Awali ya yote tunakiri gari iliyotajwa hapo juu ni mali ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro.

Mnamo tarehe 30/01/2012 majira ya saa 13:20hrs huko maeneo ya Maseyu kati ya Mikese na Bwawani barabara ya Morogoro/Dar es salaam, Mkuu wa Polisi Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro SP.L.R.Gyindo akiwa na askari F.4857 S/SGT Sunday, WP.4314 S/SGT Blandina, mkaguzi wa magari E.7026 PC Charles, F.1828 PC Yuda, dereva wa gari PT.1997 Toyota Land Cruiser F.4163 PC Masala wakiwa kazini (Doria ya barabara kuu) walikamata gari namba T.831 ASN Scania Bus mali ya kampuni ya Upendo linalofanya safari zake kati ya Iringa na Dar es salaam.

Kwa muda huo wa saa 13:20hrs basi hilo lilikuwa likitokea Iringa kuelekea Dar es salaam likiwa na kosa la ubovu wa kioo cha mbele na dereva wa basi hilo Said s/o Omary, umri miaka 51, kabila mnyamwezi, mkazi wa Iringa anayeonekana katika picha nyuma ya mlango wa gari la Polisi akiwa ameweka mikono kichwani aliandikiwa faini Tshs.30,000/= Notification yenye namba 1962453 ya tarehe 30/01/2012

Pia zoezi la uandikaji wa Notification hiyo ilisimamiwa na F.4857 S/SGT Sunday aliyesimama mlangoni mwa gari kushoto (mlango wa Dereva akiwa na sare).

Na wakati dereva wa basi hilo anatoa pesa za faini mfukoni na kukabidhiwa nakala ya notification, alionekana mtu mmoja akipiga picha kutoka ndani ya basi hilo ambapo kwa wakati ule haikufahamika dhamira yake ni nini mpaka picha hiyo ilipoonekana kwenye BLOG ya www.issamichuzi.blogsport.com (BOFYA HAPA KUIONA POST HIYO) na kuhusishwa na tuhuma za rushwa.

Aidha kwenye picha hiyo watu wengine wawili wanaoonekana mbele ya gari la Polisi ni muosha magari ambaye yuko upande wa kushoto akiendelea kuliosha na upande wa kulia aliyevaa kofia nyekundu ni mfanyakazi wa basi la upendo. Wengine ni wafanyakazi wa basi lingine lililokamtwa kwa makosa mbalimbali.

Kwa ujumla RTO Morogoro na askari wake wakiwa na gari PT.1997 L/Cruiser walikuwa kazini wakitekeleza majukumu yao ya kila siku hususan kufuatilia mienendo ya madereva barabara na kuwaadhibu wale wanaokiuka sheria hizo kama walivyofanya kwa dereva wa basi la Upendo.

Hivyo taarifa ya mwananchi huyo haikuwa ya kweli bali ilikuwa na lengo la kupotosha hali halisi na kujenga hisia kwa umma kwamba kulikuwa na mazingira ya rushwa na hasa dereva alipoonekana akitoa fedha kumpa askari aliyekuwa akiandika faini.

MOHAMED R. MPINGA – SACP
KAMANDA WA POLISI
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 59 mpaka sasa

  1. kamanda asante kwa kufafanunua, ila mimi kama mtanzania na dereva hawa maaskali baadhi yao wanayotabia hiyo ya kutaka rushwa na ukisema unataka uandikiwe faini ulipe wao wanaweza wakakuzushia hata umewatukana...na mkifika kituoni woote wanakuwa upande wa maaskali wenzao na kuanza kukutisha na kukusweka ndani,,, ndo maana WANANCHI WANACHUKIA VYOMBO VYA DOLA badala kuvipenda..asante

    mdau...dereva

    ReplyDelete
  2. Asante Afande Mpinga kwa ufafanuzi.Sisi hatuwachukii askari hawa hata kidogo.Ila kwa wale tunaoendesha magari(acha Dar) safari ndefu za kwenda Mbeya,mwz,Bk,Musoma,nk tukiwa na gari binafsi tunaweza kukusaidia michango yetu ya kinachoendelea humo barabara kuu.Hapa hapatoshi,siyo wote kuna wengine ni wastaarabu sana hata akikumata na kosa anavyoku-approach unaona kabisa yuko kazini,kuna wengine wana majibu ya jeuri,dharau,ubabe,nk

    David V

    ReplyDelete
  3. Polisi mmepinga ila jirekebisheni.
    Inaonekana mmepoteza imani kwa wananchi.
    Aliyepiga picha ana haki ,picha inazungumza.
    Tuache tabia ya kujitetea ,tufanye kazi tuone kama raia watalalamika.
    Punguzeni ajili kila mtu atendewe haki.
    Tutakuja kuweka kamera kwa siku zijazo kwa hiyo mjiandae.

