Mfanyabiashara katika soko la Usa River wilayani Meru, Mariana Raymond akimwombea mgombea wa ubunge katika jimbo la arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Joshua Nassari wakati alipotembelea katika soko la Usa River kuomba kura kwa wafanyabiashara wa soko hilo jana.
 Mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari akiombewa na bi Asha Meneji wakati wa ziara yake katika soko la Usa River jana.
 Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Usa River wakimshangilia mgombea wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari, alipozuru katika soko hilo kuomba kura jana.
 Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Usa River wakimshangilia mgombea wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari, alipozuru katika soko hilo kuomba kura jana.
 Hedikopta ya Chadema ikipasua anga Arumeru mashariki
 Godbless Lema akiwasili kwa mbwembwe
Na Zitto Kabwe
"Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi navyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu". Haya yalikuwa baadhi ya maneno yangu katika hotuba ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuzindua kampeni za chama chetu katika viwanja vya Leganga katika mji mdogo wa USA River wilayani Arumeru.
Siku moja kabla ya siku ya uzinduzi nilikuwa najisomea makala mbalimbali kuhusu Wilaya ya Arumeru. Pia nilitumia muda mrefu kuzungumza na wananchi wa Meru ili kujua uchaguzi huu una maana gani kwao. WaMeru wengi niliozungumza nao waliniambia namna wanavyochukizwa na ukosefu wa Ardhi kwa wananchi. Baadhi waliniambia kwamba Kama Serikali haitachukulia suala la Ardhi kwa uzito wake Meru kutatokea vurugu kubwa sana.
Vurugu Meru sio Jambo jipya kabisa. Inakumbukwa kwamba miaka ya 1950 kulitokea fujo na wananchi kuchomewa nyumba zao ili kupisha wakulima wakubwa kutoka Afrika Kusini (makaburu) katika eneo la Engarananyuki. Vurugu hizi ndio zilipelekea WaMeru kuchanga fedha kumpeleka ndugu Jafet Kirilo huko Umoja wa Mataifa kutetea Ardhi ya Wameru mwaka 1952 kufuatia vurugu za mwaka 1951. Licha ya juhudi hizo bado Ardhi ni tatizo kubwa kwa wananchi wa Meru.
Mashamba makubwa ambayo walipewa walowezi wakati wa Uhuru yaligawiwa kwa familia chache sana Meru. Wanasiasa walijipa mashamba makubwa na mengine mpaka Leo hayakugawiwa. Ujamaa na utaifishaji wa mashamba haukufanyika Meru kwa mshangao mkubwa sana na hata mashamba ambayo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliagiza wapewe wananchi walipewa Wabunge, Madiwani, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri (soma Brian Cooksey kuhusu uwekezaji katika Maua, June 2011).
Hivi Leo Ardhi kubwa ya Meru imeshikwa na matajiri na kulimwa Maua. Kilimo hiki cha Maua mwaka 2008 kiliingizia Taifa fedha za kigeni takribani tshs 150bn. Hata hivyo kuna malalamiko makubwa sana ya wananchi wanaofanya kazi katika mashamba haya kuhusu malipo duni na nyenzo za kufanyia kazi. Kuna malalamiko kuhusu kemikali na madawa yanayotumika na  afya ya mfanyakazi kutozingatiwa.
Ifahamike kwamba Benki ya Rasilimali Tanzania inasimamia mikopo ya zaidi ya tshs 50bn ambazo kampuni za Maua zilipewa kwa Dhamana ana ya Serikali. Katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, suala hili liliibuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TIB kukiri kwamba hakuna kampuni umeanza kulipa mikopo hii. Ni dhahiri Serikali itajikuta inalipa madeni haya yaliyokopeshwa kwa kampuni binafsi! Hii pia inaonyesha namna amabvyo serikali inafanya haraka na wepesi kusaidia wawekezaji kuliko wananchi wanaoteseka na kukosa Ardhi ya kulima na kujipatia ruziki.
Wawekezaji wanapewa Ardhi na mtaji!
Haya ndio yanajenga hasira ya wananchi wa Meru. Hasira hii kwa vyovyote itahamishiwa katika sanduku la kura ili kumpata Mbunge kutoka miongoni mwao atakayeweza kusimama kidete kuhakikisha Ardhi inapatikana kwa wananchi wa Meru. Kwa nini huko nyuma, katika chaguzi zilizopita Jambo hili halikuwapa hasira wananchi? Ni dhahiri hapakuwa na Mwanasiasa ambaye ana uwezo mkubwa wa kulieleza na kuwapa imani wananchi. Ndugu Joshua Nassari amedhihirisha kwamba analijua tatizo hili kwa dhati kabisa. Nilivyomsikiliza akiongea katika kampeni, na pia katika mazungumzo yetu binafsi amenithibitishia kuwa ni mwanasiasa kijana mwenye kipaji kikubwa katika kujenga hoja na ku articulate masuala ya msingi.
Changamoto nyingine kubwa kwa Meru ni haki ya kupata Maji. Meru kuna Maji mengi sana lakini matajiri wenye mashamba wameyazuia Maji hayo na hivyo wananchi wa kawaida hawapati Maji ya kumwagilia mazao Yao na pia kwa matumizi ya nyumbani. Hili nalo linajenga hasira kubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Ardhi na Maji ni masuala yanayokwenda pamoja wilayani Meru.
Mwisho kabisa nimeona makundi ya vijana wasio na ajira na hivyo kukosa Kipato. Vijana wengi wanashinda kwenye stendi za mabasi na kuita abiria. Ukosefu wa Ajira kwa vijana Kama tusemavyo kila wakati ni changamoto kubwa sana kwetu viongozi na hasa viongozi vijana. Natumai ndugu Joshua Nassari atahusisha suala la Ardhi na Maji katika muktadha mzima wa Ajira na Kipato kwa wananchi wa Arumeru Mashariki. Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi kati ya kuwa na Ardhi au kuendelea kutokuwa nayo. Ni uchaguzi muhimu kwa watu wa Meru. Wasio na Ardhi watamchagua mgombea atakayesimamia mgawo wa Ardhi unaozingatia haki. Mgombea huyo ni mgombea wa CHADEMA ndugu Joshua Nassari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. dalili zinaonesha CCMagamba 0 vs CDM 3...............WARUDISHE MPIRA KATI TU SASA

