Beki wa timu ya Dira, Makubuli Ally (kushoto) akijaribu kuwazuia wachezaji wa IPP, wakati wa Bonanza la waandishi wa habari (Media Day) lililofanyika Msasani Beach jijini Dar es Salaam leo. Bonanza hilo limeandaliwa na TASWA na kudhaminiwa na TBL. Dira ilishinda 3-1.
Mchezaji wa Kick Boxing wa timu ya Free Media, Agness Yamo, akipambana na mchezaji wa TSN, Adam Amon wakati wa Bonanza la waandishi wa habari (Media Day) lililofanyika Msasani Beach jijini Dar es Salaam leo, na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Agnes Yamo alishinda kwa Pointi.
Waandishi wa Habari toka vyombo mbali mbali nchini wakiwa kwenye Bonanza hilo la waandishi wa habari (Media Day) lililofanyika Msasani Beach jijini Dar es Salaam leo, na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.
Du huyo mama hapo juu naona teke lake amelenga pabaya kweli. kila nikiangalia damu zinasisimka.
ReplyDeleteAhhh Shangazi upigaji wako upo nje ya kanuni za Mchezo ni vile kuna mipaka ya maeneo ya kupiga,,,zaidi ya hapo ni kuelekea kutoana kizazi na kuingizana kwenye Utasa!
ReplyDeleteMnhhh baada ya kuchapwa teke la namna hiyo, 'chakula cha usiku' kitakuwa hakipandi kabisa !
ReplyDelete