TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI

Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini
kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana
mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si
chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana
haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa
kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi
kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya
Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.

KATIBU MKUU - MAT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Ha ha ha ha!!! Tayari mmeishiwa nyinyi. Endeleeni na huo mgomo basi ili sisi tufe na nyinyi muishi milele.

    ReplyDelete
  2. Wamefanza nn hao kina Mponda na Nkya? hebu uelezeeni umma wa Watanzania ni kwa nn mnawaita maadui wa madaktari na sekta ya afya afya kwa ujumla, maana kuna tetesi Jamaa wamebania madaktari zile ishu zao za kupiga deal za madawa yaagizwayo na serikali then mnayakimbizia kwa hospitali zenyu binafsi...ingawaje for me hizo rumours ni tooooo cheap ...

    ReplyDelete
  3. Sawa madaktari turingishieni kwa kuwa tunawategemea katika maisha yetu.

    Lakini muelewe kuwa bila ya wengine huo udaktari wenu hauna manufaa. Mfano bila ya mkulima kule akalima na kuleta mazao yake mjini huo udaktari utakufaa nini? Bila ya mwalimu kukufundisha utafikia hapo ulipo?

    Pili, jee ni madaktari tu ndiyo wenye mahitaji jamii nyengine hawana?

    Tatu, tukija hapo Muhimbili munatumia vifaa vya hapo na halafu munatufanyia reference kwenye hospitali zenu za binafsi ili mupate malipo ya mara mbili.

    MHESHIMIWA RAIS KUANZIA MWAKA HUU MUSIWAPATIE MADAKTARI SPECIAL FAVOUR YA KUWASOMESHA BURE. NA WAO WAPEWE MKOPO NA WALIPE KAMA HAO KADA NYENGINE. WAMEONYESHA KUTOTHAMINI JUHUDI ZA NCHI HII NA KAFARA WANAYOTOA WANANCHI WENGINE KWA MANUFAA YAO.

    ReplyDelete
  4. Hiyo imetulia. Ila fundisho moja kwa MAT. Kamwe hatuwezi kufanya maamuzi magumu nchi nzima kama hakuta kuwa na Matawi ya MAT nchi nzima yanayo tambulika kisheria. Ikumbukwe kuwa vyama vingi vya kitaaluma au kikazi, wanachama wake wanakuwa na Usajiri na Vitambulisho maalumu vya chama, pia ili kujua wanachama walio hai kila mwaka kunakuwa na Ada ya Uanachama.
    Halafu ijulikane kuwa kamwe uhuni na jazba havitasaidia kuleta umoja ndani yetu.Tujenge hoja za msingi na zenye mashiko ambazo kila mtu mwenye akili akizisika hatatubeza kama ambavyo watu wamekuwa wakutubeza kwa sasa.
    Kwa upande mwingine tumefanikiwa kutoa somo kwa serikali na wananchi pamoja na kwamba walikuwa wanaumia.
    SOLIDARITY FOREVER.

    ReplyDelete
  5. Kweli kama nikikwazo huyu waziri wa afya lazima aachie ngazi uwezi kuongoza kundi ambalo alikutaki linajua fika kuwa utendaji na usimamizi unawakandamiza unao waongoza kwa hiyo lazima atoke kwenye idala hiyo

    ReplyDelete
  6. Mungu ibariki

    ReplyDelete
  7. kuna haja gani ya kumaliza mgomo halafu mnaweka mashariti,fanyeni kama wasomi!kwa nini wasipewe ushirikiano wa madaktari hao wakuu wa wizara? Mbona mnakuwa hivi? na unapungukiwa nini usipokuwa kwenye chama cha madaktari kama una leseni yako halali?Kama mgomo umekwisha inamaana yote yamekwisha.ukikataa kutoa ushirikiano kwa maofisa waandamizi wa wizara kwisha kwa mgomo kuko wapi?Haitoshi kurudi kazini usitoe ushirikiano.Mdai yote ni ya msingi hili tu limenicheafua.Ili kuonekana waungwa mnaotaka suluhu mani yangu ni kuwa mfute kauli yenu ya mwisho,ya kutotoa ushirikiano ,sasa ikulu mlifuata nini?Bora yaisheeeeee!!

