Salaam Ankal,

Naomba uwape wadau hii ili waone umuhimuwa wa kuwa karibu na familia zao,hii ilipatikana kanisani, pale mchungaji aliyealikwa kutulisha neno la bwana alipoamua kutushirikisha matatizo yanayowapata wana kondoo wa bwana. 

kuna siku alipigiwa simu na wazazi fulani aende nyumbani kwao akamuombee binti yao mdogo mtoto wa darasa la nne.

 kisa cha kuitwa ni kuwa yule mtoto anasoma hizi shule za academia,siku moja asubuhi wakati anawahi basi la shule alisahau kuzima fan (pangaboi la juu) chumbani kwake, kupitia kioo cha juu ya mrango wazazi wakaona pangaboi linazunguka baba akaamua aingie chumbani kwa binti akazime ghafla akakutana na vidonge juu ya meza ya kusomea....akamuita mama akamuuliza ni vya nn?

lahaula vilikua ni vidonge vya majira ya uzazi, wazazi wakahamaki sana wakajiuliza maswali mengi, wakakubaliana wamsubiri binti akirudi jioni wamuulize. Binti aliporudi akabanwa na wazazi, mwanzo alitaka kugoma, wakamtishatisha akakubali kuwa amepewa na Mlinzi wa getini hapo nyumbani, mazingira wanayoishi ni katika estate ina nyumba kama kumi na tano, so the whole compound imezungushiwa ukuta na ina geti moja kubwa la kuingilia.

Mtoto akaanza kueleza kuwa mchezo huo aliuanza miaka miwili iliyopita na fundi mwashi aliyekuwa anajenga hapo estate ndo alianza kumfundisha Ngono, thena aakafuata Mlinzi, mlinzi aliponogewa akamwambia mwenzie, huyu wa plili akamtishia mtoto kuwa asipompa na yeye atamsemea kwa baba yake, mtoto akampa, akaja wa tatu, huyu ndo akamfundisha na kutumia vidonge, sasa akawa mtaalam. 

 Mchungaji alipoitwa akasema kabla sijamuombea naomba mnipe mda nikae nae mm na yeye tu nimfanyie counselling, hapo ndipo yalipofumuka memgi makubwa, yule mtoto akakiri mbele ya baba mchungaji kuwa ameshazoea sana mchezo wa ngono hata hapo kwenye estate wanapoishi ameshatembea na wababa wanne, huwa anaaga anaenda saloon wkend akifika nje hao wababa wanampakia kwenye magari yao wanampeleka huko wanapopajua kumfanyia uharibifu, akaendelea ku-narate kuwa hata dereva na konda wa school bus tayari ameshafanya nao, shuleni amefanya na walimu wawili na Mwalimu mkuu pia.

 Mchungaji hakuwaeleza wazazi extent ya uharibifu aliyofanyiwa mtoto wao, aliwaita wote akawaombea, next akaenda kwenye hiyo shule kupambana na mwl mkuu, ushauri wa mwisho aliwapa wazazi ni kumwamisha binti shule, pamoja na kuendelea na maombi kwa binti huyo..........................

story hii iliwatoa machozi watu kanisani. Kikubwa kinachojitokeaza hapa ni hii style ya maisha ya sasa, wazazi tupo too busy na kazi,kutafuta hela kiasi hatupati kuwa karibu na watoto wetu, sasa upweke wanaoupata watoto ndo wanatumbukia kwenye mambo ya ajabu kama haya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. its true wala si uongo naunga mkona kabisa story hii tena huku marekani kuna wazazi wako so busy hata time ya kukaa na watoto wao hawana wao wana ubusy wao wakutafuta pesa za kulipa pango na kujifaharisha tu kipumbavu na huku watoto wanapotea tena huku ndo inasikitisha ile mbaya na ni watanzania wakuwajua wenye heshima zao.
    yani wee acha tu, na si watoto wa kike tu hata watoto wakiume kuna wenginewe wanageuka mashoga kwa ajily hii hii ya wazee kukosa time na watoto wao kutafuta pesa za obama tu ndo wao wanajua.
    yani acha tuu, lakini mungu atasaidia.