    ReplyDelete
  4. Na bado mtaumbuka sana, ngoja jerry muro arudi kazini muone kama mtaweza kumbambikiza kesi tena. Kamanda ndio maana hatuleti ushahidi wala kesi maana hakuna mtakalofanya kama inavyojidhihirisha hapa
    polisi wa usalama barabarani wanapokea rushwa tena wakati mwingine mpaka wanatia aibu, kama ombaomba.

    ReplyDelete
  5. Kwa Tanzania imekuwa ni Kawaida kwa watu hasa polisi Kulindana!! Kwani Mara nyingi hawa polisi wamekuwa wakipokea Hongo kwa njia ya Kuwalipisha Watu Kwenye Notification Book!! Hii sio sahihi kabisa kwani malipo Halali ya serekali Hufanyika Katika risiti ya Njano!! Je ina maana Hata Mpinga Hajui Hili!! Hii ni Dhairi inaonyesha hiyo ilikuwa ni Rushwa kwani Notification sio risiti halali ya serekali!!

    ReplyDelete
  6. je matukio ya kweli ya rushwa yakitokea mtaweza kutupa maelezo kama mlivyofanya kwa taarifa hii? je hakuna walaji rushwa katika barabara hiyo ya morogoro?

    ReplyDelete
  7. kamanda unawatetea bure vijana wako!
    Rushwa kwa polisi imekithiri na ni aibu tupu,polisi wote kuanzia trafic police na hawa wa kawaida wametuchosha kwa kudai rushwa,hivyo na wewe na hao vijana wako wote mnanuka rushwa,nashauri jeshi la polisi libinafsishwe afadhali waletwe hata wazungu watafanya kazi kuliko nyinyi! JAMANI TUMECHOKAAAAAAA

    ReplyDelete
  8. Unajua mtu mwizi hawezimkukubali na kwa kuwa polisi hukusanya mapato na kugawana na wakubwa zaoi ni vigumu kukubaliana.
    Sina hakina kama sheria inaruhusu polisi kupokea pesa barabarani,ila atafafanua kamanda aliyetoa ripoti hii.
    Ninachokifahamu,mtu mwenye kosa la gari huwa anaandikiwa na kisha kwenda kulipia kituoni na si barabarani.

    Labda tunaomba kupata taarifa ni kiasi gani cha fedha zilishawahi kukusanywa barabarani ikiwa ni sehemu ya adahabu ya makosa ya madreva?

    Sasaa tutawapiga sana picha na tutawaripoti sana,hata wasipochukuliwa hatua tutaendelaza vita.
    Pilai kulikuwa na sababu ipi nya kuogopa kupigwa picha?Policy ni ya public na kama unafanya kazi ya wema na ya public kwa nini uogope kupigwa picha?
    POLISI KWA KUWA WALA RUSHWA NDIO WAMELIFIKISHA TAIFA HAPA TULIPO.WALA HATUKWA NA HAJA YA PCCB ILA KWA SABABU YA KUSHINDWA KWA JESHI LA POLISI

    ReplyDelete
  9. MTAWALEA MAFISADI MPAKA LINI?SHAME IN YOU.

    ReplyDelete
  10. Mhe.KAMANDA,

    NI VIGUMU KUTOFAUTISHA KATI YA MAPOKEAJI YA FEDHA YALIYO KATIKA MAZINGIRA YA RUSHWA NA UPOKEAJI WA MALIPO YA FAINI:

    TAARIFA IMEELEZWA KUWA WATU WAMEFANYA UFUATILIAJI NA WAKAGUNDUA HUO MCHEZO WA WANAUSALAMA BARABARANI WA KUWAWEKA WAOSHA MAGARI WAKIENDELEA HUKU RUSHWA IKITOLEWA NA KUPOKELEWA.

    WACHA KUWA TETEA HAO MAAFANDE KWA TAARIFA YAKO WAPO WATU WAMESHA CHUKUA MATUKIO YA RUSHWA YA HAPO WAMEREKODI VIDEO ZAKE WAKIWA KATIKA MAGARI YENYE TENTED.

    HII TAARIFA YAKO NI YA KISANII KULIKO UHALISIA.

    JE GARI YA POLISI INAOSHWA KUTWA NZIMA?

    TAFADHALI WAWAJIBISHE VIJANA WAKO WAJIREKEBISHE!

    USIMTISHE MICHUZI KWA MAONI HAYA KAMA UNATAKA WASILIANA NA MIMI MOJA KWA MOJA KWA NAMBA HII CHINI.

    TEL: NO. 022 2116679 ELEZA KUHUSU TUHUMA ZA RUSHWA KWA IDARA YA USALAMA BARABARANI MOROGORO ZINAVYOWAKABILI.

    ReplyDelete
  11. hehehehehe, mngeacha ipite tu. Hivi Kamanda kweli unafikiri askari wako watakwambia walikuwa wakipokea rushwa??