    ReplyDelete
  8. SAWA NINYI HATA MSIPOKUWA NA IMANI NAO,AU MSIWAPE USHIRIKIANO WOWOTE,SISI KAMA WANANCHI WA TZ TUNACHOTAKA MREJEE KAZINI.

    ReplyDelete
  9. Mbona breaking nyuz kwamba mgomo umeanza huwa huweki? mnafiki wewe, mchumia tumbo!

    ReplyDelete
  10. Asante Mheshimiwa Rais,.Mwisho wa siku sisi wote ni Watanzania.

    David V

    ReplyDelete
  11. Nyie bwana nadhani kazi imewachosha au imewashinda. Si mtafute kazi nyingine tu? Mlisema hamtarudi kazini mpaka hao mawaziri waondoke. Mbona hawajaondoka na mmeamua kurudi..! Mnawatuhumu watu kiasi cha kusema hamtawapa ushirikiano bila kueleza tuhuma zao, wasomi wa wapi nyie...! Eti nyie sio mashine, ina maana sie wengine wote tunaohangaika kuitumikia nchi hii pamoja na matatizo yake ni wapumbavu, sio...! Bahati yenu mimi sio rahisi, ningewatimua wote...! Shame on you...!

    ReplyDelete
  12. Tumewasikia madaktari. Tunashukuru mmerejea kazini. Shukrani za dhati kwa mheshimiwa rais Jakaya Kikwete kwa uongozi wako imara. kama madaktari walivyo na imani na wewe, jamii pia ina imani kuwa madai yao utayashughulikia kwa manufaa ya Watanzania wote. Sasa jamani turudie shughuli kujenga taifa.

    ReplyDelete
  13. Nani Mshindi?

    ReplyDelete
  14. mawazo yangu binafsi...ningekuwa Rais kikwete hawa madaktari wote ningewapeleka vijijini na ingekuwa hakuna ruksa ya wao kukanyaga mjini mpaka wapate barua kutoka serikali za mitaa..mbona dikteta Nyerere alitunyanyasia mababu zetu kwa stail hizi na kulikuwa hakuna migomo ya kipuuzi kama hii? Kikwete watu wanakuchezea watakavyo? waadabishe halafu ingia hasara kwa kukodisha madaktari kutoka nje...achana na wapuuzi wachache..!

    ReplyDelete
  15. jirani zetu kenya wamewafukuza madaktari wao! Hawa wa kwetu wamshukuru sana Mhe Rais kwa kuwavumilia hivi. dawa yao ilikuwa kufukuzwa na kupigwa marufuku kufanya kazi kwenye hospitali zozote zile za umma.

    ReplyDelete
  16. Hamna lolote nyie! Kama mnaona udaktari wa binadamu haulipi jaribuni jembe la mkono huenda likawatoa kimtindo!!
    Mnarudi kazini na masharti kibao!! Hatakama msipotutibu kifo huoangwa na Mungu na hakuna yoyote mwenye uwezo wa kuua ni Mungu tuu!!!

    ReplyDelete
  17. mimi naomba kuelewa mitaala wanayofundishwa madaktari. ni kutibu watu tu au wanafundishwa vitu kama organisation behavior au human resource, au labor law n.k mbona wanakuwa kama sio wasomi? wanakurupuka tu na jazba.

    mimi siafiki eti mawaziri wang'oke kwa sababu wao wamesema. na sisi tukiandamana kusema ulimboka na wenzie viongozi wa MAT wanyang'anywe leseni kwa sababu waliitisha mgomo na ulileta madhara watakubali?

    nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria na sio hisia au jazba. mnataka kujiweka juu ya kila mtu kwamba mmesema! hakuna kitu kama hicho

    mnaweza kuweka madai yenu bila kumlaumu yeyote.

    na mnaporudi kazini mkahakikishe wagonjwa wanatibiwa kwa wakati na kutoka hospitali. mara ngapi siku tatu daktari hajapita wodini, kama mngekuwa mnatuhudumia kwa wakati hata msongamano usingekuwa hivi mlivyo.

    kila haki ina wajibu

    jichunguzeni na mjitafakari. si serikali tu "inayowadhulumu" hata nyie mnaidhulumu kwa kutofanya kazi iinavyopasa katika muda na ubora unaotakiwa.

