Wazalendo,

TPN inasikitishwana hali inayoendelea ya kuzorota kwa huduma katika hospitali zetu nchini na inawapa pole Watanzania wote wanaondelea kuathirikia na waliothirika kwa namna moja au nyingine kutokana na mgomo huu wa madaktari.

Kufuatia hali hii TPN itaunda timu ya wataalamu ambao watachunguza kwa kina mgogoro huu, kufanya tathimini ya hali halisi na kutoa mapendekezo ya kutatua tatizo hili , kamati hii pia itapendekeza njia za kuepusha migogoro ya aina hii kutokea siku za baadae.

Wajumbe wa timu hii watakuwa ni wataalamu katika fani mbalimbali na watokana na wanachama na wadau wetu wa TPN, muda wowote wajumbe wa timu hii ya wataalamu watatangazwa na kuanza kazi yao haraka iwezekanavyo.

Phares Magesa
Rais- TPN
Tanzania Professionals Network
website: www.tpntz.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. timu ngapi nyie acheni wazim bana watu wanakufa huku madaktari walishasema wanataka nini tokea siku ya kwanza.. sa mnachunguza nini?

    ReplyDelete
  2. TPN nanyi mnakuwa kama wanasiasa.. wakati mnatoa matangazo watu wanakufa.. kuna taarifa kuwa mortuary ya pale Temeke hospital kwa kawaida huwa inapokea maiti 15 kwa siku lakini sasa inapokea 30 na zaidi ambao wamekufa hapo hospitali.. nyie by the time mnaunda tume mgogoro utakuwa umeisha na watu wengi wamepoteza maisha.. professionals tuwe pro active haraka si kama wanasiasa.. miye nilitegemea hapa ungeweka tangazo kuwa hiyo tume iilishafanya kazi na hapa ungeweka ripoti na mapedekezo..

    ReplyDelete
  3. Phares, ulitakiwa uandike kirefu cha TPN tangu ulipoiandika kwa mara ya kwanza katika document yako maana umetupa taabu wasomaji kujua TPN ni nini hadi tulipokuja kuiona mwisho kabisa ambao tayari tushapoteza muelekeo na uelewa.
    Taratibu za kiuandishi zinataka kwa mara ya kwanza unaandika kirefu na abbreviation yake katika mabano then baada ya hapo ukitumia abbreviation msomaji atajua unarefer kwenye nini.
    By professional mass communicator, Ipyana

    ReplyDelete
  4. Ni ujinga na wastage of time&resources kuunda tume katika mambo ambayo yako so direct...mtapendekeza nn kipya?madai yao yanajulikana tena yapo so direct?mnaunda tume kuchunguza hayo madai au?then mtapendekeza njia za kuepuka migomo kama hii kwa nani??serikali au watu binafsi??maana serikali imeshaunda tume..hivi ni professionals gani ninyi msioweza hata kufikiri?kweli Tanzania haiwezi kuendelea endapo hata watu wanaojiita wasomi thinking capacity yao ni sifuri kama hii..! MICHUZI FOR THE SAKE OF OUR NATION NAOMBA USIIBANE HII MSG ILI HAWA WATU WAPATE UFAHAMU MAANA NAONA DARASANI HAWAKUUPATA

    ReplyDelete
  5. ILI JAMBO MSILIFANYIE MCHEZO HAWA TPN WAO WATAENDA KUONGEZA NINI WAO MADAKTARI WANACHO ITAJI WAPEWE HAKI YAO INAYO STAILI SIYO TENA KAMATI MAHALUM YANINI NA WATU WANAENDELEA KUFALIKI KILA SIKU ILI LINAELEWEKA JE ? KAMATI YA WABUNGE IMEENDA KUFANYA NINI KWANI KAMATI YA WABUNGE HAITOSHI NAONA ILI JAMBO MNALIFANYIA MZAHA

    ReplyDelete
  6. TPN mnatak kuuziwa mbuzi kwenye kiloba kuweni makini kwa hili.Kuna kamati ngapi baada ya kuundwa na kutoa mapendekezo,hayo mapendekezo yakatekelezwa!? ama si zaidi ya kukali mafaili.Ngoja nikupe habari kidigo:
    Mimi ni muathirika mkubwa sana wa haya mambo ya kamati Mnamo mwaka 2005 nikiwa mwanafunzi wa Dar es salaam Institute Of Technology mwaka wa mwiho wa tatu,kulitokea mgomo mkubwa chuoni hadi bunge waliingilia ikaundwa kamati,wakatoa mapendekezo yao lakni mpaka leo takriban wanafuzi karibia 600 tulishindwa kumaliza kwa kuwa naimani mapendekezo yatazingatiwa tunasufer mtaani na transcrip zetu hatuwezi kujiendeleza tena,tukirudi chuo hawataki kutusikia tena
    Mimi navyoona kwa upande wangu serikali huwa wanatumia technique hiyo ili kuwapumbaza watu kuwa kunakitu kinafanyika lakni hamna llte na Madaktari wakilegeza uzi tu wako watakaotolewa muhanga,na utasikia wale wanaliosababisha mgomo upande wa serikali wanakuwa promoted.
    Msikubali kwa hilo labda mfanye pasipo kujihusisha na serikali moja kwa moja.

