Na Lady Jaydee


Kuna watu inatokea wanakuwa na bahati ya kuwa na vitu vyote tu 
Mume tajiri, kazi nzuri, mshahara mnono na nafasi zingine za juu katika maisha.
 Ni rahisi kuwa envy na kuwaonea wivu.
Lakini ukiutumia wivu huo kwa njia nzuri unaweza kuwa wa manufaa
Na ukiutumia wivu vibaya unaweza ukaumiza zaidi hisia zako mwenyewe.

Inawezekana kabisa kuwaangalia watu waliofanikiwa na kufurahia mafanikio yao Lakini wivu unaanza kukula pale unapotamani kuwa kama wao
Inasemekana wivu unawaathiri sana watu wenye umri chini ya miaka 45 
Lakini ukiangalia kwa undani watu wengi waliofanikiwa, wamepitia njia nyingi sana hadi kufikia hapo walipo. 


Je! uko tayari kupitia magumu kama yao? Au unaona wivu tu?

Watu wengine wamesota zaidi ya miaka 20 kufikia mafanikio
Sacrifices, kutokulala usiku na mafanikio mengine sio hata katika njia halali 
Wakati watu wengi wenye wivu wanahitaji mafanikio ya haraka haraka na njia za mkato
 bila kujua kuwa ili ufanikiwe ni lazima utumike kisawa sawa 
Zaidi ya hapo labda ucheze lotto/Bingo ndio njia pekee na rahisi lakini pia mpk uwe na bahati
 

Wivu unachangia mtu kuwa na roho mbaya (chuki) na kutojiamini

Na wivu unamuumiza zaidi mtu anaeona wivu, kuliko yule anaeonewa wivu 

Kama hufurahii vile ulivyo, au kile ulicho nacho
 

Wekeza nguvu katika kupanga mipango ya baadae ya kuboresha maisha zaidi kuliko kujijazia chuki na kupoteza muda kufikiria kitu ambacho huwezi kuwa nacho.
Ni ngumu lakini ukiipa muda na kujitolea utaweza
SHINDA VITA DHIDI YA WIVU

1. Kuliko kupoteza muda kwa kile ambacho huna, weka nia katika kuendeleza kidogo chochote ulicho nacho, Ndoto zako, kipaji chako hivyo ndio vyanzo vya mafanikio yako


2. Ni vizuri kuwa mshindani, kwa njia ilio sahihi kwakuwa tupo kwenye dunia ya ushindani.
Lakini uwe na tahadhari na ujiepushe na hatari ya kushindana ili uwe bora kuliko wengine
 
Jikubali kwanza na ujitambue wewe kama ulivyo, nini malengo/makusudio yako katika maisha.
Ukubali wazi kuwa itachukua muda na sio kazi rahisi kufikia walipofikia wengine bila kufanya kazi kwa bidii
 

3.Ukishaamua nini cha muhimu kwako, elekea katika kutafuta kazi zenye manufaa
. Kubali kujifunza kadri uwezavyo kutoka kwa wakubwa, au waliokutangulia kiujuzi ili kuongeza ujuzi wa zaidi ya kile unachokifahamu, huku ukikubali kukosolewa 

Ndio hapo na wewe unaweza kumiliki simu 2 moja ikiwemo Back Berry kama unahitaji. Lakini jitahidi ununue kile kitu ambacho tu ndio uwezo wako
 Na sio kuwa na kitu ili mradi watu wakuone kuwa umefanikiwa kukipata hata kama haukihitaji au hakiko ndani ya uwezo wako

4. Kubali na ridhika na ulicho nacho hata kama ni kidogo, jua jinsi ya kupanga na kukitumia kikakidhi mahitaji yako

5. Tafuta watu waliofanikiwa uongee nao, wauliza njia na jinsi gani wamefanya mpaka kufikia mafanikio walio nayo (Japo wengine huwa hawasemi ukweli) ila sikiliza halafu chuja 

6. Kama una mwili mkubwa na unahitaji kupungua, ni lazima ufanye mazoezi na ufatishe njia unazoelekezwa ili kupata mwili unaouutaka
Sio kwa kukaa nyumbani unaendelea kula na kumchukia mtu mwembamba kwa kumtoa kasoro
Kama unahitaji kuanzisha biashara nenda kwenye seminars zinazohusu mambo ya biashara ukajifunze ili ujue wapi pa kuanzia
Chochote unachotaka kufanikiwa nacho ni lazima ukitumikieJINSI YA KUKABILIANA NA WIVU

1. Jiangalie na ukubali kuwa una wivu, halafu itumie hiyo nafasi kama silaha ya kukujenga. Ni ngumu sana watu kukubali kuwa wana wivu, na hilo ni tatizo 

2. Ni rahisi kukutwa katika hali ya kuamini kuwa watu matajiri ndio washindi na maskini ni loosers lakini sio kweli.

Usiangalie mtu kutokana na kiasi gani alicho nacho, angalia vitu ambavyo ni vya muhimu
 
