Jioni hii nimeona kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani ( Mohammed Mpinga) amekuja kutoa taarifa juu ya tuhuma za rushwa zilizotolewa  na mmoja wa wasomaji wako wiki ilopita.

Hii mada ya U-Turn nilishawahi kuileta hapa kipindi fulani lakini hakuna mtu kutoka usalama wa barabarani aliyekuja kutuweka sawa.

Sasa naliuliza tena hili swali.

Kati ya mambo muhimu yuyafuatilia unapoendesha gani ni alama za barabani, lanes na bila kusahau hazard perception (hatari ya watu au watumiaji barabara inayoweza kutokea muda wowote ule)

Kwa nini mtu ukiendesha gari Tanzania na hususan Dar es Salaam ukafanya U-TURN sehem ambayo hakuna kibao cha kuzuia U-TURN askari wa usalama wa barabarani wanakukamata?

Nauliza kwa sababu binafsi nishawahi kukamatwa na nikapelekwa Central na wakataka kuniweka ndani kwa kuuliza kuwa hakuna kibao kinachoruhusu U-TURN nilipofanya hiyo u-turn. 

Je sheria za uslama barabarani za Tanzania zinatofauti gani na za Uingereza kwenye hili suala la U-TURN? nasema kwa sababu unakuta nchi zingine kama UAE na hususan Dubai U-Turn zinafanywa kila sehem unless kuwepo na kibao cha kukataza

Naomba mkuu wa kikosi aje kutuweka sawa kama alivyofanya juu ya ile mada ya tuhuma za rushwa.

Asante

Mdau,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Ndugu yangu na mimi yalinitokea hayo lakini Askari nikamwambia siendi popote sababu nilipo u-turn hakuna kibao na nikampa leseni yangu ya international akasema twende polisi ya magomeni nikamwambia siendi akaingia kwenye gari kwa nguvu nikamwambia mimi ninakwenda safari mbali na utarudi mwenyewe kwa miguu akaomba nimrudishe ile sehemu nikamwambia sikurudishi akarudi mwenyewe nikweli watuwekee sheria zao kama hawafati international rules!halafu pia watuwekee wazi kuhusu maswala firestingwish vipi uwe na mtu halafu uwe na stika hii stika iko na maana gani wakati uko na mtungi mimi naona hatuna wabunge tanzania sbb vitu vingine wananyonywa wananchi nivyakijinga!

    ReplyDelete
  2. Nami jambo hili lilishawahi kunikuta. Nilipiga u-turn pasipo na kibao, ghafla polisi akatoka mafichoni na kunipiga mkono.

    Kamanda wa Polisi kamwe hawezi kupoteza muda wake kwa suala hili. Lile lingine la rushwa aliamua ajitetea kwa kuwa ni suala nyeti.

    Polisi wetu hawajui sheria! Huo ndio ukweli!!! Ni mara kumi kuongozwa na machinga kuliko polisi wetu.

    ReplyDelete
  3. Nimeisoma habari ya kamanda wa usalama barabarani wa Mkoa wa Iringa, sheria inasema unapokutwa na kosa na askari wa usalama barabara unapewa siku 28, huwe umelipa faini yako, sheria haitamki mahala popote kwamba lazima notification ilipwe siku hiyo hiyo au kama hukulipa basi polisi abaki na leseni yako. Kama polisi anakulazimisha kulipa siku hiyo basi hilo kosa kwa polisi na kama anataka leseni yako ibaki na polisi nalo ni kosa la polisi, inawezekana polisi hawajuhi hili au wanajua ila hii ni njia ya kujipatia chochote na hapa ndicho chanzo cha serikali kukosa mapato kwani Tanzania ya leo kila mmoja wetu mchakajuaji si ajabu kitabu cha risti za notification kikawa na nembo ya polisi lakini kikawa kimechapwa kariakoo.
    Serikali ingefanya magari yote yakawa centralised kwenye data base ya polisi hii ingesaidia katika siku 28 dereva akalipa kwa wakati wake kabla ya siku hizo, na hii ingesaidia kuokoa muda ili watu waende kazini kuliko kupoteza muda na polisi kwa kupatana bei, wakati fulani unakuta barabarani hakuna kibao cha speed limit lakini bila kutegemea utakuta polisi anatoka mbio na tochi na anakwambia mwendo wako mkali sana, hii siku moja ilinifanya niwe mkali sana na polisi barabara ya Chalinze na Bunda ilibidi niulize polisi kuna kibao cha speed limiti hapa? jibu hakuwa nalo alichosema kama silipi faini niache leseni, swali langu la pili lilikuwa hivi naenda Bukoba inamana wewe ni polisi peke yako kilomita 1600? Ndugu hii inatusumbua serikali fanyeni utaratibu wa kuweka magari yote kwenye data base ya polisi au TRA ili tulipe faini hizi tukijua hazipelekwi bar na nyumba ndogo.
    Prudence kahatano

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli waweke sawa hili suala la u-turn...sijawahi kukamatwa lakini ninapokuwa likizo Dar es salaam huwa nina wasiwasi sana wa kufanya u-turn hata inapolazimu.Je,sheria zetu zikoje hapa?

