Moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza vyumba viwili vya mabweni ya wasichana maarufu kama Hall 6 vyumba Block W katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE) mjini Iringa leo. 


Mashuhuda wa tukio hilo wamemueleza mwanalibeneke Francis Godwin wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika .

Walisema kuwa moto huo ulianza kuwaka katika chumba kimoja wapo ambacho ni chumba Block W muda wa saa 6 mchana na kuwa wakati huo baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha katika vyumba hivyo .

Mkuu wa chuo hicho cha Mkwawa Prof. Philimon Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la moto japo amesema kwa sasa ni mapema sana kuelezea kwa kina suala hilo na kuwa taarifa zaidi ataitoa baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika ikiwa ni pamoja na kujua madhara yaliyojitokeza na chanzo cha moto huo.

Hakuna aliepata Madhara yeyote katika tukio hilo na bado taratibu za kuokoa mali za wanafunzi hao zinaendelea.



Chumba cha wasichana katika chuo cha mkwawa kikiwaka moto


Hapa ndipo moto ulipoanzia katika bweni hilo
Chumba ambacho moto ulianza kuwaka kikiwa kimeteketea vibaya.
Polisi wakichukua maelezo kwa wahanga wa tukio hilo


Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo akichukuliwa maelezo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni Wanafunzi!

    Pia kama sio hujuma, pana uwezekano miongoni mwenu pana waovuta Sigara kwa siri ndio maana labda mtu amevuta sigara akiwa kitandani akapitiwa na usingizi moto ukashika ktk godoro na ikawa mwanzo wa Janga!

    ReplyDelete
  2. Quality ya vyuo...inatisha in 255

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...