    ReplyDelete
  7. TPN,

    Sawa ni wazo zuri kwa vile mnatambulika kwenye Mamlaka muwashauri Wakubwa wajaribu kudhibiti 'mabao' ya matumizi hewa kama lile la Wilaya ya Kishapu BILIONI 7 labda wakibana huko wataweza kuwajali Madakitari.

    HAKUNA LINGINE KWA MADAKITARI NI MASLAHI TU!

    ReplyDelete
  8. Unajiungaje na TPN. kuna form za kujaza au kama ni mtaalam imeshatoka hiyo. Ningeomba nijiunge na TPN na moja kwa moja niombe uwakilishi wa dhati katika kuyatatua matatizo yanayojitokeza kila wakati sio tu katika fani afya pamoja na fani nyingine. Tuzibe nyufa kila mahali.
    Nilikuwa sijui kuwa kuna chombo kama hiki Bongo, na kama kipo basi pamoja na hiyo Project wanayotaka kuifanya afya ambayo naiona ni ya muhimu sana, ningeomba vile vile kikundi kingine cha hicho chombo (TPN) kishughulikie mkanganyiko uliojitokeza hivi karibuni hapa Bongo kwa wasomi na wanataaluma, wa-kujitambulisha elimu, taaluma au ngazi zao za kisomo kiajabu ajabu, and they dont follow international Code.
    kwa mfano ni ajabu na si kawaida kwa mwanataaluma, msomi aliyebobea kwenye upande wa ufundi kokote pale duniani, ajitokeze au amuombe Mwaandishi wa habari including Issa Michuzi kuwa anataka anapotajwa jina lake au kuliandika ati itangulie kwa mfano: Eng./injinia Bakari na kadhaklika.
    kwangu mimi na wengine tunaofuata international Code nikichekesho na nisingetaka mtu aniulize nacheka nini, maana kila kitu hapa duniani kipo for reasons na kwa utaratibu maalumu na mambo mengine ni lazima kufuata utaratibu uliopo wa kimataifa.
    Angalau basi mtaalam au msomi huyo Bakari angekuwa Creative, akatupigia kazi nzito ya ufundi wake hapo Bongo tukashangaa, kwa kweli nisingesikitika saaaana kumuenzi hivyo atakavyo, ijapokuwa still is unappropriate.
    Jamani, shule mmeenda, si haba!!!, lakini wasiwasi wangu ni kuwa je Mmeelimika? mnafuata taratibu zilizopo na kukubalika? la sivyo wenzenu wanawacheka. kwenye kisomo msilete uchakachuaji au ufisadi.
    Waacheni Madaktari wa Afya wajinome na Dr. mbele ya majina yao maana ni utaratibu uliokubalika.
    Hapa nina maana vile vile kwa wale wasomi wenye Phd. wanaothubutu kujiwekea Dr./Dkt. mbele ya majina yao, hili nalo linanitia kizungu zungu. Wachukue mfano kwa waalimu(supervisors)wao, wa majuu kama walishawaona wakitumia Dr. kama si daktari wa Afya.
    Hapa kuna upungufu nafikiri, hivyo na hilo mlishughulikie.
    Na mwisho ningeomba ijapokuwa ninyi hamshungulikii kutathimini degree za wasomi hapa Bongo, lakini nawakilisha wasiwasi wangu mkubwa sana kuhusu degree zinazotolewa na CHUO HURIA cha Dar-ES-Salaam (Hazipo kwenye Kiwango, I am so sorry for that).
    Nimewakilisha tuuuuuu

    ReplyDelete
  9. kama kawaida ya nchi za afrika kila kitu ni lazima kiundiwe kamati hata kama mtoto mdogo wa miaka miwili anajua fika sababu ya kilichotokea.

    Hebu tuambieni hiyo kamati itafanya uchunguze wake bure? hakutakuwepo na posho za kula, kulala na kusafiri n.k?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...