    ReplyDelete
  12. Kuepusha hali hii ni bora polisi waache kukusanya pesa wanapomkamata mtu,cha kufanya ni kumpa mtu notisi ya kulipa baada ya muda fulani labda wiki 4 kwenye ofisi za mahakama, hii itaepusha tatizo la rushwa japo kamanda wa polisi anataka kukana na polisi wata concetrate na usalama wa raia na sio kukusanya faini.

    ReplyDelete
  13. afande mpinga,mimi binafsi sitakushangaa na wala siwezi kuanza kuumiza kichwa changu kuyafikiria hayo uliyoyasema wewe kwani hii si mara ya kwanza kuona viongozi wetu wakiwatetea wala rushwa kwani ni wenzao, walalahoi tulie tu kwa hili na mengine mengi tu...mungu awasamehe bure tu...na ipo siku.
    kwaheri

    ReplyDelete
  14. Ushauri wa bure kwa ndugu zangu polisi,hizo faini muziandike hadharani ili wananchi tujue na tuwasifu kwa kazi mnayofanya..ukweli ni kwamba hamuaniki,hivyo kuweni wawazi kwenye kazi zenu..kwani hiyo faini mngeandikia nje kuna ubaya gani mpaka mjifiche ndani ya gari??

    ReplyDelete
  15. Impressive statement, well done.

    ReplyDelete
  16. Mi naona kila kitu kuhusu hii nchi yetu inatilisha imani, kwanza yaani huyu mkuu wa polisi yaani anatetea kabisa uozo bila hata haya??? hizi rushwa zitaisha vp??
    YAANI FAINI ZINALIPWA KIHOLELA HIVYO...SI NDO MIONYO YA RUSHWA INAONGEZEKA!!!

    ReplyDelete
  17. Kamanda,
    For sure unajua ulichokiandika ni kujikosha tu, lakini ukweli unabaki pale pale, ya kwamba ninyi ni wala rushwa wazuri sana.

    ReplyDelete
  18. Mimi nakanusha kitendo cha askari anapokamata gari kwanini alipwe pesa yeye direct badala yakumwandikia mtu makosa na yule mtu akalipe mahali panapohusika. Mbili askari wabarabarani wanapo mkamata mtu kwanini wanarudi kukaa kwenye magari yao mtu awfuate badala yakuongelea palepale alipomkamata mtu hayo ndio mazingira ya rushwa. Na tatu maaskari hawa wanapokukamata wanakaripia watu sana nakutishia watu fanya haraka kutoa chochote lasivyo tunakuandikia makosa nautalipa zaidi ya hii. Mimi binafsi nime experince hii bongo hivi karibuni ilikuwa tarehe 29/1/2012 maeneo ya mikocheni kwenye kona yakwenda cocacola na clouds fm mida ya saa tano mchana. Kulikuwa na maaskari wanne watatu wavulana na mmoja mwanamke wamesimamama kwenye kona kama unaenda kwa Maznat saloon wanasimamisha magari. Mimi sikuwa na wasiwasi sababu nilikuwa najua kama kuna kosa lolote nitaelezwa kisha kama kunataratibu zozote za kulipa nitalipa. Nilipo simamishwa nikasimama nikajua askari atanifata kunieleza kanisimamishia nini nikaona kimya anaendelea nakusimamisha magari mengine kisha baada kama ten minutes akaja akasema sasa wewe hushuki kuja kuleta vitu vyako. Minikasema nilete nini maana mimi sijui nimgeni hapa nanimezoe ninapokamatwa nchi za watu wananieleza nini kimefanya nisimamishwe. Akasema lete lesseni na kadi ya gari nikampa kisha akaenda mbele yakioo akasema stika yako imeisha 2days ago mi nikasema sikujua sababu nilikuwa natumia gari ya nyumbani. Nikasema sasa taratibu inakuwaje akasema pesa ni nyingi sana utalipa nikikuandikia tena boss wake alikuwa amekaa pembeni nakitabu akaanza kufoka anataka tumwandikie kosa litakuwa si moja tena iliakome. Pembeni yake kulikuwa na askari wakikie nae amekamata bajaji anamfokea mwenye bajaji kwakumtisha atamwandikia kama analeta jeuri. Basi mwenyeji wangu akatoa pesa akampa huyo askari kisha akatuachia. Nilishangaa sana ninaushahidi wote, wa jina lake na namba zao wote niliandika sasa huyo kamanda wapolisi wa morogoro asibishe. AKIBISHA mimi nitafanya research nanitatoa documentary CNN AU BBC ndo ataamini maana wanafanya live tena kwakung'ang'anza. Mimi ningependekeza kama mtu anakosa andikiwe na akalipe kwenye jiji na si polisi au kumpa mtu pesa live ni hatari kwa usalama wake na mtu yeyote.

    ReplyDelete
  19. kamanda MPINGA vizuri umeeleza ila itakuwa vizuri zaidi maaskari kuacha kujificha kwenye magari , kwani kama dereva analipa faini kwanini wasiweke kitabu hata kwenye bonet la gari na kumuandikia huku abiria wakiona kuwa inaandikwa faini ? wanavojificha au kuwavuta madereva pembeni ndo maana wanaonekana wanapokea RUSHWA... HAYO NI MAONI YANGU

    mdau kariakoo

    ReplyDelete
  20. KAMANDA naomba nikuulize kwani ni KOSA kumpiga askari picha ?

