Baadhi ya vijana wakiokoa mali zao kutoka katika nyumba za Bandari na Reli mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam ili kupisha kituo kikuu cha mabasi yaendayo kasi. Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Mahakama kutupilia mbali kesi waliyokuwa wamefungua wakaazi hao na serikali ya Mkoa wa Dar es salaam kuchukua hatua chap chap
Picha iliyopigwa juu ikionesha eneo linaliotarajiwa kujengwa kituo cha mabasi yaendayo kasi
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Afande Faustine Shilogile akikagua hali ya usalama katika eneo la tukio.
Mabaunsa wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart wakiwa wameimarisha ulinzi
Juu na chini yanaonekana matingatinga yakibomoa nyumba hizo
mbona hii bomoa bomoa imekaa kama vita vile, ni kwamba hawa watu hawakupewa taarifa au!
ReplyDeletehayo mabasi yaendayo kasi yatakuwa yanapita barabara zipi?
ReplyDeleteMabasi yaendayo kasi? jamani naomba mnitoe ushamba.
ReplyDeleteSASA SERIKALI NDIO INAFANYA KAZI. PAMOJA NA KWAMBA NASHABIKIA UPINZANI LAKINI KWA HILO LILILOFANYIKA SERIKALI YETU INAHITAJI PONGEZI WALA WASIWE NA WASIWASI WA KUPATA KURA..KWA HILO NAWAFAGILIA. MPAKA LINI WATU WATAZUIA MAENDELEO? WATANZANIA WAMEDEKEZWA SANA NDIO MAANA UVUNJIFU WA SHERIA UMEKUWA KITU CHA KAWAIDA...MARA WATU WAMEJENGA KWENYE VYANZO VYA MAJI MILIMANI, MARA WAMEVAMIA ROAD RESERVES, JUU YA MABOMBA, NA KARIBU NA NGUZO ZA UMEME. KILA SIKU HAKUISHI MATATIZO KISINGIZIO..CHAMA KIMESHIKA HATAMU.HAPO RAIS NA SERIKALI NZIMA NAWAPA TANO MNASTAHILI KUPONGEZWA.
ReplyDeleteTUNATAKA BARABARA ZENYE HADHI NA WATU KUWA NA UTAMADUNI WA KUFUATA SHERIA.
Na mimi ngoja niulize 'mabasi yaendayo kasi' ni yapi? Maana mabasi yaliyopo sasa Tanzania yana uwezo wa kwenda mpaka 'maximum speed' na kuzidi iliyopo kwa mjibu wa sheria za barabarani (80 km/hr). Sasa hayo wanayotaka ni ya kwenda 150 km/hr au 200 km/hr? Maana speed kwa magari ya mjini, hata si 80 km/hr, ni chini ya hapo. Maana hata kama yatakuwa express kwa kujengewa barabara zake, lakini vilevile yatatakiwa kusimama vituoni kushusha na kuchukua abiria, japokuwa tunategemea vituo vyake viwe vichache. Isije kuwa tena 'MSAADA KWENYE TUTA'
ReplyDeleteSiyo mabasi yanayokwenda mbio tu,ni Eurostar wanajengea reli.
ReplyDeletehivi hawa waliojenga viwnja wamepimiwa na nani-yaani miaka yote hiyo serikali haijajua kuna travellers?
ReplyDeleteDART::::Mabasi yaendayo kasi kila la kheri!
ReplyDeleteKinachonitia imani ni Mkandarasi wa Mradi kuwa Mjerumani, na kama tujuavyo Mjerumani ana rekodi nzuri Duniani kwa usimamizi na uendeshaji wa mambo.
La muhimu ni kufikia matekelezo kamili na Ufanisi baada ya muda mrefu wa Mpango huu kuwa kiganjani.
Wenzetu walijenga barabara na reli za chini ya ardhi na kujenga vituo vya mabasi vya chini ya ardhi (underground rails and stations) tangu miaka ya 1905 sisi hadi leo zaidi ya karne hatujaweweza kuwafikia. Leo hii wananchi wanyonge waliouziwa nyumba na viwanja wanakuja kubomolewa. Kwanini wasizijenge hizo barabara za mabasi yaendayo kasi chini ya ardhi kupunguza msongamano!!!!kuwabomolea watu nyumba zao ni kurudisha nyuma maendeleo pia, ilitakiwa hizi nyumba ziimarishwe kuwa za kisasa na kuwapa makazi bora ndio maendeleo.
ReplyDeletemadereva, makondakta na wafanyakazi wa mabasi hayo nao watatoka ujerumani? au ni hawa hawa wa daladala na wanaotoka uda? kama ni hawa wa uda na daladala basi mimi naujua mwisho wa mradi huu!!
ReplyDeleteSasa kituo hiki ,kitakua mali ya serikali au ndio mradi wa wajanja kwa kupitia jina la wawekezaji? kama alivyosema hayati Mwl.Nyerere ukoloni unarudi kwa jina uwekezaji
ReplyDeleteNawaonea huruma hao wanaofanya kazi ya kubomoa, hasa kwenye suala la health yao na safety, Hizo nyumba zina asbestos materials, sijui hatua gani serikali yetu imechukua kuwawezesha hao wanaofanya kazi ya ubomoaji na wanaosimamia ili kujizuia na vumbi la asbestos.
ReplyDeleteNawashauri wale wote wanaofanya kazi katika eneo hilo wachukue tahadhari na baada ya zoezi hilo waende kupima afya zao, na ikibidi wachukue hatua za kisheria dhidi ya serikali ili walipwe fidia