    ReplyDelete
  5. KUNA NA ASKARI WA JIJI LA DARESALAAM;UNAKUTA SEHEMU IKO WAZI HAINA KIBAO CHOCHOTE CHA KUZUIA KUPARK UKIPARK WANAKUDAKA.HAKIKA KUNAKUWA HAKUNA KIBAO CHA KUPARK WALA KUTOPARK5HII INAKUWAJE SASA?°.NI WASUMBUFU SANA;WEKENI ALAMA JAMANI SIYO KUVIZIA TU HIZO FAINI ZENU ZA 80000/-

    DAVID V

    ReplyDelete
  6. Kamanda mimi nipo kwenye mada ya Tuhuma za Rushwa dhidi ya vijana wako njia ya MOrogoro.

    1.Unaweza kutuhakikishia au unaweza tofautishaje upokeaji wa Rushwa na Upokeaji wa Faini?

    2.Gari la Polisi PT 1997 linaoshwa kutwa nzima likiwa limesimama tu?

    Pale njia ya Morogoro watu wamefuatilia na wamefanya uchunguzi wa kina RUSHWA INALIWA hivyo wewe hukutakiwa upingane na tuhuma hizo na kukaa upande mmoja ulitakiwa kufanya uchunguzi ili ubaini ukweli kabla HUJALIUMBUA JESHI NA WEWE MWENYEWE PALE UKWELI UTAKAPO ANIKWA!

    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  7. Tatizo la watendaji Tanzania ni kubweteka au kudumaa kiakili. Kwamba alama alizoacha mkoloni ni hizo hizo tu hakuna kuongeza zingine wakati hali halisi inaonyesha kuwa kuna hitajio la kuwa na alama kama hizo.

    ReplyDelete
  8. michuzi nashukuruumeirudisha hii. Juzi nilikamatwa kwa kosa hilo na ilibidi elfu 5 intoke

    naomba uiweke juu ili waheshimiwa wa usalama barabarani waione na waje kuitolea maelezo

    ReplyDelete
  9. Leo nimeguswa kwa kweli na swala hili nami nili U-Turn heeeeee mji mzima polisi waliarifiwa...imagine ilikuwa asubuhi namchukua mtoto twende kanisani...polisi mwanamke mfupiiii kama ....ya asubuhi akanisimamisha nami bila kukaidi nikasimama akaingia ktk gari nikasema nina mtoto mdogo hapa ngoja nipeleke nyumbani ndio twende nawe kituoni loooo akaita polisi wote njiani loooo mwanamke namchukia yule kama .....yake. Basi nikaomba msaada mtoto akaja kuchukuliwa mie na polisi kama wanne hadi polisi....heti niwekwe ndani ninaumri wa miaka 60 nikawauliza hamna hata simanzi ...nimeua...hapana nimejeruhi hapana....wakanijibu mama acha leseni yako kesho uje kwa Mpinga....naye bila ya ethics za kazi akakubaliana nao nifungwe au leseni yangu ichafuliwe....utachafua ngapi utafunga wangapi jela zinafunga watu wa U-Turn...wao ndiyo wenye daladala zenye makoso kadha hawawafungi watu wao...aibu Tanzania Police force wanashirikiana katika hujuma nyingi..wanagawana hongo pesa chafuuu....hivi ona kama hakuna umeme polisi hao hawakai ktk traffic lights kama kuna umeme wanajidai wapo busy kama kweli...waongo watupu wanatuudhi watanzania wote...mbadilike...Mpinga hukupewa kazi kwa hilo kama huwezi nenda ukalime kwenu

    ReplyDelete
  10. yamenikuta mie pia natoka peacoak hotel mbele kuna u turn kurudi bibi titi road wakanikamata tukabishana sana alikua mdada tukaenda mpaka trafic nikapaki uani gari tukaenda ofisini tukakuta askari wengine humo akatoa kitabu chake anataka kuandika faini nikapiga simu nikaongea na boss wake.boss wake akaongea nae akaniachia.ukweli sheria hawajui

    ReplyDelete
  11. Kuna baadhi ya heria na miongozo hapa Tz huwekwa ili kuongeza mapato, na wala si kwa sababu za kimaadili au usalama wa watumiaji wa huduma fulani. Mfano, stika ya mtungi wa 'fire extingiusher' ni kwa ajili ya kuongeza mapato, kuna kingozi mwandamizi wa Jeshi la Polisi - Usalama Barabarani aliwahi kulitolea ufafanuzi; na akasema watalisitisha kwa kuwa linaleta mtafaruku kwa jamii.

    ReplyDelete
  12. Madereva wengi hawajui sheria na haki zao na hili ni tatizo. Wengi hukamatwa na kudaiwa rushwa kwa makosa ambayo hawakuyafanya. Kwa mfano kupiga U-turn sehemu ambako hakuna alama inayokataza kufanya hivyo si kosa. Alama za aina hii zinatakiwa ziwepo muda wote. Kama kibao kimeibwa au kugongwa basi mamlaka husika zinatakiwa kukirejesha mara moja.

