NA Mery Ayo,Arusha

WANAWAKE wa jamii za Wafugaji katika Wilaya ya Longido Mkoani hapa wametakiwa kufuata sheria na kanuni bora za uzazi wa mpango ili kuepusha madhara mbalimbali kama vile vifo, na familia kubwa ambazo
haziwezi kupatiwa huduma za msingi.

Rai hiyo ilitolewa jana na afisa Muuguzi wa Wilaya hiyo, Bi Jocye Mwanga wakati akiongea kuhusiana na hali ya uzazi katika wilaya hiyo ya Longido,mkoani hapa.

Bi Joyce alisema kuwa Jamii za kifugaji hasa katika wilaya hiyo bado zinaonekana kutokubali huduma mbalimbali za uzazi wa mpango kwa kuwa zina hofu mbalimbali hasa za kimila na desturi hali ambayo ina
sababisha kuwepo na madhara mengi.

Aliongeza kuwa bado wapo baadhi ya wanawake ambao wanaogopa huduma hizo kwa kile wanachodai kuwa huduma hizo zina madhara ndani ya miili yao hali ambayo nayo huchangia kuwepo kwa madhara na matatizo makubwa sana.

“Bado jamii hizi zinakabiliwa na changamoto ya kuamini mila na desturi hali ambayo inafanya washindwe kupenda huduma hizi za uzazi wa mpango lakini kutokana na hali hiyo bado sisi kama wataalamu tunafanya
jitiada mbalimbali za kuhakikkisha kuwa wote wanatumia huduma hizi ili kuepukana na madhara mbalimbali”alisema Bi Joyce.

Alisema kuwa ni vyema kama wanawake wakatumia fursa mbalimbali ambazo Serikali imetoa sanjari na kutumia ushauri wa Wataalamu mbambali wa afya ili kuepusha madhara ambayo yanatokea kwa wanawake ambao wanatumi a njia za Kimila na desturi.

Akizungumzia hali ya uzazi salama kwa Wilaya hiyo ya Longido alisema kuwa bado kuna tatizo la baadhi ya Wanawake Kujifungulia zaidi Majumbani, pamoja na Suala la Ukeketaji kwa baadhi ya watoto wa Kike.

Hataivyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo bado Halmashauri ina mikakati mbalimbali ya kuendelea kutoa elimu zaidi ya uzazi ili kuepusha madhara ambayo yanawapata baadhi ya wanawake katika wilaya hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Waacheni hawa jamani kwa nini mnawaletea mambo yenu ya uzazi wa mpango. Pesa mchukue nyinyi, midawa yenu muwapatie hawa masikini wa mungu. Hawaombi chakula wala msaada kwenu period!

    ReplyDelete
  2. Kuna sheria ya uzazi wa mpango Tanzania? Au Tanzania imekuwa China?

    ReplyDelete
  3. hamna sheria ya uzazi wa mpango Tanzania msituletee mabalaa hapa ebo!!

    ReplyDelete
  4. leave them alone

    ReplyDelete
  5. Uzazi wa Mpango kwa Staili ya Marekani ya Kengele, Nyota ya Kijani na Cheza Salama ni balaaa na Maafa zaidi ya Suluhisho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...