Ajali mbaya imetokea usiku huu barabara ya kuelekea tunduma eneo la iwambi kati ya gari aina ya toyota hilux na daladala aina ya toyota hiace mtu mmoja amefariki ambaye alikua dereva wa  gari pick up toyota hilux na majeruhi wanne waliokuwa kwenye dala dala hilo

Mke wa mmiliki wa basi la dala dala akilia kwa uchungu kuwa gari hiyo haijamaliza hata wiki tangu wanunue inapata ajali analia akisema sasa umaskini umeingia katika familia yao
Habari kamili tutawaletea kesho asubuhi
(Picha kwa hisani ya Mbeya yetu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hapo lazima kuna mambo ya overtake.Haiwezekani gari zigongane uso kwa uso kama kila dereva amebana upande wake.Mungu awasaidie majeruhi wapone haraka,nawapa pole familia ya huyo dereva wa 2.8

    David V

    ReplyDelete
  2. kweli watu wameweka mali mbele kuliko maisha . yaani ajali imetokea roho imepotea ata haimuumi ati analilia gari. Ninavyoamini kama mungu hajataka uwe tajiri ata iwe vipi huwi na kama utajiri basi utakua tu tajiri ata kitokee kitu gani.

    Allah atatufumbua macho sisi wanadamu.
    amin

    ReplyDelete
  3. Mama kwa kweli anasikitisha amerudi kwenye umasikini. Lakini yote ni mipango ya Mungu. Amshukuru Mungu na kujirudi pia kwani la kwake hilo mbona ni dogo kuliko la wale/yule aliyepoteza maisha na familia yake? Mali atapata nyingine, uhai ni wapi unapatikana?

    ReplyDelete
  4. Nimechoka na Wabongo wenzangu kumsingizia Mungu kwa kila ajali inayotokea. Eti ulikuwa ni mpango wa Mungu kwa ajali hii. Tuanze kuwa Responsible na kujilaumu wenyewe kwa uzembe wetu. Hivi vifo haviletwi na Mungu bana.

    ReplyDelete
  5. Hapa msimlaumu huyu mama. Habari za waandishi wengi wa Kitanzania zinapotosha. Hapa ni mwandishi kafikiria tu kwamba mama atakuwa anaweza pesa yake. Lakini nijuavyo mimi, vyombo vya usafiri kama magari vimekatiwa bima. Kwa hiyo inapotokea ajali mbaya ikawa gari aliwezi kufanyiwa matengenezo, kampuni alikoweka bima wanampatia pesa kulingana na thamani ya gari kabla ya kupata ajali. Of course, kiasi anacholipwa ni: buying price 'minus' depreciation value. Chonde chonde, waandishi muache kupotosha!

    ReplyDelete
  6. Mama analilia gari badala ya maisha ya watu! Kweli ubinadamu hakuna. Gari utanunua lingine lakini roho ya mtu anazaliwa nayo na hakuna aliyezaliwa mara ya pili.

    ReplyDelete
  7. Hivi huu ujinga gani?
    Kuwa na gari kwani ni utajiri?
    Na kutokuwa na gari je inamaanisha umasikini?
    Mbona wabongo tunafikira potofu kiasi hiki?

    ReplyDelete
  8. daladala ni mtaji wa kuingiza pesa ambazo zitakuwezesha kuyamudu maisha vizuriyawe na unafuu kuliko ambaye hana kipato, kwa lugha nyingine utajiri. wewe mdau hapo juu ndo mwenye fikira finyu, use your head to think!

    i hope alilikatia bima....otherwise mbombo jilipo!

    ReplyDelete
  9. Kama kila kitu ni mapenzi ya mungu mnatafuta nini mahosipitali kuhudumiwa?.

    ReplyDelete
  10. Kama hilo gari lilikuwa na comprehensive insurance hakuna haja kwa huyo mama kulialia. Au hilo gari lilikuwa halina bima?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...