Kama utu, ukarimu, ukweli na usimtathmini mtu kutokana na mfuko wake.
 Unaweza kuangalia mambo yanayotamanisha kwa nje kama hujui ki undani yakakufanya ujisikie mnyonge na kuyadharau maisha yako binafsi 

3. Kama ukimuonesha roho mbaya mtu unaetamani maisha kama yake haitasaidia, inaweza kuwa mbaya zaidi maana hata kama ilikuwa akupe msaada hutapata kitu
 Kama umefanya hivyo rudi ukaombe msamaha 

4. Kama huwezi kuondokana na hali ya wivu, iongelee na uelezee hisia zako kwa mtu wako yoyote wa karibu itasaidia
 
Wivu unaweza kukupelekea katika matatizo ya kuwa na stress zisizo isha, blood presure na kutokulala usiku unakesha ukiwaza



KILA KHERI KATIKA KUJARIBU KUJIKOMBOA NA GONJWA LA WIVU
NI UGONJWA AMBAO UNAKUATHIRI ZAIDI WEWE ULIE NAO KULIKO HATA YULE AMBAE UNAMUONEA WIVU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 56 mpaka sasa

  1. Very well said...in a way though!

    ReplyDelete
  2. Kweli dada umezungumza point za maana sana! Mimi ninakusapoti asilimia mia na katika ujumbe huu. Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa Wananchi na kipimo cha utu na kila mtu anaowajibu wa kushiriki kwa kujituma na kuwa mwaminifu katika kazi halali na ya uzalishaji mali na kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia malengo ya pamoja yanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria. Tukifanya hivi wote tutakuwa na mahitaji yote muhimu tunayoyahitaji katika maisha yetu na kila mtu akifanikiwa hakutakuwa na mtu mwingine kumwonea wivu. Tunatakiwa tuwe na wivu wa maendeleo sio wivu wa kutaka kumrudisha mwingine nyuma.

    ReplyDelete
  3. full of crap, i don't believe in kuridhika and the other non sense we are all in this world for a purpose, one has to find their talents and maximize their potentials. this woman has issues hajui jinsi ya kuwapa watu moyo. wivu is a very natural thing hata mtoto mdogo ukicheza na mama yake anaona wivu. labda anacho taka kuongelea ni chuki na sio wivu.

    yeye kama hana wivu amuazime gardner mwanamke mwingine.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli mwenye macho na asome, mwenye na mwenye kusikia na asikia, ushindwe mwenyewe! na mwenye wivu ajinyonge, asante Jide.

    ReplyDelete
  5. Kwakweli mimi namuunga mkono huyu mchangiaji wa 3. Kuna utofauti mkubwa kati ya Wivu na Chuki. Na kiukweli ni kwamba huyu mwanadada ameshindwa kutofautisha maana halisi ya maneno haya mawili katika ujumbe wake. Na kutokana na hili ameshindwa kufikisha dhamira yake kwa wasomaji. Msomaji makini atagunduwa kwamba mara atakapomaliza sentesi ya mwisho ya ujumbe wa mwanadada huyu,atakosa kujua nini dhamira aliyokuwa nayo mwandishi.Nionavyo mimi upande mmoja ameongelea chuki, na akachanganya na wivu ndani yake,amejaribu kutengeneza mahusiano kati ya Wivu na Chuki, na hatimaye ameshindwa kudhihirisha uhusano huo ndani ya ujumbe wake.Wivu pia upo wa aina nyingi, na upo wivu unaosababisha/na usiosababisha chuki.Ninamatumaini mwandishi alikuwa akimaanisha tupige vita wivu unaosababisha chuki. Na kama huu mtazamo wangu ni sahihi, basi njia alizoainisha kama jinsi ya kupambana na aina hii ya wivu si sahihi hata kidogo.

    ReplyDelete
  6. Pumba tupu!

    ReplyDelete
  7. "mume tajiri". Hii peke yake inatosha kuona kwamba mtoa mada ana matatizo makubwa akilini. Kwa sababu hakutaja sifa yoyote nzuri kwa mwanaume zaidi ya utajiri.

    ReplyDelete
  8. Baada ya kusoma maelezo ya huyu dada, nimeyalinganisha na tungo zake zinazohusu maisha na wivu. Yaonekana huyu dada muda mwingi anawaza jinsi watu wanavyomwonea wivu kwa maendeleo yake na jinsi anavyoweza kupangilia miradi yake ambayo ukweli inafanikiwa.

    Nilikwenda kwenye kiota chake mwaka jana na ilikuwa siyo siku yake ya kuimba, nilipoenda kulipa counter maana yeye alikuwepo niliuliza mbona hukuimba? (mimi ni mgeni Dar na hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kwenda pale) alinijibu kwa hasira kidogo kuwa kaulize ratiba yangu! Nilisikitika lakini ndo hivyo. Haikunizuia kwenda tena siku ambayo alikuwa anaperfom maana nina niece wangu awliopenda kumwona anaimba lakini attitude yake ilinifanya niwe na swali why anger? Yawezekana amefikishwa pale na watu wasiokubali kazi zake ambazo mimi nazihusudu, au kuna personal issu????