    ReplyDelete
  2. Kaka Joshua umefanana na baba yako!! Proud of you and i will pray for you, but ukipata ubunge usiende kulala na kuishi Dar to enjoy ur life, angalia moshi wana barabara nzuri but Arumeru tuna moja tu inayokwenda Nkoaranga Hosp. All da best brother
    Your own sister
    Uk

    ReplyDelete
  3. hiv ccm huwa wanashinda vp?

    ReplyDelete
  4. La muhimu Arumeru Mashariki , Wapiga kura muwe makini na Wagombea waliotajwa kwa tuhuma za Rushwa kwa kuwa:

    1.Imethibitika Kisayansi kuwa RUSHWA ina uhusiano wa karibu na UFISADI.

    2.Angalieni tofauti yenu kimaisha kati ya ninyi mnaoshi kwa kutandika magunia Soko la Usa River mkiuza mboga za majani ili mkono wende kinywani na wale wenye mazizi ya ng'ombe na mbuzi wanao chinja wakijisikia uchu!

    Wenzenu wa Rombo walifanya uamuzi wa busara kwa kummwaga Mramba licha ya takrima zake!

    Sasa akili kichwani kwenu!

    ReplyDelete
  5. watu wasikubabaisheni, watanzania hawatabiriki.

    ReplyDelete
  6. sio kweli hao watu wengi wametoka sehemu mbalimbali za arusha wapiga kura hapo ni asilimia ndogo sana ya hao unaowaona, ngoja tusubiri uzinduzi wa ccm nao.

    ReplyDelete
  7. CHAMA CHA UDINI HUKOHUKO...!

    ReplyDelete
  8. MMh!Igunga ilikuwa hivihivi mbwembwe nyingi! CCM ikazoa kura sasa sijui.. Mpira dk 90 tusubiri tuone!!

    ReplyDelete
  9. Hapo UMATI WOTE wa 'Mgambo wa CHADEMA' upo chini ya Ulinzi wa AKINA RAS MAKUNJA KAMILI!!!,,,GUSA UNASE UFUNGWE PINGU,UZAME LUPANGO!

    Msije mkaleta mambo yenu ya mafujo kama Mbeya na Arusha, mtafungwa!

    Kutoka nje ni baada ya Uchaguzi kuisha!

    Sasa akili kichwani ufanye fujo usipige kura, au tulia upige kura?

    ReplyDelete
  10. Chadema mtambue kuwa hii ni POLISI sio USHARIKA WA KIDINI wala PAROKIA,,,,MKILETA MCHEZO MTAMEZWA NA MAMBA!!!

    ReplyDelete
  11. Hii ni Polisi au Idara ya Usalama wa Raia,

    Jamaa wana Mabomu, pingu, Bastola, Machine guns, wana Magari kama nyuki na Pay Roll ya uhakika,,,Uwezo wao kiuendeshaji hawana kuchangishana ktk Mabaa na Mikopo kupitia SACCOS!

    Fanyeni Kampeni kwa kufuata sheria na taratibu, kanuni, utulivu na ustaarabu!

    Chadema mkileta Pyeee, Arumeru Mashariki ohhh, ohhh, ohhh, mtatawanyika na kukusanya viatu kimoja kimoja na ndara moja moja,,,unakuta shati limechanika kwa kipondo imebaki ukosi tu,,,mmekufa! nyundo ya chuma imewaangukia hakuna atakaye pona!

    ReplyDelete
  12. Magwandazzz

    Mkianza ile mipango yenu 'kavu' ya Mbeya na Arusha, Lohhh Dunia itawaangukia!

    Hao jamaa msifikiri hizo ni Magwandazzz kama yenu na kuwa mpo sawa, la hasha hao Jamaa zao ni KOMBATZZZ na wana mafunzo ya KUKATA CHEMBE!

    JE MPO TAYARI KUFANYA UCHAGUZI AU KUKATWA CHEMBE CHA VIFUA???

    LETENI MCHEZO MUONE!

    ReplyDelete
  13. Msifikiri hao ni Mgambo wenzenu,,,ohhh hao ni Kikosi kazi Wana wa Ras Makunjas!

    ReplyDelete
  14. Halafu CDM tazemeni ninyi mmevaa makaki yenu ya Mgambo, Magwandazzz halafu mpo nyoro nyoro laini laini mmeshiba ndizi na mtori!

    Wenzenu wamo ndani ya Kombatzzz na ukiwaangalia wakavu wakavu!

    Sasa tieni maguu hapo muone kazi!

    Wacheni mchezo kabisa na Polisi!

    ReplyDelete
  15. A coward dies 1000 deaths before his actual death (Mnyonge au Mwoga hufa mara 1000 kabla ya kifo chake). Vitisho siyo maendeleo jaribuni ushauri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...