Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya akipanda kwenye ndege inayomilikiwa na Kampuni ya Auric Air Services Ltd leo katika uwanja wa ndege wa Mwl. J.K. Nyerere Dar es Salaam kama ishara ya kuzindua rasmi huduma ya safari za anga kutoka Dar es Salaam kwenda Sumbawanga Mkoani Rukwa itakayoendeshwa na Kampuni hiyo, huduma hiyo haikuwepo hapo kabla. Kampuni hiyo itakuwa inaendesha safari zake siku ya Jumatano na Jumapili ambapo gharama za safari hiyo kwenda na kurudi itakuwa Dola za Kimarekani 370$ sawa na takriban Tshs 598,000/= kwenda na kurudi. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Utumishi ,mm0ja Yambesi, Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Huduma za Ndege ya Auric Air Services Ltd Deepesh Gupta na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Mohammed Chima 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akimkabidhi Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Huduma za Ndege ya Auric Air Services Ltd Deepesh Gupta zawadi ya Ua na Kadi kama pongezi na shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuanzisha huduma ya safari za ndege za abiria kutoka Dar es Salaam-Sumbawanga Mkoani Rukwa kupitia Mbeya leo katika uwanja wa ndege wa Mwl. J.K. Nyerere Dar es Salaam. Kampuni hiyo itakuwa inaendesha safari zake siku ya Jumatano na Jumapili ambapo gharama za safari hiyo kwenda na kurudi itakuwa Dola za Kimarekani 370$ sawa na takriban Tshs 598,000/= kwenda na kurudi. Wanaoshuhudia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Mohammed Chima, Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal na Katibu Mkuu Utumishi Daud Yambesi,


Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipanda ndege ya Kampuni ya Auric Air ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa huduma hiyo kwa safari ya kuelekea Sumbawanga Mkoani Rukwa leo 
 Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini (CCM) Aeshi Hillal alikuwa sehemu ya abiria 13 waliopanda ndege hiyo leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Sumbawanga Mkoani Rukwa katika uzinduzi wa huduma hiyo. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa kwa ushirikiano na Mbunge huyo pamoja na wadau wengine ndiyo matunda ya muwekezaji huyo Mkoani Rukwa. 
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambesi ambaye pia ni Mwanarukwa akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari. Hakusita kuelezea furaha yake
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya akiwa na  Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Huduma za Ndege ya Auric Air Services Ltd Deepesh Gupta (kushoto kwake), Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Mohammed Chima (kushoto), Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal (kulia) na Katibu Mkuu Utumishi George Yambesi muda mfupi kabla ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam leo kuelekea Sumbawanga Mkoani Rukwa katika sherehe za uzinduzi wa huduma hiyo.
Ndege ya Auric Air itakayoendesha huduma za anga za kampuni hiyo ikiwa katika maandalizi ya safari ya leo kutoka Dar es Salaam kwenda Sumbawanga Mkoani Rukwa. Picha na mdau Hamza Temba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. dolari 370 one way Dar to S'wanga?

    London to DSM return pia ni dolari 370!

    Pamoja na hayo pongezi kwa kuanzishwa safari ya route hiyo .

    Mdau
    London

    ReplyDelete
  2. Naomba kurekebisha jina la Katibu Mkuu Utumishi ni George Yambesi na sio Daudi Yambesi.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kwa jitihada za kupanua uchumi na maendeleo kwa taifa

    lakini kwa upande wangu mimi siwezi kupanda hivyo videge hata bure maana naona kabisa maisha yapo mkononi mwe!

    ReplyDelete
  4. mdau London,
    umenunua wapi ticket toka london to tz kwa dola 370? Mbona natafuta ticket kwa mwezi sasa na sijaona hata moja chini ya £600?

    I am serious nijulishe kwa kupitia anuani hii mr_taymour@hotmail.co.uk

    ahsante

    ReplyDelete
  5. US dolar 370? allowance ya mizigo ni uzito gani? Mbona nahisi kama bei ni ghali mno kiasi kwamba wafanya bisahara wa kipato cha juu peke yao ndio wanaolengwa hapa?

    ReplyDelete
  6. haya, mkumbuke kuipeleka service on time na sio kuangalia mshiko tu.Hongera sana.

    ReplyDelete
  7. Very very expensive Airline fares ever !

    Dar-Sumbawanga US$ 370
    Dar-Nairobi US$ 199

    Is going to Sumbawanga such expensive than going to Nairobi ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...