    ReplyDelete
  9. mbona amefafanua vizuri kabisa kuhusu wivu au una yako moyoni ndugu yangu? kasema kila mtu ana wivu ila utumie vizuri kujiendeleza na sio kwa mabaya. what else do need from her explaination. dude get a life!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Maneno na Ushauri ni wa Maana sana, licha ya baadhi ya yetu kuelewa ndivyo sivyo.


    Zaidi ya madhara makubwa ya WIVU aliyotaja ndugu yetu Jide haya ni miongoni mwake:

    1.Wenye wivu kuishi maisha ya tabu kutokana na msongo wa mawazo, kupata mashinikizo ya damu, mapafu kujaa maji,kukata pumzi,visukari,kupooza n.k kwa vile wanataka mambo yawe kama wanavyotaka wao tofauti na alivyopanga Mungu kitu ambacho haiwezekani kabisa, Mungu ndiye mwenye Mamlaka na ndio kila kitu!

    2.Wenye wivu kuzeeka haraka na kuwa na sura zisizovutia unakuta mtu ana umri wa miaka 19 tu lakini anaonekana kama ana miaka 91 hivi!

    3.Wenye wivu hufa haraka zaidi na mara nyingi wanakufa ghafla sana!

    ReplyDelete
  11. Ni kweli kabisa maneno ya Jide.

    Mara nyingi mwenye wivu usio endelevu hafanikiwi ng'o na ndio kwanza Mwenyezi Mungu anampiga RUNGU LA KICHWA PUUU!

    MUNGU HAKUBALIANI NA KIBURI NA JILASI (wivu)!

    ReplyDelete
  12. Imedhihirika wazi kuwa Mungu huwaadhibu sana kwa ghadhabu wenye wivu dhidi ya wenzao.

    DHARAU huzaa WIVU
    WIVU huzaa CHUKI

    DHARAU=WIVU=CHUKI

    Ndio yale mambo unamwona mtu unaejuana naye kitambo tu lakini anakukimbia anakukwepa hataki muonane!

    ReplyDelete
  13. Unakuta mtu mnafahamiana vizuri tu, lakini habari zako anaulizia kwa watu badala ya kukuuliza wewe mwenyewe!

    Hii inakuwa ni Unafiki,Fitina na Chuki.

    Hii yote ndio yale yale maradhi ya WIVU!

    ReplyDelete
  14. Nionavyo mimi ni kwamba maelezo ya mwandishi yamewalenga wanawake wenzake ambao anahisi wanamuonea wivu katika mafanikio yake..it is girls talk..thats why kazungumzia mambo ya mume tajiri..haikuwa ishu ya ujumla..naona ujumbe umeingia kwenye wrong blog..labda ungebakia kwenye blog yake..kwa sisi wanaume na hairing bells hata..imekaa kimipasho pia..ni kama tu nyimbo zake mingi zilivyo..dada huwa anatabu kidogo ya kutenganisha kazi na moods au peronal issues zake. Ni mawazo tu

    ReplyDelete
  15. Nadhani kila mtu mwenye busara na akili timamu anapoandika ujumbe wake kupitia hizi blogi na media outlets mbalimbali,analengo jema la kufikisha ujumbe na maudhui aliyonayo moyoni kwa wasomaji na hatimae wote kwa pamoja kushiriki hisia na mafunzo yajiliyo ndani ya maandishi hayo.
    Dada Jide naye alikuwa na lengo zuri la kufikisha hisia zake na kutufanya sisi wasomaji kushiriki hizo hisia kwa kujifunza au kutambua ukweli wa mambo ulivyo.
    Kwa sura ya piliyake dada ameshindwa kutushawishi wasomaji jinsi ya kutofautisha wivu na chuki.Hata hivyo wivu aliouzungumzia haku-uhainisha na chuki alizoziongea amejikita zaidi kwenye mahusiano nadhani.
    Hata hivyo ukidadafua kwa mbali utaona kwamba ameshindwa kuoanisha maandishi na picha alizoweka kwani havina shabaha moja hivyo havishahabiani katu.
    Mwisho,dada una mawazo mazuri lakini nadhani kuyaboresha kwa kuyapitia mara nyingi na kujiridhisha kupitia vyanzo vyenye dondoo kuntu ni jambo jema litakalokufanya uwe na weledi katika ufikishaji wa mawazo na hisia zako upande wa pili.
    Nakupenda sana.

    ReplyDelete
  16. Ni KWELI KABISA!

    GONJWA LA WIVU:

    Mambo hutokea kama MWENYEZI MUNGU MKUU ALIVYOPANGA!

    Haiwezekani mambo yaende kama wale Zumbukuku Vijiba vya Roho wanavyotaka, mfano katika picha hapo juu Mungu amechagua kuwapa Ankali(suti kaliii) na Jay Dee(mavazi bomba) kama unavyoona wanavyong'ara na mavazi yao!

    Sasa huyo asiyetaka au atakae kereka ndio walewale wenye gonjwa!

    Hamjui watu hawa wamepitia changa moto gani hadi kufikia hapo walipo?

