Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Meck Sadick akiongea na waandishi wa habari jioni ya leo juu ya bomoa bomoa ya nyumba za mtaa wa Gerezani zilizokuwa zinamilikiwa na shirika la Reli pamoja na mamlaka ya bandari. Zoezi hilo litafanyika kuanzia kesho saa kumi na moja alfajiri, pia amewataka wakazi wanaoishi maeneo hayo wawe wameishahama katika maeneo hayo kabla zoezi hilo kufanyika. Amesema zoezi hilo litafanywa na kampuni ya Yono action mart ili kupisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo kasi.

Wawakilishi kutoka wakala wa serikali (DART)pamoja na (YONO ACTION MART)wa kwanza kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa (DART) Bw.Cosmas Takule. Katikati  ni Mkurugenzi mtendaji wa Yono Bi Scholastica Kevela na kulia Afisa masoko Yono action mart Bw. Joseph Assey. 
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. sasa hii serikali hawa wawekezaji kwanini wasiwatafutie eneo jipya wakawa wanatanua mji?na mji ukwa wa kisasa inakuwa vp mpaka wafanye mjini na utakuja kukuta hilo eneo halitawatosha huo ndio ukweli kituo kama hicho kinatakiwa kiwe nnje ya mji na mabasi yawe yanapita tu mjini sio kukaa mjini ni aibu serikali hamfikiri advance map?mdau bwegenaz ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Huku ughaibunimiradi hiyo yote ipo lakini gereji na depo zake hazipo mjini au katikati ya mji zipo nnje ya mji na mabasi yanapita tu mjini kuweka hicho kituo hapo ni kuongeza msongamano mjini na uchafu tu hamna lolote mlichofanya na pia eneo hilo haliwezi kutosha kabisa kama kweli mnasema mradi huo,mdau bwegenaz ughaibuni,mstahiki meya tembeya uwone miradi ya miji inayoendelea utakase macho acheni kuchafua mji na kuongeza msongamano na ikiwa bado kuna nafasi za kutosha maeneo ya wazi.

    ReplyDelete
  3. Haw DART Wanatuchezea akili wamekua wakibomoa nyumba za watu kwa kisingizio cha mabasi yaendayo kasi.

    NI MWAKA JUZI TU TULIONA WATU WAKIBOMOLEWA NYUMBA HAPO SHAURI MOYO WAKIDAI NI KITUO CHA MABASI YAENDAYO KASI LEO TUNAONA KUNA ICD IMEOTA HAPO INAITWA (TOLL)LABDA WATUPE UFAFANUZI NIMAGARI YAPI YAENDAYO KASI WANAYOZUNGUMZIA MANAKE TULIAMBIWA BY 2010 MRADI UTAKUA UMEMALIZIKA.

    KAMA WAMESHINDWA KUTEKELEZA HUO MRADI WASICHEZEE AKILI ZA WATU.

    INAUMA SANA!!!

    ReplyDelete
  4. yono ACTION mart hii itakuwa mpya ile ya ubabe ya zamani ilikuwa inaitwa yono AUCTION mart

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...