    JAMANI HEBU NIFAHAMISHENI MIE MANAKE SIJUI, YAANI ILI UMPIGE PICHA ASKARI NI LAZIMA UWE MWANDISHI WA HABARI AU VP ? NISAIDIENI HAPA KIDOGO SIELEWI

    ReplyDelete
  21. askari wamezidi kupokea rushwa wanatia doa jeshi zima

    jirekebisheni wajameni

    ReplyDelete
  22. mimi binafsi tangu nimeanza kuendesha gari nimeanza kuwachukia trafiki hata sijui imekuwaje na nimeanza kuwachukia, nikiona wanavyosumbua madereva najua na mimi siku moja yatanikuta , maana wakikusimamisha lazima wakutafutie kosa hata kama huna kosa utaambiwa tu una kosa aaaahhh tumechoka mmezidi, UKWELI UNAUMA

    ReplyDelete
  23. Ni faini ya namna gani inayolipwa chini ya MWEMBE, ndiyo maana raia wanapoteza imani.Askari sio muhasibu yeye iweje apokee fedha chini ya mti? Kazi ya polisi ni kutoa ticket ya faini sio kupokea fedha. Huu ni wizi na hata mujaribu vipi kujisafisha ukweli unabaki pale pale.RUSHWA ITATUMALIZA.

    ReplyDelete
  24. Sawa. Inawezekana hawa hawakuchukua rushwa, lakini ukweli ni kwamba barabara zetu kuu zimejaa trafiki ambao kazi yao pekee ni kudai na kupokea rushwa kutoka kwa madereva. Natoa changamoto kwa Mpinga kufanya utafiti ulio rahisi. Nashauri siku moja avae kiraia na kusafiri mchana kwa gari lisilokuwa la Jeshi la Polisi kutoka Dar es Salaam na kwenda, mathalan, Arusha au Mbeya. Atajionea mwenyewe jinsi tatizo hili lilivyokithiri. Yaani ukiona sehemu trafiki wanasuburi pembeni ya barabara basi ujue hicho ni kituo cha kupokea rushwa.

    ReplyDelete
  25. Nilienda znz new year, tutakodi tax na wenzangu kwenda Masada ya mbali kidogo kuyoka town kwenye dolphin. On the way tukakutana na askari wakatusimamisha,dereva akatoka noti sikumbuki shs ngapi akampa, askari akasema EEG sikuku yang eehh,ntukaondoka.nilikuwa kiti cha mbele wenzangu hakuna aliona hichi kitendo. Ila sikukaa Kimya nikamuuliza kaka vipi lie hela ya nini umempa askari? Akasema ndio kawaida bila ivyo utazungushwa kwahiyo ye Kilauea akipita lazima ache kidogo.Doh nikachoka! Cha kushangaza wakati wa kurudi,tukasimamishwa tena. Wakati huu partner wa Yule askari wa kwanzaakatufuata,dereva akamwambia nilishampatia mwenzio! Yule wa kwanza wakati hue hat a hatuangalii, kaka a mbali, ila partner wake akasema hay a nendeni! Nikachoka- yaani rushwa imezoeleka imekuwa kama sheria!

    ReplyDelete
  26. Michuzi,mwulize kamanda kama fines zinalipwa barabarani,utuletee jibu tafadhali,hiyo notice wanaweza kuiandika hata jana.

    ReplyDelete
  27. taarifa ya TAKUKURu ya mwishoni mwa mwaka jana inasema kuwa ktk taasisi za serikali jeshi ra porisi ndo vinara wa rushwa HONGERENI....!

    ReplyDelete
  28. Kamanda Mpinga usibishe kwa kutetea uozo wa Askari wako, kwa kuwa jeshi la polisi linanuka kwa rushwa, nina ushahidi wa picha na movie ambazo nilizirekodi barabarani za Askari wako katika vituo vya Tukuyu na Tanga na nina mpaka majina ya hao Askari na namba zao yaani hapa unachokiongea ni uongo ambao umepewa, na jina lako kutumika tu kny hiyo taarifa.Mfano ktk movie nilizorekodi ninaweza kutoa picha ya anapoomba rushwa kisha ukakanusha ndipo mimi nikakuletea movie sijui utauficha wapi uso kwa aibu. Mfano katika kituo cha Tukuyu wamekaa na vijana wanabrashi viatu lkn hao vijana huwa hawaonekani siku polisi wakienda vituo vingine wakiwa barabarani,yaani Jeshi la polisi halina tofauti na "Matonya" inapofika mahali Askari anaomba mpaka anunuliwe kilo X ya nyama ni aibu kwani mashahara anapeleka wapi? Naweza kukuletea picha ukanushe ndipo nikuletee movie hakuna cha kuchakachua sauti. Tanga nako pia niliwarekodi wakipokea rushwa na nina clip nyingi tu za polisi wa barabarani nitazituma kwa Michuzi ukanushe ndipo nikuletee movie tuone kama utakanusha pia. Kuna moja niliirekodi Tanga na nilikuwa kny basi nilichokifanya nilibana wireless mic kwa utingo na walipokwenda kny gari mimi nikaanza kurekodi sauti ilikuwa clear sana yaani hakuna cha notification ni kupokea rushwa tu. Kamanda Mpinga naomba kama una email na wewe nikutumie copy uone uozo uliopo kny kitengo chako. Niko jikoni kuandaa documentary ya jinsi askari wako wanavyopokea rushwa hasa kwa vituo hivyo vya Tukuyu na Tanga.