    MUELEWE KUWA MUNGU HANA MSHIRIKA!

    ReplyDelete
  17. Ni KWELI KABISA!

    GONJWA LA WIVU:

    Mambo hutokea kama MWENYEZI MUNGU MKUU ALIVYOPANGA!

    Haiwezekani mambo yaende kama wale Zumbukuku Vijiba vya Roho wanavyotaka, mfano katika picha hapo juu Mungu amechagua kuwapa Ankali(suti kaliii) na Jay Dee(mavazi bomba) kama unavyoona wanavyong'ara na mavazi yao!

    Sasa huyo asiyetaka au atakae kereka ndio walewale wenye gonjwa!

    Hamjui watu hawa wamepitia changa moto gani hadi kufikia hapo walipo?

    MUELEWE KUWA MUNGU HANA MSHIRIKA!

    ReplyDelete
  18. watanganyika? wadanganyika bwana!!!. ninamtazamo tofauti sana wa maisha na maendeleo yote yaliyoko duniani leo ni matokeo ya wivu.

    ReplyDelete
  19. Mjomba zile Fulanazzz ni pati taimu tu, kumbe ukiwa katika suti walahi unakuwa Balozi wa kiukweli haswaaa!

    ReplyDelete
  20. ila simwelewi sana huyu dada kwa sasa , hiyo aliyotoa kwenye gazet la rasasi huu ni mfano wa jeneza lake na huku kuna maneno haya napata shida kujua ana tuambiaje

    ReplyDelete
  21. wewe ndio unaona amefafanua vizuri kwa kuwa akili zako ni fupi, lakini kwa mtu ambaye hana hasira hasira za ovyo na ana mtazamo positive kuhusu maisha hayaniingii akilini, nchi masikini kama hizi za kwetu ni za kujazana moyo ili watu wapate muamko wa kuchacharika na sio kuanza kuongelea wivu. wivu ni muhimu kwa maendeleo.

    ReplyDelete
  22. WIVU:

    Tuache chuki, kuchafuana, kudharauliana na kuchunguzana huku kufuatiliana kwa nia mbaya,

    Turidhike na kushukuru alivyotujaalia Mungu huku tukiongeza bidii zaidi!

    kama pana yule ambaye anahisi hajaridhika na vile Mola alivyomjaalia...ajaribu bahati yake ktk mipango mingine, AANZE SAFARI KWENDA KUKATA MKAA KALIUA TABORA!

    ReplyDelete
  23. Ya nini??? kupata,

    -shinikizo la damu,
    -kutahayari baada ya kuonana usoni,
    -kukwepana njiani,
    -kukosa usingizi,
    -kuota ndoto za kushituka shituka,
    -kuota ndoto za kutisha,
    -ndoto za jinamizi,
    -kukosa hamu ya tendo,
    -msongo wa mawazo,
    -vidonda vya tumbo,
    -ganzi mwilini,
    -kisukari,
    -kupooza,
    -kikohozi kisichotulia,
    -kwikwi,
    -mapafu kujaa maji na pumzi kukatika.

    Kisa?...eti Mwana fulani amepata, amefanikiwa!

    ReplyDelete
  24. Sioni tatizo katika aliyoyasema. Labda tu ni ile hasira tuliyo nayo dhidi ya watu waliofanikiwa ndo inafanya watu wengine wasute. Nafikiri maoni mengine yamezingatia nani kaandika na si nini kimeandikwa.
    By the way yeye kaandika kama mtu mwingine yeyote kwa maoni yake na si kwa sababu ya nafasi yake. Kama hukuipenda ipotezee lakini ina maana kubwa sana kwa wengine.
    Thanks dada Jide, Ila ujage mara moja moja kanda ya ziwa basi!
    ------Mdau wa Mwanza.

    ReplyDelete
  25. wivu mwingine kiama!

    wengine wanazeeka kwa wivu uliokithiri!

    unamkuta makunyanzi kibao usoni wakati yeye bado mdogo ki umri, anakuwa mchafu hata akioga anapauka kama hajaoga vile!

    mtu anajisikia kuharisha wakati haumwi na tumbo!, mtu anasikia chembe kifuani (kama kisu kinazama rohoni) wakati hana hata mafua!,mtu anasikia shoka linazama utosini kichwani!!!

    Duhhh hili balaaa!

    ReplyDelete
  26. This clearly is a message directed at her detractors, both real and imagined. It seems that Jide is obsessed with this 'wivu' thing. It borders on paranoia, and I fear for her mental wellbeing. Jide inabidi aelewe kuwa mtu yeyote aliyepata mafanikio makubwa kama yake lazima ataonewa wivu, whether well intentioned or otherwise. This is a fact of life she has to live and cope with as long as she is successful. Mafanikio aliyopata Jide ni kielelezo kuwa kuna watu wengi tu wanaothamini kipaji na juhudi zake katika sanaa na biashara. Hawa inabidi naye awathamini na kuwaenzi. The best thing to do about watu wanaomuonea wivu ni kuwadharau ili mradi wivu huo hauzai chuki. Inabidi aige mfano wa Ankal ambaye amepata mafanikio makubwa sana akiendesha blog hii. I have never heard Michuzi moaning about ‘wivu’ in his blog, although I’m sure he too has his fair share of detractors.

