Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar imetoa ufafanuzi juu ya hali ya ununuzi na uhifadhi wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba kutokana na taarifa zilizochapishwa na Gazeti la Daily News la Februari 4 mwaka huu ambapo inadaiwa kwamba wakulima wa Zao la Karafuu wamekataa kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara la Zanzibar ZSTC

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Wizara hiyo imesema kuwa kauli hiyo siyo sahihi na wakulima bado wanaendelea kuliuzia Shirika hilo Karafuu zao kama ilivyopangwa ambapo hadi sasa jumla ya Tani 588.735 zenye thamani ya Tshs 8,824,850,750.00 zimeuzwa kwa Shirika hilo kwa Wilaya ya Micheweni tu.

Aidha kwa Wilaya ya Wete jumla ya tani 1,530.536 za Karafuu zenye thamani ya Tshs 22,923,724,500.00 zimeshauzwa kwa ZSTC jambo ambalo linaonesha utayari wa wakulima kuliuzia Shirika hilo.

Taarifa hiyo pia imefafanua kwamba Mkulima anaruhusiwa kuhifadhi karafuu zake kwa muda apendao iwapo tu Karafuu hizo zitahifadhiwa katika Maghala ya ZSTC na Mkulima hupewa Stakabadhi inayoonesha kiasi kinachohohifadhiwa ambapo kwa sasa kuna idadi kubwa ya wakulima wanaotumia utaratibu huo wa kuzihifadhi na kuziuza kwa siku za usoni.

Serikali ilichukua hatua hiyo ya uhifadhi kwenye maghala  salama ya  ZSTC kwa lengo la kuziepusha Karafuu Kusinyaa,kupungua kwa daraja la ubora na kuziepusha kushika moto,mambo ambayo yanaweza kupelekea maafa na kumkosesha mkulima faida iwapo zitahifadhiwa nyumbani

Kuhusu madai ya bei ya Karafuu taarifa hiyo imesema ukweli ni kuwa katika bei ya soko la dunia kilo moja inauzwa kwa Dola za Marekani 11-13 ambapo wastani wake ni sawa na Tshs 17,270 hadi 20.410 jambo ambalo linaifanya tofauti kati ya soko la ndani na nje iwe ni kati ya Tshs. 2,270 hadi 5,410

Kutokana na Uchambuzi huo taarifa hiyo imesema kwamba madai kuwa bei ya Karafuu kwa sasa kuwa ni Tshs 40,000 kwa kilo hayana ukweli wowote na upotoshaji wenye dhamira ya kulifanya Shirika la ZSTC na Serikali ionekane kuwa inawanyonya wakulima wa zao hilo

Taarifa hiyo inawashukuru wananchi kwa kuendelea na moyo wao wa kuzidi kuliuzia Shirika la ZSTC ambapo mpaka sasa shirika hilo limeweza kuvuka lengo la manunuzi kwa asilimia 119.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...