    ReplyDelete
  29. Waddle waddle the duck went to the lemonade stand, waddle waddle!

    The duck ask do you sell grapes, waddle waddle! the lemonade man said no we dont sale grapes, we only sell cold lemonade! Waddle waddle

    the duck went away til the next day waddle waddle

    the next day the duck come back again and ask the lemonade man, do you sell any grapes? the lemonade man said we dont sell any grapes.

    the duck went away til the next day waddle waddle

    the next day the duck come back again and ask the lemonade man, do you sell any grapes? the lemonade man become very angry and say we dont sell any grapes but I will take you to the groceries store and get you grapes!

    The lemonade man took the duck to the grocery store and buy grapes, and he gave one to the duck waddle waddle!

    The duck told the lemonade man no thanks, can you ask the lady if they sell lemonade in the grocery waddle waddle!!

    AND THAT IS THE STORY OF THE POLICE AND THE PUBLIC WADDLE WADDLE!!!

    ReplyDelete
  30. AAAAA KAMANDA MPINGA WEEEE....UNAJISAFISHA KWA TOPE UTATAKATA KWELI?HAO TRAFIC TUACHIE WENYEWE WANANCHI NDIO TUNAWAJUA WEWE HUWEZIAMINI HATA TUKIKUELEZA,UKO MBALI SANA NA HALI HALISI MANA HAIWEZI KUKUTOKEA YANAYOWATOKEA WANANCHI......WEWE FANYA SEHEMU YAKO USTAAFU YAISHE ILA HUNA JIPYA UKIWATETEA HAO WANANCHI WANAKUONA KAMA CHIZI TU KWAKUWA UNAJARIBU KUWAPELEKEA KWENYE MBINGU YA KUFIKIRIKA WAKATI UHALISIA WANAUJUA.HAO TRAFIC HATA AIBU HAWANA KWENYE KUPOKEA RUSHWA HAKUNA ASIYEJUA LABDA NYIE TRAFIC WAKUBWA LAKINI KWAKUWA NANYI MLIKUWA HIVYOHIVYO KABLA YA KUWA WAKUBWA LAZIMA MLINDANE.

    ReplyDelete
  31. wakukanusha hapa upande wa serikali siyo jeshi la polisi, lkn kwa kuwa serikali inaajiri polisi kwa mishahara ya chini, haiwezi kuzuia hili, pale polisi wanapoamua kujitfutia riziki kwa njia nyingine badala ya mgomo, kwani polisi akigoma moja kwa moja kazi hana, sasa ataendeshaje maisha yake? Rushwa polisi ni moja utashi wa yeye kujiunga na jeshi hilo kwa easy money u can get it! watznia ni wanyonge sana, lkn mimi naamini hakuna lililo na mwanzo likakosa kuwa na mwisho!

    ReplyDelete
  32. Kwani kamanda huwa tunalipa pesa kwa notification au tunalipa pesa kwa risiti za serikali ERV ambazo ni rangi ya orange kama si manjano, ambazo ndio zinaonyesha malipo halali, naomba nieleweshwe hapo maana hizi notifications zipo nyingi feki na lengo la hizo ni kwamba ulipe hiyo faini na upatiwe risiti-wizi mtupu.

    ReplyDelete
  33. Kweli! Polisi wanapokea faini, pesa hizo zinafika! Wahasibu maofisini wanafanya nini? Lini hizo pesa zitafika......wacheni kutudanganya.....walarushwa wakubwa! na Motoni mtaenda!

    ReplyDelete
  34. Kamanda Mpinga bwana! Notification zinaandikiwa ndani ya gari kwenye mapaja/steering? Mimi nafikiri sehemu nzuri ya hilo jitabu lenye notifications kuwekwa ni juu ya boneti, yaani hapo hata mwandiko haupindi, au? Umeshawahi kusikia mtu anahukumiwa kwa ushahidi wa 'mazingira', haya kwa hawa wateule wako je? Natamani ungekaa kimya kuliko ulivyojibu, umezidi tu kupipaka uchafu kwa kuogea maji machafu.

    Anyways, tumewazoea kuteteana.

    ReplyDelete
  35. Kamandaaa, Mungu anakuona lakini!