    ReplyDelete
  27. Ndio maana najisikia kumuunga mkono anony wa kwanza!

    ReplyDelete
  28. Safi sana. Hapa naona maoni yanayomuunga mkono na kumkosoa Lady Jay Dee. Nimesoma post hii hii kwenye blog yake ajabu ni kwamba maoni yote yanaunga mkono mada yake kwa asilimia 100. Inaelekea ni bingwa wa kuminya maoni yasiyompendeza.

    ReplyDelete
  29. Wajuaji huwa hamkosi cha kuongea ila katika kusoma kila mtu ana upeo wake katika kuelewa, wengine tumeona kuwa maelezo yako wazi na yanaeleweka ni kweli wivu ukiendekeza huzaa chuki. Lakini wivu ukiutumia kimaendeleo unaleta faida ndio maana akaeleza kuwa unatakiwa ukubali kwanza kuwa una wivu halafu ujue jinsi ya kuutumia, sasa wewe anony ulieleta swla la amuazime gardner inahusiana vipi? huo ndio wivu na chuki zenyewe

    ReplyDelete
  30. there's a thin line btn wivu na chuki ni vitu vya kuangalia sana

    ReplyDelete
  31. MIE KWA MAONI YANGU SIONI KAMA KAKOSEA SEMA ANGESEMA WIVU WA CHUKI, WIVU UNATAFAUTIANA NA VIPIMO VYAKE MTU ANAKUWA NACHO VIPI KAMA UNAWIVU WA CHUKI,ROHO MBAYA YA KWANINI,HUSDA,AU UNAWEZA KUWA NA WIVU MZURI KWA MPENZI WAKO, MBAYA PIA KWA MPENZI WAKO UKASABABISHA HATARI MWENYEZI ATUEPUSHE NA WIVU USIOFAA. YEYE KUWA NA WIVU NA MUMEWE HATA KAMA ANAJIAMINI VIPI KWAKE AU MUMEWE KWA JIDE SI WIVU MBAYA NI MZURI HUO, UKIENDA KIPIMO CHA UGOMVI NDIO UNAPOENDEA KWENYE UBAYA MPENDE ZAIDI MOLA. JIDE ATAKUWA KATOWA DUKUDUKU LAKE, ITAKUWA WIVU WA ROHO MBAYA NA CHUKI KAONGELEA. MZEE

    ReplyDelete
  32. wewe mtoa comment ati kuolewa na mume mwenyepesa hayo ni mawazo ya kizamani au na wewe ni wa uswahilini? kwenu mnakula mlo mmoja kwa siku au vipi ? Utajiri sio sifa za mwanaume kwa hiyo wewe Huyo aliekuwa rais wa Libya Gaddafi na Mobutu wa zaire au kongo wewe unaona ndio bahati ya kuolewa na watu kama hao pamoja na mauaji yote walioyafanya ili wao wawe matajiri na mamlaka zaidi ya wengine kwa hio wewe umona ni sifa kubwa sana kuolewa na watu kama hao ? Nenda kwa LIYUMBA kama wewe unaona ni raha kuolewa na tajiri akuue na ngoma

    ReplyDelete
  33. wivu watu wanaoneana sana!

    Tukubali tusikubali!

    Ndio maana maradhi mengi kama Kifafa cha Ukubwani, Dege dege la Ukubwani hadi kubaki midomo wazi, Viharusi,Kushindwa kupumua baada ya mapafu kupata hitilafu, ingawa maradhi hupangwa na Mungu,,,ukichunguza wengi wapatao mambo haya waliwachezea rafu wengine au walicheza rafu hivi au vile,,,na kwa kuwa walitaka mambo yawe kama wanavyotaka na Mungu alishaapa hana Mshirika matokeo yake hutoa Adhabu kwa hasira dhidi ya wabaya!

    ReplyDelete
  34. simfagilii Jide kiivoo lakini sioni alichokosea katika uandishi wake. kawapa ukweli watu wenye wivu na chuki na wenzao. wivu wa kimaisha ni wachache sana walionao. wengi wetu tuna wivu wenye chuki, wanawake kwa wanaume. na alichosema Jide ni kweli kwamba anaeona wivu ndie anaeumia wakati mwenzie anaendelea na maisha yake kama kawaida. Punguzeni wivu na chuki watanzania mnaboa sana. kutwa kufuatiliana yule anaishi vipi, kaolewa na mtu wa aina gani, ana pesa kiasi gani anavaa nini. yanahusu nini yote hayo mind ur own business people n stop hating for no reasons.wa kumfatilia ni mwanao tu au mmeo au mkeo na sio binadamu mwingine. ndomana siku izi hakuna tofauti kubwa kati ya mtu wa miaka 50 na 20 wote wanaonekana age moja sababu wengine wanazeeka kwa wivu na chuki. mtake msitake huo ndio ukweli..meseji delivadi..

