Afisa Uhusiano wa TACAIDS Grory Mzirai akitoa mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandaji wa vipindi vya Redio na Watangazaji kwa Kanda ya Mashariki inayofanyikwa kwa siku mbili kwenye hoteli ya Kibaha Confernce Center Maili moja Mjini Kibaha.Waratibu wa Ukimwi katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Lindi na Mtwara wapo kwa ajili ya kuwaelezea masuala mbalimbali washiriki wa semina hiyo,  kuhusu maambukizi ya ukimwi na kupambana na janga zima la Ukimwi linalotishia jamii na nyanja mbalimbali za  kiuchumi nchini Tanzania kutokana na kudhoofisha nguvu kazi ya Rasirilimali watu.Semina hiyo imeandaliwa na Taasisi ya kuzuia ukimwi TACAIDS ikishirikiana na kampuni ya Masoko Agency ya jijini Dar es salaam  na tayari imeshafanyika katika kanda Kaskazini Arusha, Kanda ya Ziwa Mwanza, Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya na sasa ni Kanda ya Mashariki Mjini Kibaha
 Meneja Mawasiliano na Mafunzo wa kampuni ya Masoko Agency,Lugano Henry akizungumza katika semina hiyo inayofanyika kwa siku mbili katika hoteli ya Kibaha Conference Center mjini Kibaha.
 Mmoja wa watoa Mada ambaye pia ni mtangazaji wa ITV Bw. Godwin Gondwe (kushoto)  akiteta jambo na Meneja Mawasiliano na Mafunzo Lugano Henry.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini masuala mbalimbali katika semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...