    ReplyDelete
  36. Ila hili jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani,wamezidi,inabidi wabadilike,sio kuutetea uozo uliopo,hata ukiwakuta wale wanaokuwa na vifaa vya kupima mwendo kasi wa gari aka tochi,wanatabia ya kubambikizia mwendo uliokuwa,ilishanitokea nilikuwa nasafiri kutoka mbeya naendesha gari ndogo,ilifika sehemu kuna kibao kinaonyesha mwisho speed 50,nikapunguza nilikuwa 45,nimefika kwa mbele kidogo trafick akanisimamisha,akaniambia nilikuwa na speed 95,nikamwambia sio kweli,akaniambia nitaingia tuu kwenye anga zangu,nikabaki kumshangaa,kuna trafick wanafanya kazi kama miungu watu,lazima wabadilike,ukija kwenye haya mabasi lazima wachenji hela kila kituo anaposimamishwa anaacha kwa trafick hela,hiyo ndio kazi yao,hakuna jipya kwa hawa jamaa

    ReplyDelete
  37. Mpinga aachie kazi yeye ndiye aneyewatuma polisi pesa ushahidi upo kwani nao wanasema wakibanwa na wajuaji....shame on you! Nyerere you died tooo soon we need you now more than then!

    ReplyDelete
  38. Mimi nina shangazwa ha hawa polisi: Inakuwaje gari ya polisi ikaoshwe na waosha magari wa vichochoroni? Nijuavyo mimi kazi kama hizi hufanywa na mahabusi katika vituo vya polisi. Na siamini kwamba sehemu hiyo kuna magari mengi ya kumvutia huyo mwoshaji,kwa hiyo wanataka kutwambia alifuata gari hiyo ya polisi tu? Pili,kama polisi wanafanya kazi huku wamezungukwa hovyo na watu namna hiyo umakini unakuwepo kweli? Vile vile kweli gari ya polisi inaachwa watu waizunguke ovyo ovyo tu? Gari si ni ofisi? usalama upo wapi? Kwa hiyo ninachokiona mie katika picha hii ni mazingira yalioandaliwa mahususi kwa kupokea rushwa full stop. Maelezo ya Mpinga ni mwendelezo ule ule wa watu kufikiri bado waTanzania ni wadanganyika. Kwa kweli kwa hili nampongeza alotoa picha hii, tumewabamba...Mpinga lazima utapinga tu si ndo jina lako?

    ReplyDelete
  39. Hivi huyu Mpinga inamaana hajui the way askari wake wanavyochukua rushwa? hawa traffic na wale waliopo kwenye doria na magari na wale wa pikipiki ni wachukuaji rushwa wazuri tu, Inawezekana hao uliowataja walikuwa kweli kwenye doria na walifanya kazi yao kwa usahihi lakini hao askari hawapaswi kubeba taswira ya jeshi zima la polisi kuwa hawachukurusha lahasha, kwa kukujuza tu askari wako wanalamba mkwanja kila kukicha na ndo mana unaona kila mtu anamaisha mazuri sasa hivi karibu traffic wote wanadrive magari yao binafsi tena mazuri haswaa sasa hiyo mishahara mnayolipana inamuwezesha kumili vitu kama hivyo?

    ReplyDelete
  40. Kamanda Moinga, siku nyingine waambie hao askaei wetu waweke kitabu kwenye boneti la hiyo Cruiser, ili notification iandikwe abiria tukiwa tunaona. Utakuwa umepunguza sana maswali na wasiwasi wa abiria

    ReplyDelete
  41. anonymous wa 07:09:00 nina kuunga mkono na nyie wengine wote huo juu, mnachokisema ni kweli na kipo nahuyo afade mpinga nakifahamu, i guess peleka BBC na CNN labda watashika adabu, vijana wake Mpinga wengi hawajui sheria wanajua kukamata na kuomba rushwa, wanafikiri hela inapatikana kirahisi.

    ReplyDelete
  42. asante sana kwaufafanuzi wako ulioutoa, ila binafsi ningependekeza kuwa suala zima la ulipaji faini lingefanyika sehemu maalum kama vile Bank/mojakwamoja kwenye Account ya serikali au kituoni ilikuondoa visingizio na mikanganyo ambayo inajitokeza mara kwa mara, tuseme labda hao Askari walichukua au hawakuchukua hiyo rushwa how could someone prove that? pia how comes pesa ya serikali iingie mifukoni mwa hao Polisi kwanza, unatuthibitishia vipi kama itafika pesa yote?

    ReplyDelete
  43. Asante kamanda kwa ufafanuzi wako, ila siku hiyo hiyo na mimi nilipita hapo na nilikamatwa na nikatoa rushwa ya sh elfu kumi ili kuondoa usumbufu wa polisi wako, maana ukitaka kulipa hiyo mnayoita notification unaanza kuletewa maneno mengi sana ndio maana sisi wengine huwa tunataka kurahisisha maisha, unawalipa tuu rushwa yao unaendelea na safari ili kupunguza mlolongo wa maneno.