    ReplyDelete
  35. MDAU wa 11 hapo juu Anonymous wa Sat Feb 04:07:52:00 AM 2012

    Amesema,

    DHARAU huzaa WIVU
    WIVU huzaa CHUKI

    Hivyo,

    DHARAU=WIVU=CHUKI

    Kwishwa,

    TUKUBALI AU TUKATAE, WATU TUNAONEANA SANA WIVU NA CHUKI!

    KWA USHAHIDI NI MAJUNGU,KUDHARAULIANA, KUFUATILIANA,KUSENGENYANA, USALITI NA FITINA ZINAZOTUZUNGUKA KATIKA SEKTA ZOTE ZA MAISHA SIASA, KAZI, BIASHARA,DINI, MICHEZO NA MENGINE MENGI!

    ReplyDelete
  36. Unakuta mtu anakudharau, akiona dharau yake haifanikiwi anabadilika anakuonea wivu,,,akiona bado ANAKUCHUKIA!

    AKIULIZWA KWA NINI UNAMCHUKIA JAMAA?...ANAJIBU BASI TU MIMI NAMCHUKIA!...YAANI ANAKUWA HANA HOJA KWA NINI ANAMCHUKIA MTU!

    ReplyDelete
  37. Jamani acheni kukufuru Mungu,Wewe Jide na wengine mliochangia kuwa watu wanaopata ugonjwa wa moyo na kisukari,blood pressure,eti ni 'WIVU'.Yaani ina maana wote waliokufa kwa ugonjwa huwo ni WIVU.Au ina maana nyie wote wenye uwezo huwa hampati huu ugonjwa?,Na mdau uliesema kuwa mtu mwenye wivu,sura yake inakuwa mbaya na anazeeka haraka,,Hivi jamani wote nyie wenye uwezo sura zenu zinamvuto?,Hapa mimi naona kwamba mnachukulia kila masikini ana wivu kwa tajiri.Na kusema eti mtu asokuwa na kitu aulize mwenzie aliefanikiwa amueleweshe,hili nakataa watu wengi majiri hawatoe siri zao na wala hawataki maendeleo ya wenziwe,,kila ukimuona tajiri kajaliwa na Mwenyezi Mungu,na hao masikini huwa wanajitahidi kadiri wanavyoweza lakini Mungu anakuwa hajajalia,,kama kweli wote tungekuwa matajiri na masikini angekuwa nani,,Mfano mzuri ni Mitume wote wa Mwenyezi Mungu,walikuwa ni masikini ispokuwa Nabii Suleiman.
    Nyie watu wenye uwezo huwa mnahisi mnaonewa wivu,wewe J.Dee ni mfano wa yote hayo uliyoyasema,ni kweli huwezi kumuelekeza mtu awe kama wewe,pia huwa una majibu mabaya kama mdau alivyosema hapo juu,,mimi mwenyewe siku moja mara ya kwanza tu kukutana na wewe ile kukusalimia,,yaani ulivyoact niliona mwenyewe vibaya nikajuta kwa nini nimekusalimia,,hiyo unayojichekesha kwa watu ni promo tu ndugu yangu,,,,Kama ni uwezo ni wako,,amekupa Mungu,,na kuhusu maisha ya watu kama huna jinsi ya kuwasaidia waache na Mungu wao.siku zinaenda.Wivu wanaokuonea ni jadi yao,,sidhani kama itakupunguzia chochote,,kuliko kutoa mada katika blog kama hizi kuwakandia watu kisiasa,,,zidi tu kuwasimanga katika nyimbo zako,,Ubalikiwe mama!

    ReplyDelete
  38. Inanza DHARAU, inafuatia WIVU mwisho inageuka CHUKI...!

    Isipokuwa mada ameieleza vizuri sana kuwa zipo aina mbili za WIVU:

    1.WIVU WA MAENDELEO:, mtu anauliza kwa nini na mimi nisijitahidi nipate?,,,mtu wa namna hii anaweza muuliza aliemtamani na kumkubali kuwa anacho.

    2.WIVU WA SITAKI:, mtu anafanya kila jitihada kukwamisha au kuhujumu na hafurahi au kumkubali aliye kuwa nacho.

    Aina ya wivu wa waliowengi ni No.2 hapo juu ambao huanzia kwenye DHARAU inakuja WIVU na mwisho inafikia kwenye CHUKI!

    ReplyDelete
  39. Ukiwa na mafanikio lazima utaonewa wivu tukubali tusikubali!

    Jamaa mmoja ilimtokea siku moja alikutana uso kwa uso na mtu ambaye inaonekana alimfahamu jamaa tokea akiwa hoi, sasa alivyomuona tu na unajua Neema ya Mungu ikikushukia haina siri, utang'ara utapendeza...sasa ile uso kwa uso ,,duhhh jamaa aliguna kwa kushangaa hadi akatoa upepo pyuuu(ali ja....ba),,,Muonewa wivu alisikia lakini akajikausha kama hajamsikia!

    Manabii wa Mungu walionewa WIVU sembuse ije kuwa sisi na Mafanikio yetu ya BAHATI?

