Uzinduzi wa jengo la utafiti wa magonjwa, madawa na chanjo mbali mbali la Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) tawi la Bagamoyo utafanyika rasmi siku ya Ijumaa tarehe 3/Februari/2012.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa IHI ndugu Mbarwa Kivuyo inasema ufunguzi huo utafanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Ufunguzi wa jengo hilo utakuwa utawezesha IHI kufanya tafiti daraja la kwanza (Phase One clinical trials) za chanjo, madawa na magonjwa mbali mbali ukiwemo ukimwi, kifua kikuu na malaria. Hadi sasa ni Afrika Kusini tu ndiyo inaendesha tafiti za afya katika daraja la kwanza, hivyo maabara hii itakayozinduliwa Ijumaa itaweka Tanzania katika ramani ya dunia katika suala la tafiti za daraja la kwanza.

Jengo hilo ambalo sehemu yake ni hospitali na maabara ya kisasa, lina uwezo wa kuwalaza wagonjwa 30 kwa wakati mmoja.

Ujenzi huo ulioanza katikati ya mwaka 2009 eneo la Kingani nje kidogo ya mji wa Bagamoyo, umegharibu takriban shilingi bilioni moja ambazo ni msaada kutoka Malaria Vaccine Iniative (MVI) na serikali ya Norway. Kazi za utafiti zitakazofanyika katika jengo hilo na viwango vyake vitafanya kituo hiki kuwa miongoni mwa vituo vichache Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katika miaka ya hivi karibuni, Taasisi ya Afya Ifakara imepanuka kutoka ofisi moja iliyoanzishwa mwaka 1949 katika mji wa Ifakara wilayani Kilombero hadi kufikia ofisi saba zikiwemo za Dar es Salaam, Rufiji, Mtwara, Kigoma, Dodoma na wilayani Bagamoyo. Aidha IHI inaendesha vituo vidogo katika wilaya 27 kote nchini vikiwa na kazi ya kukusanya takwimu za hali ya afya na huduma za afya katika ngazi ya vituo vya afya na katika jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...