    Samahani kwa kukiri kuwa nilitoa rushwa ila ndio hali halisi ya bongo ili mambo ya ende, hasa kwa Mapolisi.

    Hapo kamanda unawatetea tuu ukweli tunaujua sisi waendesaha magari wa safari ndefu mara kwa mara, lazima uweke au utenge hela kwa ajili ya kuwalipa Polisi njiani na sio ya Notification bali ya rushwa.

    Nawakilisha...

    ReplyDelete
  44. Mimi hili gari kila nikipita hii barabata nalikutaga hapo hapo....nina wasiwasi na maelezo ya Afande....kujitetea kwingi sana lkn ukweli ndio huo. Kwani nani asiyejua wanachokifanya polisi wa barabarani? Watanzania wote hata wanafunzi wanajua....Poleni sana wazee wa usalama, badilikeni sasa.

    ReplyDelete
  45. Aliyepiga picha was quite right kutokana na mazingira yenyewe yanaonyesha wazi kuwa kuna utata. Hii picha itumike kuwafundisha waache tabia mbaya ya kulazimisha na kuomba rushwa. For sure Police force is leading in corruption!!

    ReplyDelete
  46. mimi nimekamatwa na askari mmoja wa kike kaaangalia kila kitu anasema fresh ila anasema eti ile fire tingisha yako ime-expire angalia date..hii mpya!!!

    ReplyDelete
  47. vijana wenye machungu ya nchi tuishio ughaibuni tunajiandaa kurudi nyumbani na nguvu mpya na vitendea kazi vya kisasa kazi kwenu wala rushwa

    tumejipanga kikamilifu kuja kupambana na nyie wala rushwa kuanzia polisi wa barabarani vituoni mpaka uwanja wa ndege

    tunakuja na vifaa vya kurekodi video picha na sauti
    safari yetu na utendaji wetu utasaidiwa na wakubwa wenu wa kazi tutafanya kazi na wakubwa wenu mguu kwa mguu

    tumechoka na wizi wenu wa kudhurumu haki za raia shame on u mnatia aibu serikali ya tanzania

    ReplyDelete
  48. Wadau, nimechelewa kweli kuipata taarifa hii. Mimi niliyepiga picha hiyo nipo. Anachokisema Kamanda ni kuudanganya umma. Ile faini iliyopigwa, dereva hakuilipa hapo hapo. Alichofanya ni kuwapa fedha kidogo ili aachiwe aendelee na safari, kisha adhabu ilipwe baadaye. Huyo dereva alikuwa mmoja tu, lakini kwa muda wa dakika kama 10 tulizokaa hapo, ilikuwa ni aibu tupu. Watu wengi walishuka na kuwapa fedha wakiwa ndani ya gari hilo bila kushuka. Hawa polisi ni wala rushwa wa hali ya juu. Ushahidi zaidi ninao. Lakini polisi kwa kuteteana ni kawaida kabisa. Bado nitaendelea kuzileta nyingine nyingi.

    Mdau mchukia rushwa

    ReplyDelete
  49. Hawa watu wanatufanya wajinga kwa kutengeneza stori za kutudanganya. Wajifunze kwa maafisa habari wa Muhimbili na wizara ya Afya kwamba hata ukifabricate story na kumdanganya mtu akiwemo waziri mkuu kumuandalia hotuba mbovu, mwisho wa siku ukweli utajulikana tu. Mimi nimewahi kugongwa kwenye taa za kuongozea magari na afisa mmoja wa shirika kubwa tu hapa nchini aliyetembelea taa nyekundu wakati tumeruhusiwa sisi lakini cha kushangaza mimi ndiyo nilishitakiwa baada ya jamaa kuahidi mshiko kwa askari wa kituo cha ubungo terminal. Kuna kajamaa kanaitwa Deslei pale Ubungo na Mwenzake mfupi mweusi ni wabaya sana kazi zao ni kuuza kesi kwa matajiri huku wanyonge wakiumia.
    Mi namshangaa sana bosi mkubwa wa polisi kusimama kutetea kwamba kinachofanyika hapo siyo rushwa. Huu ni usaliti kwa watanzania. Yeye alitakiwa kuchunguza na si kutengeneza stori. Tushawazoea hao ukiwaitia tatizo kama ajali ya pikipiki au baiskeli wanatupiana mpira nani aende wanasubiria za magari sana sana ya biashara. Wenzao ukiwaitia tukio labda la mauaji wanaweza kukaa hata masaa sita bila kufika lakini dili ya magendo ni dakika tano au kumi kimeshaeleweka.

    ReplyDelete
  50. kiufupi short and clear HATUWAPENDI NA NI WALA RUSHWA MTAKE MSITAKE THAT IS FACT

    ReplyDelete
  51. jamani mimi mwenzenu nilikuwa sijui kama ile karatasi nyeupe ukipewa hutakiwa kutoa pesa , eeehh michuzi asante sana umenipa elimuleo nilikuwa naibiwa siku zote mi najua ile ndo faini kumbe !!! yarabiiiii mtumeeee duh nimechoka hadi basi

    ReplyDelete
  52. Mimi mnachonikera Polizi ni kumwelezea mtu kwa kabila lake!