    ReplyDelete
  13. Ukweli ni kwamba Kamanda Mohammed Mpinga anapaswa kuonewa huruma kwa kuwa anaongoza kitengo ambacho kimeoza mpaka kwenye kokwa kwa rushwa. Huyu bwana hakuna anachoweza kufanya kwa kuwa system yote ni corrupt. Rushwa imeota mizizi trafiki kiasi kwamba kila kamanda anayekuja husubiri tu siku zake za kustaafu zitimie ajiendee zake kupumzika.

    ReplyDelete
  14. Kibao sio jukumu la askari wa usalama barabarani mdau mtoa mada. Lugha yako yaelekea ilimkera askari ndio maana ukapelekwa central hata utishiwe kuswekwa rumande... swala la fire-extinguisher na sticker naona kama vile ni ukosefu wa mawazo. magari mengi yetu ya sticker yet hatuna fire extinguisher. Moto ukitokea sijui sticker itakusaidia vipi... Askari nao wawe na uelewa (wengi wameenda shule cku hizi).. bora fire extinguisher ipo ni nzima ya kiwango au sticker akiiona kwenye kioo ameridhika.... very un-professional. Cku hizi askari wanataka uwe na first aid kit kwenye gari ya binasfi.. ya kazi gani? emergency services that over-stretched au wana lack hata plaster na pamba?... Je ni sheria gani inataka uwe na first aid kit kwenye gari la binafsi... sasa je kwenye pikipiki itakuwaje? tuamke jamani....

    ReplyDelete
  15. mwenye taafifa za alichosema Mpinga kuhusu rushwa pale Bwawani atuwekee hapa ukumbini ili tumjadili, na ikibidi tumpe ushahidi tulionao.

    mdau

    ReplyDelete
  16. Mzee hiyo ya fire-extinguisher sticker ni baala. Sasa sticker inanisaidia nini kwenye kuzima moto?

    ReplyDelete
  17. Nakubaliana na Kahatano iwepo central database bwana unapigwa fine jina lako linaingizwa kwenye system,unaenda kuilipa ndani ya mwezi,kadri unavyozidi kuchelewa na faini inaongezeka.Lazima utaenda kubadilisha road licence tu TRA na huko ndiko utakutana na moto.Wa kulipa papo kwa papo yale magari ya kupita(International Transit) ambao huwezi kukutana nao tena wakishapita.

    PRUDENCE kama ndiye wewe wa Kagondo "ka lugulu",Bukoba naomba unicheki hapa fridokazadi@gmail.com nakufahamu,bado uko UK?

    ReplyDelete
  18. polisi wezi tu na yote kutokana na njaa kali na mishahara midogo na wengine wanatumwa kuchukua hizo rushwa na wakubwa kama wewe jikate zako huna maana wezi wote nyie kudadadeki


    polisi weziiiiii mnakumbuka mliiba mishahara yenu pale polisi msimbazi?

    polisi waliiba mishahara yao pale msimbazi polisi

    na polisi wengine walikuwa wanakaa barabara ya morogoro usiku na bunduki likipita fuso wanasimamisha wanakuuliza maswali ya uongo alafu wanateka gari na kuenda kushusha mzigo wote

    polisi wa tanzania weziiiii majambazi aibu kubwa kwenu mnatia aibu sana kwa taifa la tanzania polisi gani mnakuwa wezi wezi kila idara uwanja wa ndege bandarini kila sehemu mnaiba duh aibu kubwa.

    ReplyDelete
  19. Kamanda wa usalama barabarani,tunasubiri majibu yako kwenye hili na mengine waliyogusia wadau hapo juu..tafadhali ucjifiche..chonde chonde majibu muhimu kama ´ulivyotetea` suala la rushwa..umeanza mwenyewe kujitokeza humu,lete majibu kwani sasa tunajua kuwa ujumbe unafika

    ReplyDelete
  20. kusema ukweli fire extingushire muhimu. ila maaskari wakibongo ni njaa jamani. ukiwa huna kazi sawa sisi wenye haraka inabidi tutoe tu tuanze mbele. wengi shule hawakwenda basi muda hawajui thamani yake...wanakula rushwa na vitumbo ndiiiiii

    ReplyDelete
  21. Kiboko ya trafiki wapenda rushwa Bongo ni Wazungu na raia wengine wa kigeni wasiojua Kiswahili. Trafiki akilipiga gari mkono akiona tu dereva ni Mzungu hapohapo anamwambia aende zake hata kama kuna makosa ya wazi. Hii imekaaje, wadau?

    ReplyDelete
  22. Fire Exstingusher ok inamaana lakini stika maana yake nini!Halafu chakuchekesha ulipie stika halafu ulipie mtungu!angalia ulipia bima unapewa stika sio kulipia bima na stika viongozi watanzania naona pumba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...