    mnashangaza

    ReplyDelete
  18. mimi hata nawashangaa hawa watanzania wenzangu,eti madaktari wa binamu,mm sipendi kuamini hilo.nadhani wangerudisha leseni za udaktari wa kutibu binadamu,wapewe leseni za bwana na bibi MIFUGO.maana niko na wasiwasi wanachodai kama hakitatekelezwa mapema ndo yale yale ya upasuaji wa kichwa unapasuliwa ngiri.madaktari mwogopeni Mungu

    ReplyDelete
  19. Tatizo ni madaktari wetu wa kibongo kujiona wako juu sana huku wanaongoza kwa kuvunja maadili ya kazi na rushwa, kulazimisha wateja kwenda hosp zao na lugha chafu kwa wagonjwa. Mnaumaalum gani ninyi? wakati kila mtaalam wa fani fulani anajenga nchi kwa nafasi yake.

    ReplyDelete
  20. MGOMO WA MADAKTARI NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI NA PIA KIMAADILI YA UTAALAAM.
    THANKS GOD MHESHIMIWA RAIS AMEAMUA KUTUMIA NJIA MUAFAKA KUONA KUWA MNARUDI KAZINI, LAKINI SERIKALI HAIJASHINDWA KUCHUKUA HATUA ZIFAAZO ZA KINIDHAMU JUU YA WALE WALIOGOMA.
    MIMI BINAFSI SITAKUWA NA IMANI NA SERIKALI ENDAPO RAIS ATALAZIMISHWA NA KUNDI DOGO LA MADAKTARI NA KUWAONDOA MAWAZIRI KWENYE NAFASI ZAO.
    UDHAIFU ALIOONESHA PM WA KUKURUPUKA KUWASIMAMISHA KAZI KATIBU MKUU NA MGANGA MKUU ULITOSHA KUCHOCHEA MGOMO ZAIDI KWA MAANA HATA WALE WALIOOGOPA KUGOMA WALIONA KUWA TUNAWEZA KUILAZIMISHA SERIKALI TENA HATA BILA KUPITIA MAJADILIANO.
    SERIKALI NA WATENDAJI WAKE WANATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZILIZOPO HASA ZA AJIRA INAPOFIKIA KATIKA HATUA ZA MIGOGORO YA KIKAZI.
    NINGESHAURI SERIKALI KUPITIA TUME YA UTUMISHI WA UMMA, NK WAPITIE UPYA SHERIA NA MIKATABA MBALIMBALI YA AJIRA ZA WATUMISHI WA UMMA ILI KUWABANA WALE WACHACHE AMBAO WANAWEZA KUSABABISHA ATHARI KWA BINADAMU WENGI KWA VISINGIZIO.
    TUFIKE MAHALI KWAMBA KAMA KAZI UNAONA HAILIPI, BASI KWA HIYARI YAKO UNAONDOKA NA KUTAFUTA KAZI NYINGINE ITAKAYOLIPA.
    WATUMISHI WA SERIKALI SI VEMA WAKATUMIA NAFASI ZAO KWA KUATHIRI HUDUMA ZA KIJAMII.

    ReplyDelete
  21. Kama kweli waliofikia maazimio niliyoyasoma ni madaktari, basi sishangai kwanini mgonjwa wa goti alipasuliwa kichwa na wa kichwa kupasuliwa goti.
    Hakuna mantiki hata moja ndani ya tamko hilo linaloweza kuhalilisha madai yao kwa mgomo.
    Shame on you

    ReplyDelete
  22. Hawa madaktari ni ---------kabisa. Huwezi kujiona wewe ni bora kuliko watumishi wengine wa nchi hii. Rais nakuomba uwape TU, yale madai ya haki wanayodai na SI kuwapa upendeleo kwa sababu eti watagoma tena.

    ReplyDelete
  23. Wengi wenu humu mnatibiwa India. Mmeshindwa kuona hoja za kimsingi za madaktari wenu. Poleni sana.