    Kwani watu wanaweza kuwa na majina sawa wakawa na makabila tofauti? Sasa nini umuhimu wa kuelezea kabila la mtu au dini yake??

    ReplyDelete
  53. LIBENEKE OYEEEE !!! MITHUPPU OYEEEEE...KAMANDA MPINGA OYEEE.. WALA RUSHWA OYEEE !!!

    MESSAGE DELIVERED!!!

    ReplyDelete
  54. Hebu sikieni hii: BASI LILIKUWA NA UBOVU KIOO CHA MBELE!! HALAFU ASKARI WAKALIRUHUSU KUONDOKA NA ABIRIA NDANI!! Jamani basi limegundulika kioo cha mbele halafu askari anaruhusu liendelee na safari????!! kuna askari hapo:

    ReplyDelete
  55. Ukienda kuangalia hiyo notification utakuta imeandikwa 'To pay 30,000' au 'Paid 30,000' bila kupewa risiti. Huu ni wizi wanaoutumia askari wengi wa barabarani. Mie niliandikiwa hivyo na kuwagomea, nikapelekwa kituoni nako nikaambiwa anaeandika risiti katoka na kulazimika kumsubiri kwa saa 3. Nani ana muda kama huu kama sio kuwapa watu ugumu ili waiachie polisi na kufaidika na pesa za bure.

    ReplyDelete
  56. ASKARI WATANZANIA NI AIBU KWANZA HAWAAMINIKI 2 WANATETEANA UONGO WANAWEZA KUKUWEKA NDANI BILA SABABU KWA KUSINGIZIA KESI WAO WAJITETEE.

    ASKARI HAO KWANZA TIZAMA WALIVYO WAVIVU WAMEENDA KUWEKA GARI CHINI YA MUEMBE UKIWAULIZA KWANINI WATASEMA TULIWEKA GARI LIOSHWE KWANI KAZINI KWAO HUKO HAKUNA WAFANYAKAZI WA KUOSHA GARI? KAZI KUKAMATA NJIA ZENYEWE MBOVU KIASI VIOO VIVUNJIKE.

    ReplyDelete
  57. Kamanda umejiaibisha tu na utetezi wako wa jumla. Hilo jeshi linahitaji mabadiliko na tatizo kubwa ni kuwa askari wengi ni watoto au ndugu wa wakubwa wa polisi ma walio kazini au wastaafu. OCD gani anaweza kumchukulia hatua mtoto wa RPC?? anajipenda?? Traffick nao wanalazimika kuchukua rushwa sababu wanasubiriwa kupeleka chochote kwa wakubwa na kila chombo anachopewa traffick kufanyia kazi mfano pikipiki, gari kina bei yake ya kupeleka na kila eneo la kzi lina bei pia. huo ni ukweli mimi ni polisi na nimewahi kuwa traffick nayajua

    ReplyDelete
  58. Samahani ndugu zangu waTanzania, nakubalina na yote mliyoyasema. Hili swala la rushwa tumeshawi lizungumzia hapo zamani. Narudia niliyosema awali. Kwanza nyie mnawaonea Polisi bure, siyo pekee yao wanaouchukua rushwa, halafu rushwa wanayochukua ni cha mtoto ukifananisha na mahela viongozi wachache wanayoibia Taifa letu masikini. Ndio wote tunalalamika kuhusu rushwa,ni unafiki mtupu. Rushwa ni kama kansa kwetu. Nani anaweza kusema ameishi bongo maisha yake bila kutoa chochote ili asaidiwe kwa haraka? Au ajatumia jina la fulani au cheo chake?!! zote ni rushwa. Rushwa kila mahali bongo-tusemage ukweli tu. Tanzania nzima itabidi ibadilike kwa sisi kuua rushwa.

    ReplyDelete
  59. We anony wa Thu Feb 09, 10:38:00 PM 2012

    unatupeleka kule kule kwa wabunge kuhalalisha posho kubwa kwa sababu katika mashirika watu wanalipana posho kubwa. Hairekebishi kosa kwa kufanya kosa lingine( Two wrongs doesn't make it right! nasisitiza kwa kiinglishi) Waache wachambwe kwa sababu ukikataa matakwa yao ya kuwapa hela bila risiti kwa sababu umefunga mkanda utawekewa bangi na wanaweza hata kukukwida ili ukipaniki wakuongezee mengine kwamba umepiga askari. Kwa hiyo hata kama unajua mara nyingine unawekwa kwenye mazingira ya kutoa rushwa. Kwanza utalalamika kwa nani kwa sababu aliyewatuma ni bosi wao na ndo maana anasimama kuwatetea kama alivyofanya? Anaogopa likisanuliwa atagundulika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...