Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi aliyepiga umbali mkubwa zaidi, Vivienne Mwaulambo wa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011 katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula-Mfugale ambaye benki yao ilidhamini mashindano hayo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi wa jumla wa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011, Halima Makame yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC Katika Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi wa tatu wa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011, Violet Peter katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi.
Mmoja wa viongozi wa DGC kitengo cha gofu ya wanawake, Stephanie Sayore (kulia) akikabidhi tuzo kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula-Mfugale kwa kutambua mchango wa benki hiyo kufanikisha mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011 katika viwanja hivyo juzi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (wa pili kulia) akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa kitengo cha gofu ya wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011 yaliyodhaminiwa na NBC katika viwanja hivyo juzi. (Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula-Mfugale).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mama Tibaijuka 'wakola muno'.Fanya mpango NBC walete tawi dogo Muleba,siku hizi kunachangamka siyo kama zamani,lami(Uganda-Rwanda,Burundi-Mwanza),umeme wa uhakika kutoka victoria falls, Uganda,hakuna mgawo..,wafanya biashara mashuhuri wa kutoka kwenu Nshamba,wamejaa!!Tuko pamoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...