    ReplyDelete
  40. Watu wanahangaika na Maisha wanakwama, sasa leo wewe unachezesha mipango unatoka kimaisha lohhh lazima wajinga watakuchukia!

    ReplyDelete
  41. Ni bahati mbaya sana katika maisha yetu Wanaadamu hasa Waswahili, inatokea BAD WISHERS(Wakuombeao mabaya) wanakuwa wengi zaidi kuliko WELL WISHERS(Wanaokuombea mafanikio)!

    ReplyDelete
  42. WIVU;

    Sayansi hii imekuwa

    -Kikwazo kikubwa cha maendeleo katika jamii wa Binaadamu!.
    -Utenganishi wa hali ya juu miongoni mwa watu.
    -Dhuluma kubwa sana na Fitina imejiri kutokana na wivu.

    HII KITU INA DHAMBI KUBWA SANA MBELE ZA MWENYEZI MUNGU!

    ReplyDelete
  43. Asanteni wadau wooote kwa kuchangia mada hii inaonekana imewagusa wengi, kila mtu ameongea points nzuri kwa yule aliyekosoa na yule aliye support wote mmefanya kazi nzuri kwani sehemu yoyote ile wanapokuwa zaidi ya watu wawili huwa wanatofautiana kimawazo na jinsi yakuelewa mambo. Lakini at the end wote mnakuwa katika jungu moja mnafikia muafaka na mnakubaliana hoja zenu life goes on! Kila mtu amepata somo hapo na ni mada iliyo na changamoto kwani inagusa maisha halisi ya mwanadamu. Ila inaonyesha pamoja na watu kutofautiana at the end sote tunaikubali kazi yake ya usanii na tunampenda huyu dada! Asiyempenda atakuwa ana WIVU na maendeleo yake. Ila tujue kwamba ametumia haki yake ya kikatiba ya kuwa na uhuru wa Mawazo Sheria Na.1 ib.5 pitia katiba yako ya sasa kwa ufafanuzi zaidi. Big up Jide
    Ni mimi Jide's Senior Advivor

    ReplyDelete
  44. we mpuuzi wa juu hapo..nani kasema dharau huzaa wivu?? Nikikudharau maana yake sikuonei wivu..wivu na dharau haina uwiano

    ReplyDelete
  45. Ebana kweli - tena siku hizi wenye wivu wana makundi ya kupeana sapoti. Huyu ataanzisha jambo ilhali anajua ni uongo ili mradi tu amchafulie mwenzie CV kisa Wivu - sasa akishalianzisha wale wote waliokuwa wakimuonea wivu jamaa wanaunga azimio kila mtu anapiga upande wake - jamani!
    chuki ya nini? wivu wa nini? mgawa riziki ni Mungu pekee na kila alivyoumbwa mtu na vyote alivyojaaliwa ni kutoka kwa Mungu mwenyewe.
    ANONYMOUS hapo juu amewaambia: MUNGU Hana mshirika sana sana atamzidishia na wewe kukupa lana pamoja na kizazi chako! ASANTE MUNGU KWA KUWA WEWE UNAGAWA SAWA SAWA NA MAPENZI YAKO, NA UTAWAZUILIA CHINI WENYE ROHO NA NIA CHAFU.

    ReplyDelete
  46. HAYA NI SMALL TALK, MAONGEZI YA JAMII YA KIMASKINI. UKIANGALIA SANA JIDE NI MTU MDOGO TU KWENYE JAMII ANAJITAHIDI KUPATA MLO, PA KULALA, KUSOMESHA WATOTO. HAYA MIMI NAONA NI YA KAWAIDA. ALAFU ANAKUWA PARANOID ANAONGELEA WIVU, CHUKI, PROBLEMS!. GIVE US A BREAK! WALIOFANIKIWA NI KINA MENGI, BAKHRESSA,ETC KWASABABU WANAAJIRI WENGI NA KUSOGEZA NCHI MBELE.

    david m

    ReplyDelete
  47. Anonymous wa Sat Feb 04, 08:42:00PM 2012

    we mpuuzi hapo juu...wivu na dharau havina uwiano

    WEWE NDIO MPUUZI SANA TU,..UNAWEZA MWONEA WIVU MTU BILA CHANZO AU SABABU?...UNAFIKIRI MOTO HUANZA NA MOTO?...ELEWA MOTO HUANZA NA CHECHE...INAANZIA NA KUTOKUMTHAMINI MTU KWANZA (huu ndio mwanzo wa dharau na ndio mwanzo wa wivu wenyewe)!

    ReplyDelete
  48. UNAPOFANIKIWA:

    Kaa tayari kukabiliana na WIVU, FITINA,MAJUNGU,MASENGENYO,HILA,SHARI,KUFUATILIWA na mengine mengi na mwisho wa yote ni kubwa lao CHUKI!!

