Picha na habari na Francis Dande
AZAM FC, leo imefanikiwa kukalia kilele cha Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya kuwafanyia ‘kitu mbaya’ mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga kwa kuwachapa mabao 3-1 katika pambano lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao mawili, moja kila kipindi kutoka kwa mshambuliaji anayekosa makali avaapo jezi za taifa, John Bocco ‘Adebayor’ dakika za nne na 76, na lile la Balou Kipre dakika ya 54, yalitosha kuiweka Azam kileleni kwa kufikisha pointi 41, huku Simba ikishika nafasi ya pili kwa pointi 40 na Yanga kubaki nafasi ya tatu kwa pointi 37.
Bao la Bocco dakika ya nne, lilikuwa na mchango mkubwa katika kuichanganya Yanga, iliyoapa kumalizia kwa Azam hasira za kuchapwa na kutupwa nje katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek, na kuifanya ianze kutembeza ubabe dimbani hapo.
Baada ya bao hilo, Yanga ikaonekana dhahiri kuchanganyikiwa na athari ya hili ikaanza dakika ya 11, ambapo kiungo Haruna Niyonzima ‘Fabregas alionywa kwa kadi ya njano baada ya kukaidi agizo halali la mwamuzi, Israel Mujuni, kwa kupiga mpira wakati filimbi ilishapulizwa.
Dakika mbili baadaye, akapewa kadi ya njano ya pili kwa kulalamika na kubishana na mwamuzi aliyeamuru mpira upigwe kuelekea Yanga baada ya Mnyarwanda huyo kumchezea rafu beki wa Azam.
Ni kadi iliyobadili hali ya hewa uwanjani hapo, na pambano kusimama kwa dakika tisa huku ‘mapambano yasiyo ya ubingwa’ yakishika kasi.
Fujo zikaibuka dimbani hapo, huku wachezaji wa Yanga wakimtwanga ngumi mwamuzi, vurugu zilizozaa kadi nyekundu ya pili, safari hii akioneshwa Nadir Haroub ‘Cannavario’.
Licha kuendelea kwa pambano, maamuzi ya refa yakawa ya shaka kutokana na kutojiamini tena mchezoni.  
Dakika ya 32, Hamisi Kiiza akaifungia Yanga bao lililokuwa la kusawazisha, akiitendea haki pasi ya beki Shedrack Nsajigwa ‘Fuso’.
Timu zikaenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1, huku amani ikiwa bidhaa adimu ndani ya dimba kutokana na wachezaji wa Yanga kugeuza ulingo wa ngumi. Kipre akafunga la pili dakika ya 54, kabla ya Bocco kumaliza kazi dakika ya 76.
Vurugu ziliendelea hata baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi, ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na nyenzo nyingine kuwatawanya mashabiki, huku waandishi wa habari nao wakizuiwa kuingia chumba cha mikutano baada ya kumalizika kwa mchezo.
 Akina Ras Makunja wakimsindikiza mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Azam, Israel Mujuni baada ya kutokea  vurugu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mwamuzi msaidizi, Hamis Changwalu akitoa akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Yanga Shamte Ally asimshambulie mwamuzi wa mchezo huo
Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wakimpeleka shabiki wa Yanga katika chumba cha kutoa huduma ya kwanza baada ya kuzimia Uwanjani. Kufungwa nomaaa!
 Mshabiki akishughulikiwa na kina Ras Makunja
 mashabiki wa azam
 Mrisho Ngasa wa Azam akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' wakati wa mchezo huo

Akina Ras Makunja kazini....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Poleni YANGA! Ila NGUMI tuziache kwenye NDONDI na KABUMBU ibaki kuwa KABUMBU!

    ReplyDelete
  2. EEe kumbe yanga wamekwisha namna hii!Kushindwa tu na ngumi juu!OOhh nafurahi sana Yanga kukung'guta 3 mlingoti,,Wamekoma kilimilimi!

    Ahlam ,,UK

    ReplyDelete
  3. Poleni yanga ndio mpira lazima mkubali kuna ushindi na kushindwa.