    ReplyDelete
  2. Historia ya ukweli au kuchangamsha blog?Mmm sisi wenye watoto hawa wa kisasa kazi tunayo.

    David V

    ReplyDelete
  3. eeh makubwa jamani mm mwenyewe nimeshindwa kushangaa, mmh mungu awasaidie hawa wazazi mana huu ni mtihani mkubwa

    ReplyDelete
  4. nakuunga mdau asilimia mia kwa mia. TOO BUSY TO BUSY WATOTO KIASI WANAKUWA WATAALAMU KULIKONI HATA HAO MACHANGUDOA WABARABARANI. NA HAYA MAPINDUZI YA NEW TECHNOLOGY NDIO TUNAANGAMIA SASA. HOFU YANGU ISIJE TUAPATA KIZAZI CHA MACHIZI BAADAE

    ReplyDelete
  5. Ni kweli. Lingine la muhimu ni kuhakikisha unawalea watoto kwa misingi ya kidini, ikiwemo kuhakikisha unawapeleka kusali angalau mara moja kwa wiki. Muongozo wa kidini katika umri mdogo humjenga mtoto kuwa na woga wa kufanya maovu kadiri anavyokua. Mfano mzuri ni mimi mwenyewe na ndugu zangu. Japo hatukuwa karibu na wazazi kwa kiasi kikubwa, msingi waliotujengea ulitosha kuwawakilisha pale waliposhindwa kuwepo nasi.

    ReplyDelete
  6. malezi ya wazazi tu hayatoshi.wengi wanalelewa na command..without be given chances to express themselves.wazazi wengi hawatoi fursa ya kuwasikiliza na kuwaelewa watoto wao nakuwafanya lonely
    sura muhimu kuliko zote ni uhuru ulioambatana na ukombozi wa kifikra uliosisitizwa katika nidham N.K

    ReplyDelete
  7. Haya mambo yapo sana katika nchi zilizoendelea. wazazi wanasaka hela masaa yote na watoto wao wamehamia kwenye madanguro!

    ReplyDelete
  8. Wazazi wengine wako busy na nyumba ndogo hana mda wa kukaa na watoto, akitoka kazini anawahi nyumba ndogo

    ReplyDelete
  9. U bize kwenye Malezi,,,mbona kwenye kutafuta Uzazi na kuupata Uzazi hakukuwa na Ubize?

    Malezi ni jukumu la lazima na halina Msamaha, la muhimu ni kudumisha Mila na Jadi kwa Malezi bora!

    ReplyDelete
  10. hata hapa Tanzania, mimi nimekwenda interview na mwanangu shule ya kidini Bagamoyo, nimewakuta hao watoto wa shule wana simu na lugha wanayozungumza left much to be desired. Akitoka shule ya dini nyumbani kuna nidham, tena mzazi anasema amefungiwa siku nyingi shuleni wacha apate uhuru kidogo.

    ReplyDelete
  11. Dhamana ya malezi ya mwanao ipo mikononi mwako ewe Mzazi sio Msichana wa Nyumbani au Shamba Boi!

    Tuamke, sasa unamwachia mtu mwingine mwanao na unajisahau kabisa kama wewe ni Mzazi au Umezaa hivi hii ni haki kwa Watoto kweli?

    Kuna starehe kweli na akili inatulia wewe Mzazi ukiwa huna taarifa ya kinachoendela juu ya mwanao huko nyuma nyumbani?

    Tuna uchungu wa kweli na Upendo wa dhati na Watoto wetu?

    Ndio ulezi gani huu?

    ReplyDelete
  12. mh!
    that is more than serious!ameanza two years before,maana yake akiwa darasa la pili!
    NI kweli maisha ni magumu na wazazi wanahitaji kutafuta hela kwa nguvu.BUT..LAZIMA tujenge tabia ya kuwachunguza watoto tena bila wao kujua.Mwangalie mwanao mwendo anaotembea,jenga tabia ya kumwogesha angalau mara mbili kwa wiki,mabadiliko utayaona tu.Wamama tuwasaidie watoto hawa,si wa kike tu na wa kiume pia wako exposed kwenye dunia ya satans.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...