    ReplyDelete
  49. Wewe Mdau david m...Anonymous wa Sun Feb 05, 10:43:00 AM 2012
    Huko kwa MENGI na BAKHERESSA walikofikia Matajiri ni mbali saaana, Watu tuna maindiana, tunafuatiliana kimaisha, tunakwamishana, tunatoleana macho kwa maendeleo madogo tu ya uwezo wa Ugali wa Dona na Kunde!

    ReplyDelete
  50. Mdau wa 46 hapo juu david m...huko walikofikia MENGI na BAKHRESSA ni mbali sana!.

    Watu tunatoleana macho kwa uwezo wa kubadili mboga na uwezo wa kulipa kodi ya nyumba kwa mwaka!

    PANA JAMAA YANGU ENEO MOJA JIJINI DAR ALIINGIA MWAKA 2008 KTK NYUMBA YA KUPANGA UPANDE MZIMA, SASA JAMAA AKAWA ANALIPA KWA MWAKA MZIMA UWEZO AMBAO NI WA KAWAIDA SANA,,,ISIPOKUWA KWA WAKAZI WA ENEO HILI WALIONA NI KIOJA!...MATOKEO YAKE WAKAWA WANANONG'ONA KUWA WANAHISI JAMAA NI ''CHUMA ULETE''

    mnaona sasa? WIVU haid kwenye uwezo wa kubadili mboga na kulipa kodi kwa mwaka?

    ReplyDelete
  51. NDIO MAANA NIMESEMA HAYA YA KUONGELEA CHUKI, PROBLEMS NI KUWA NA MISIMAMO HASI, HAYATUSAIDII, HATUHITAJI. TUACHANNE NAYO.JIDE AACHE KURUDI NYUMA NA UJINGA UJINGA HUU...ANGALIA MBELE, ANDIKA MAMBO PROGRESSIVE.

    david m

    ReplyDelete
  52. Wewe Mdau Anonymous wa Tue Feb 07,09:49:00 AM 2012

    david m,

    Hatuwezi kusinga kwenda mbele wakati tunarudishana nyuma!

    Sababu za kurudishana nyuma amezichambua Jide kwa mapana na marefu...ametoa kwa pande zote mbili WIVU...(CHANYA) na(HASI)

    Wivu wa Maendeleo na Wivu wa Chuki
    kwa bahati mbaya sana idadi kubwa ya wenye WIVU ni HASI...WIVU WA HAPANA, SITAKI IWE VILE!

    ReplyDelete
  53. Wewe Mdau Anonymous wa Tue Feb 07,09:49:00 AM 2012

    david m,

    Hatuwezi kusinga kwenda mbele wakati tunarudishana nyuma!

    Sababu za kurudishana nyuma amezichambua Jide kwa mapana na marefu...ametoa kwa pande zote mbili WIVU...(CHANYA) na(HASI)

    Wivu wa Maendeleo na Wivu wa Chuki
    kwa bahati mbaya sana idadi kubwa ya wenye WIVU ni HASI...

    Ndio wale wanaofikia kupata Mashinikizo ya Damu,Msongo wa mawazo na kukosa usingizi, Mapafu kujaa maji na kushindwa kupumua,Viharusi kwa kupooza,Vifafa na Wakapinda midomo huku midomo kuwa wazi bila kufunga kwa Madege dege ya Ukubwani!...sababu za kufikwa na yote hayo, kisa?

    WIVU WA HAPANA, SITAKI IWE VILE!

    ReplyDelete
  54. Mada imejitosheleza kabisa kwa mtu aliyekuwa na akili timamu atatambua!

    MAUDHUI:

    WIVU endelevu ////WIVU usio kuwa endelevu:

    Anaekataa ukweli wa Mada atakuwa katika wale wale mabingwa wa Fitina atakuwa sio mwenzetu!

    Daima mpinga maendeleo ya wenzie kwa wivu ni yule ambaye ''ndani ya moyo wake pana kimba la mavi limejificha'' anaweza kukenua meno kwa kicheko cha danganya toto lakini siri i moyoni mwake!

    Anakuwa hataki, atafanya kila liwekezakano, iwe kwa gharama bila gharama, kwa Fitina, Majungu,mipango, Uzushi,Unafiki, Usaliti, na mengine mengi ahakikishe mtu unakwama!

    ReplyDelete

  55. WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
    Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
    that will make you rich and famous in the world and have
    power to control people in the high place in the worldwide
    .Are you a business man or woman,artist, political,
    musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
    in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
    instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
    home.any where you choose to live in this world
    BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
    1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
    2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
    3.A Dream House bought in the country of your own choice
    4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
    destination.
    5.One year Golf Membership package
    6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
    Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
    account every month as a member
    9.One Month booked Appointment with Top 5 world
    Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
    If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
    or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com

    ReplyDelete

  56. WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
    Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
    that will make you rich and famous in the world and have
    power to control people in the high place in the worldwide
    .Are you a business man or woman,artist, political,
    musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
    in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
    instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
    home.any where you choose to live in this world
    BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
    1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
    2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
    3.A Dream House bought in the country of your own choice
    4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
    destination.
    5.One year Golf Membership package
    6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
    Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
    account every month as a member
    9.One Month booked Appointment with Top 5 world
    Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
    If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
    or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...