Ankali nauza gari hii kwa sababu mwezi Februari hii nitasafiri kwenda UK kula ndondos, sasa sina namna ila ni kuuza ili hiyo fedha inisaidie kumudu gharama za maisha nikiwa kwa Mama, bei ni 8,400,000. Aina ya
gari ni : -

•       Toyota Raum ya mwaka 1998 (Rangi nyekundu nje na ndani Kijivu)
•       Imetembea kilomita 49,720.
•       CC 1490
•       Ina bima ya Real Insurance/ Comprehensive.

Mnunuzi makini nipigie kupitia namba hii: -             +255754355577      
Ahsante! Ankali na kazi njema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. mil 8.4? Good luck mdau

    ReplyDelete
  2. Umeanza mbali mno. Gari la mwaka 1998 kwa 8.4ml??????? Kudadadadeki!!!!! Kila la Heri!!!!

    ReplyDelete
  3. hivi watanzania tuaacha lini kudanganyana? hivi tukiwa wakweli tutaharibu nini?

    hivi kweli wajemeni kuna gari ya mwaka 98 ikatembea chini ya km elfu hamsini 50?

    mimi nipo huku ughaibuni na kazi yangu ni kununua magari na kusafirisha lakini magari ninayonunua ni kuanzia mwaka 2004 mpaka 2008 na lakini kupata gari iliyotembea km buku 50 ni shida sana

    nyingi ni kuanzia km buku 70 na kuendelea

    au tuseme magari ya huku yanatumika sana?

    na hiyo imetengenezwa bongo?
    itakuwa imetoka kwa wenzetu sasa wenzetu hawajaitumia mwanzo?

    anyhow nisikulaumu mimi ni mnunuzi

    milioni 5 nikupe fasta fasta ukaombe ukimbizi uk

    nijibu hapa kabla sijapoteza hela zangu kupiga simu


    mdau mtoto wa fisadi wa serikali

    ReplyDelete
  4. Hiyo bei ni kubwa mno kwa gari mzee kama hiyo.

    ReplyDelete
  5. Mdau bdo gari yako unaipenda kama vp, iweke bandani ukishakula nondos,ukirudi utaikuta.

    ReplyDelete
  6. Japan kuna gari za mwaka 1997 lakini zimetembea KM.41000,ni matumizi tu,suala miaka na KM umechemsha wewe hapo juu.Nenda kwenye "tours" uone huko cruzer ina mwaka 1 imeshakula KM70,OOO na zinatoka TOYOTA TANZANIA na makaratasi.

    Mfano mdogo tu.Umenunua basi jipya hapo Dar(Jipyaaaaaa 00000..) ukawa unalipeleka Mwanza.kwenda na kurudi linakula karibu KM2500,kwa mwezi likipiga trip 10 je,kwa mwaka...?

    Hiyo gari atauza tu mbona.

    David V

    ReplyDelete
  7. mdau hapa juu uko ughaibuni,unasema unanunua magari wewe?kununua magari na pesa ya kubeba box utaweza wewe?

    ReplyDelete
  8. Ankal,waosha vinywa wamezidi humu, hasa katika matangazo yanayotolewa na wadau wanaouza magari yao. Hapa kila mtu anajifanya mjuaji wakati wengine hata hawajui gari lina magurudumu mangapi achilia mbali masuala mengine ya kiufundi. Nimeshangaa sana kuona mtu anashangaa inakuwaje gari la mwaka 1998 liwe limetembea kilomita 49,000 tu. Hii si ajabu. Inategemea watu waliolimiki gari hili hapo nyuma walikuwa wanalitumiaje. Kwa mfano, hapa Dar kuna watu wanaendesha magari yao chini ya kilomita 10 kwa siku. Mfano mzuri ni Watanzania wenye asili ya Kiasia wanaoishi na kufanya kazi katikati ya jiji la Dar es Salaam. Hawa safari zao huwa ni fupi sana na hii ni moja ya sababu ya magari yao kuonekana bado mapya hata kama wameyatumia miaka 20. Kama unaendesha kilomita 10 kwa siku, kwa mwezi ni kilomita 300 na kwa mwaka ni kilomita 3,600. Kwa miaka 10 ni kilomita 36,000. Wengine huendesha kilomita hizi 36,000 kwa miezi sita tu au hata chini ya hapo. Inategemea na matumizi ya gari. Nimetembelea yard kadhaa za magari yaliyotumika Japan na nimeona magari yaliyotengenezwa zaidi ya miaka 20 iliyopita lakini yametembea chini ya kilomita 20,000. Ukiangalia ndani ya gari ya magari hayo na katika injini na sehemu nyingine unaona ni kweli hayajatumika sana.

    ReplyDelete
  9. acheni kumkatisha tamaa wewe kama unaona ni bei kubwa si uache. Ebo mwenzenu anaitaji hela akasome na kimfaacho mtu chake.

    ReplyDelete
  10. ..ila kwa hiyo hela, labda 2kusaidie tu

    ReplyDelete
  11. usikate tamaa mama! uza gari yako, asiye taka aache. umbea tu umewazidi, (kwanza ni wakazi wa mabondeni hao hawajui hata gereji).

    lakini? punguzo kidogo silipo mama!?

    ReplyDelete
  12. @Nimependa maoni yenu woote.....thanx

    ReplyDelete
  13. Mdau iingize kwenye kontena uende nayo UK unaweza pata watu waliokaa vizuri kifedha wanaotokea nchi zingine za Dunia kama Somalia, Afghanistan, Iraq au Libya ukauza BEI HIYO AU YA JUU ZAIDI!

    ReplyDelete
  14. Kwa bei hiyo na gari yenyewe, labda umpate Haramia wa Kisomali aliyefanikisha utekaji meli Bahari ya Hindi karibuni akapewa PANGA LAKE($$$), au Tajiri wa Madawa anaetoa VELENTINE GIFT kwa Demu,,,na hivyo ilivyokuwa nyekundu!

    ReplyDelete
  15. Kwenye tangazo ulisahau kuandika kuwa madalali hawatakiwi. Hao wanaochonga wengi ni wazushi wanunuzi makini watakutafuta.
    Kila la heri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...