Mwalimu wa watoto wenye ulemavu wa Kusikia (katikati) akitoa mafunzo na maelekezo kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia wakati mmoja wa watoto wenye ulemavu wa kuoana akichangia mada.
Watoto wenye ulemavu wa macho wakielekea kupata kifungua kinywa wakati wa mapumziko mafupi ya semina hiyo.
Na Woinde Shizza,Arusha
Jamii ya watu wenye ulemavu nchini wameomuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete kuteuwa wawakilishi wa watu wenye ulemavu ili kuingia katika mchakato wa kutoa maoni ya undwaji wa katiba mpya.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa shirikala walemavu linaloshughulikia haki za kisheria za maendeleo ya Jamii na Uchumi,Gidion Mandesi wakati wa semina ya siku moja ya watoto wanoishi wakiwa ni walemavu.
Alisema kuwa wanamuomba Rais kutumia busara katika kuunda tume hiyo ya watu 32 kuwepo na watu walau watatu ambao ni walemavu ambao watawawakilisha wenzao katika mchakato huo.
Alisema kuwa kunawalemavu wengi ambao wana elimu ya kutosha na wanauwezo wa kutoa maoni yao kwa niaba ya wenzao hivyo wangefurahi sana kama nao wangeshirikishwa katika sakata hilo la kutafuta katiba mpya.
'ili katiba iwe ya haki kwa kila mwananchi ni lazima kila mtu apewe nafasi ya kuchangia maoni yake kwa hiyo tunaomba sana Rais atushirikishe na sisi walemavu katika mchakato huu wakusaka katiba ili nasisi tuweze kuibariki katiba hiyo "alisema Mandesi
Aidha alibainisha kuwa iwapo Rais atateuwa wawakilishi wenye ulemavu kuingia katika tume hiyo basi ushiriki wao utakuwa ni bora nawataweza kutoamaoni mazuri ili katiba hiiyo itoe fursa pia kwa watanzania wenye ulemavu.
Mandesi aliwataka watanzania wenye ulemavu kujiandaa kutoa maoni yao ili katiba hiyo iweze kuwasaidia na kuwanufaisha watanzania na kizazi cha kesho.
Hatahiyo alitoawito kwa watanzania wote kuwapatia fursa kwa kuwa wanaulemavu wanauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko katika nchi ya Tanzania
naungana nao walemavu wanastahali mchango mkubwa kwenye mmarekebisho ya katiba. Kusema ukweli wamesahauliwa kupita kiasi. Mtu asiyejua maumivu yao kwa undani hawezi kuwanufaisha inayotakikana, na walemu wasomi wapo. Tunaomba serekali iswanyime nafasi hii.
ReplyDelete