    ReplyDelete
  24. Hovyooooo..!!!
    Tutaiomba serikali kuondoa upendeleo wa aina yoyote kwa kundi hili
    Hovyo Sana Hawa watu tena wapelekwe mahakamani kwa kusababisha vifo Kama wanavyopelekwa wanasiasa the HaGue wauaji wakubwa hawa
    Hovyo kabisa

    ReplyDelete
  25. Jamaa zao wanaharakati kina kina Annanilea Mkiya na Bi Bisimba na chama chao CHADEMA tuwasikie sasa maana walitaka maandamano yaendelee fujo ziendelee kama walivyoenda salender bridge na hawakupata support ya mwananchi yeyote zaidi ya vibaraka wao walivyokuja navyo, sasa wakapinge na hili. maana hiyo haki ya binadamu ya kufukuzisha mtu kazi haikutimia.

    ReplyDelete
  26. "Kikwete watu wanakuchezea watakavyo?, waadabishe halafu ingia hasara ya "KUKODISHA" madaktari kutoka nje.

    ANGALIZO: matimizi ya kiswahili:
    neno, KUKODI linatumika pale tunapoingia mkataba wa matumizi ya kitu kisichokua cha kwetu.
    MFANO: Tanesco wamekodi mitambo ya DOWANS.

    Na pale tunapotoa cha kwetu kitumiwe na mtu mwingine kwa mkataba, tunasema KUKODISHA

    NB: Kukodisha kitu kisicho kua chako au usichokua nacho ni kosa kilugha!!

    ReplyDelete
  27. KWANI MSHAHARA WA MADAKTARI NI KIASI GANI JAMANI WANTAZANIA WENZANGU?

    ReplyDelete
  28. MAT ni chama cha kitaaluma, cha wafanyakazi au cha kisiasa?
    Maana naona kama nimechanganyikiwi!
    Halafu je MAT ni chama cha madaktari vijana au hata watu wazima? Maana kama juzi kwenye kile kikao chao nimeona vijana tu. No wonder busara inakosekana katika maamuzi. Au wazee wao wapo 'behind the scene'? Au hawana muda? Najiuliza tu

    ReplyDelete
  29. km sekta zote zingekuwa km MAT, i belive tungekuwa na viongozi safi na sio wale wanao jitarisha kutoka na jasho la wwalipa kodi. Nyie mnaopiga kelele kuhusu madaktari hivi ni hatua gani zimechukuliwa kwa mafisadi nani asiye wajua, madkaktari wnadai haki yao basi wasaliti, ndio miaka 50 nothing has changed in Tnzania. maskini wanazidi kuwa masikini, na matajiri wanazidi kuwa matajiri

    ReplyDelete
  30. Huu ni moshi tu kuashiria kuna moto wa kutoridhika kwa mishahara na vitendea kazi kwa watendaji katika sekta zote.

    Vipato vya watanzania vidogo havikimu mahitaji ya msingi kwa wengi na hata mahitaji kwa wadhifa mkubwa wanaokuwa nao viongozi au watendaji wengi TZ. Ndio maana wanaiba, wanaanzisha hospitali zao au mashirika yao binafsi. Rais angalia hili tusije tukawa na vita ya mawe barabarani.

    Kwa upande wenu madaktari, adui yenu sio Waziri wala katibu mkuu ila ni mfumo mzima. Mbona mnamkubalia Rais na wao mnawatenga. Inabidi nao wawemo katika chama chenu na mshirikiane nao kuleta mabadiliko ya kweli. Kwani taabu ya madaktari na hali ya hospitali zetu ni kwa ajili ya hawa wawili tu? Mbona hivi wasomi wenzangu mnaniangusha katika kuchambua suala zima?

    ReplyDelete
  31. Kweli watanzania tuna wakati mgumu.
    Mtu yeyote mwenye kufikili atajua kuwa, Mzazi kujifungulia chini(kwenye kanga au godolo) si sawa ukichukulia kwamba yeye pia ni mlipa kodi.
    Comment nyingi watu wamefocus kwa mawaziri. Mnasahau vitu vya msingi!! AFYA YA MTANZANIA. Kwa wananchi wote mijini na vijiji. Sio umekaa Dar es salaam toka utoto wako mpaka leo unafikili mtu aliyeishi Ngamboshi anapata huduma za matibabu kama wewe.
    Acheni porojo. Madaktari wanataka mawaziri wawajibike kwa kutokuwa na mikakati ya kusaidia afya ya jamii.
    Au mpaka iwe inahusu kuongezeka kwa bei ya kivuko (Kigamboni)ndio muone kitu cha muhimu????!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...