    ReplyDelete
  4. Msiyasifie haya kwa sababu katika hali ya kawaida marefa wana matatizo sana na hawa wachezaji siyo mara yao ya kwanza kufungwa na hatujawahi kusikia wametaka kumpiga refa. Tusiangalie tu ushabiki bali je hawa wachezaji walitendewa haki na mpira ulichezeshwa sawasawa?
    Waamuzi wanachangia sana katika kuharibu soka na tusiwalaumu tu wachezaji.
    Lakini wanatakiwa wajue kwamba kwa vitendo vyao vya kushindwa kumiliki uamzi hakuwatengenezei sifa nzuri na wataendelea kuchezesha mechi za mchangani tu na hatutawaona wakipata hadhi za kuwa waamuzi wa kimataifa wa FIFA ng'o!
    Lazima waweke ushabiki pembeni na kuangalia taaluma zao kwani ndizo muhimu kwa maisha yao na familia zao. Ukiididimiza timu kwa ushabiki ni kweli utafurahi kuwa timu yako uloipendelea imefanikiwa, lakini je, kufanikiwa kwa hiyo timu yako kutaleta ugali mezani kwako au kwa viongozi wa hiyo timu na wachezaji ulowapendelea?
    Hebu badilikeni na mjue kwamba maisha yenu yanaweza kubadilishwa na weledi wenu tu kwa kufanya kazi yenu nzuri na kupewa nafasi nzuri zikiwemo zile za kimataifa za FIFA ambapo mtauaga umaskini na kuondokana na pesa za hongo za kununulia pipi........
    Mdau wa Mwanza.

    ReplyDelete
  5. Ndiyo maana mpira wa Tanzania haukui, hivi huyo Mnyarwanda nani kampa jina la Fabregas? Kazi kudharilisha majina ya watu wenye kujua kazi zao. Haya mingumi kwa refa wa watu inatoka wapi? Kama mpira umewashinda anzisheni Club ya Ngumi (YANGA BOXING CLUB). Siwatusi ila mnatuboa sana nyinyi hata na mtani wako naye yaleyale, michezaji yenu ndiyo inaenda kuunda timu ya taifa, Upumbafu mtupu. Kamwe kama wachezaji wetu msipo kuwa na nidhamu mtatugharimu sana kwenye timu ya taifa.
    Aaaghhhhhrrrrr...... Mnaboa!

    ReplyDelete
  6. Yanga:Mambo yenu ya kutaka mafanikio ya haraka bila kuwekeza yatakuja kuwaletea matatizo,wachezaji hawana nidhamu baada ya kumtimua Timbe.Timbe angeweza kuwatoa hao Zamalek,mnatukera sisi mashabiki wenu..Tumefungwa kihalali,kubalini matokeo jipange na mchezo unaofuata

    David V

    ReplyDelete
  7. Ingekua Ulaya, ningesema 'canvaro'
    atafunga lkn. kwa Bongo, maamuzi yafuatayo yatafanyika;

    1)Mwamuzi ataambiwa amekosea na atackuliwa hatua.

    2)Yanga na wachezaji wake hawatachukuliwa hatua yoyote.

    Hii ndio bangi ya USIMBA NA UYANGA inavyo haribu mpira halafu tujiulize kwanini kiwango hakipandi.

    ReplyDelete
  8. pambav kabisaa!kinurraah! TFF iwazuie washabik wa yanga kwenda uwanjani wasije wakasababisha maafa kama misri,wakicheza Yanga bs wapangiwe Airwing na si stediumu ya neshno

    ReplyDelete
  9. kina Ras makunja jamani hata uruma hamna? sasa naona muziki wenu mkubwa

    ReplyDelete
  10. DUUUU HAO AKINA RAS MAKUNJA NOOOMAA ILA MLIKUWA WAPI WAKATI REFA ANAKULA KICHAPO???? MNGEMUOKOA YULEE KWANZA ....ILA NAWAAMINIA WAJOMBAA MAANA HUYOO JAMAA MLIVYO MBEBA JUUJUU KAMA SINIA LA KARAMU DU!!!

    ReplyDelete
  11. Anguko la Yanga ni anguko la Chama na Mamlaka!

    Hii ndio pale mkubwa anapokunywa 'chai ya rangi' siyo pombe halafu analewa chakari!

    ReplyDelete
  12. ingekuwa kuoneshwa kadi au kufungwa ndio kuanza ngumi, refa webb wa uingereza tusingekuwa nae, nidhamu ya wachezaji ilisababisha hadi nje ya uwanja iharibike, tutarudi ya misri si kitambo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...