Wazazi, Walezi na Wananchi wa maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar, wametakiwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na mtandao wa biashara haramu ya dawa za kulevya hata kama ni watoto wao ili wachukuliwe hatua za sheria.
Afisa Habari wa Jeshi la Polisi zanzbar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Maghari Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, wakati akizungumza na wananchi wa shehia za Mkele alipokuwa akitoa elimu juu ya Utii wa Sheria bila Shuruti.
Katika mkutano huo, Kamanda Aziz amesema endapo kila mmoja wetu atatii sheria za nchi bila ya kushurutishwa na kushiriki katika kutenda maovu na kutoa taarifa za wahusika wa dawa za kulevya ni wazi kuwa tatizo hilo nmiongoni mwa vijana hapa nchini linaweza kupungua au kumalizika kabisa.
Amesema pasipo kutii sheria ni wazi kuwa mbali ya wafanyabiashara wanaoingiza na kusambaza dawa hizo kila mtumiaji anayetumia dawa hizo, nyuma yake kuna kundi kubwa la watu wanaoathirika kwa njia moja ama nyingine.
Katika mkutano huo baadhi wananchi wakiwemo vijana ambao ndio kundi kubwa la waathirika wa dawa na vitendo vingine vya kihalifu, wameelezea umuhimu wa Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii katika kusaidia kukomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo wananchi hao wamesema katika eneo la Mkele pamoja na maeneo jirani, wananchi wamejitahidi kuwakemea na hata kuwatolea taarifa Polisi watumiaji wa dawa za kuilevya na wizi wa mali za watu.
Wakiongozwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, hivi sasa Kila Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Zanzibar anafanya juhudi za kuwaelimisha wananchi juu ya utii wa Sheria bila kushurutishwa ili kuepuka kutenda makosa pasipo kujua.
Wafichuliwe kwani nyinyi Polisi hamuajui wenye biashara ya unga, acheni kuzuga tekelezeni wajibu wenu kidhati.
ReplyDeleteyes acha wakamatwe na nchi nzima iwe hivyo
ReplyDeleteWa Zanzibari ndugu zetu ninyi wengi wenu ni Waislamu na Ulevi wowote hata kama ukilewa majani ya chani ni 'harram'
ReplyDeleteHatutegemi ninyi kwa sifa njema ya baadhi yenu muwe kundi hili baya.
ACHENI KUSHIRIKI ULEVI NA UHALIFU MKUBWA HUU.
MWOGOPENI MWENYEZI MUNGU JAMANI!
Ahamada Umelewa, Ahamada umelewa!,
ReplyDeleteAiiiii aaaaaaa Aiiiii aaaaaa,
Ahamada Umelewa, Ahamada umelewa!,
Mnnhhhhhh, lakini ulevi wenyewe sio wa Tembo bali ni wa vumbi la poda weee!
Toba Makubwa!