BENKI Kuu ya Tanzania imeongeza muda wa mwaka mmoja kwa wateja wa benki zote nchini kuboresha taarifa zao kuanzia kesho Machi 15, 2012 hadi Machi 14, 2013.
Benki na taasisi zote za fedha zimejulishwa kuzingatia kikamilifu agizo hili. Agizo la awali lilitamka kwamba muda wa kuboresha taarifa za wateja wa benki ungelimalizika leo.
Mwaka jana (2011) Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo, alitoa kipindi cha muda wa mwaka mmoja kuanzia Machi 15, 2011 hadi Machi 14, 2012 kwa ajili ya zoezi hilo. Hii ilikuwa ni kuziwezesha benki zote kuzingatia kanuni zilizomo katika Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu.
Wakati huo huo, Benki Kuu ya Tanzania inawataka wananchi na wateja wa benki nchini kutimiza wajibu wao kwa kujaza fomu za taarifa zao ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kushindwa kutimiza sharti hilo la kisheria.
Imetolewa na Idara ya Uhusiano na Itifaki
BENKI KUU YA TANZANIA
Machi 14, 2012
Kwa kweli muda umeongezwa mkubwa,watu wata relax. Kama bot wapo serious,ilitakiwa kuweka short deadlines,otherwise watu inabidi ku relax
ReplyDeleteHII NDIO NCHINYETU BWANA NA MWAKA UJAO TENA SIJUI ITAKUWAJE
ReplyDeletehahahahhahah nchi hii kwa siasa mpaka rahaa...me toka mwanzo nilijua itakuwa hv..watu wamehangaika weee kupanga mafoleni sijui nini bt ss wenye uzoefu na nchi hii wala hatukujisumbua...am waiting til machi 2013 nisikie tena ni dec 2013..walitutisha about phone line registration wakaishia kuachia...tz raha sanaaaaa wajameni
ReplyDeletesasa watu tupo nje ya nchi huku kwa kipindi hiki utaratibu ukoje hapo?
ReplyDeletetuko nje huku kwa kipindi hiki.Utaratibu ukoje?
ReplyDeleteBENKI MMEFANYA VEMA KUONGEZA MUDA MAANA HUKO MIKOANI, BENKI NYINGI HAZITEKELEZI WAJIBU WAKE. HATA MTEJA AKIENDA WATAKUKATISHA TAMAA KWAMBA HAWANA UHARAKA WOWOTE WA KUREKEBISHA HIZO TAARIFA. KUNA BENKI AMBAZO HATA WATEJA WAKE WAMEAPA KURUDI KWA ZOEZI HILO KWANI USUMBUFU WANAOUPATA HAUNA MFANO. MTEJA UNARUDI BENKI MARA TATU AU NNE KUFUATA KUREKEBISHA TAARIFA. KWANI NDIO UNAFUNGUA HIYO AKAUNTI MARA YA KWANZA? WAIGE MFANO WA WAFANYAKAZI WA BENKI HAPA JIJINI DAR ES SALAAM PENYE USHINDANI.
ReplyDeleteHili zoezi linafaa kuwa ni la kuendelea (LA KUDUMU) kwa kuwa maisha na mabadiliko ya kimaisha ya mtu haya gandi, leo umeajiriwa kesho umestaafu, leo unakaa Arusha kesho unahamia Tabora.
ReplyDeleteSasa kwa msingi huo, urekebishaji wa Taarifa za mteja uendane na mabadiliko ya muda hadi muda wa maisha ya mtu.
Wangesema mtu abadili taarifa zake mpya kama zina mabadiliko ktk kila baada ya miezi sita na kwa muda wote kwa kudumu,,,hapo ingekuwa ndio sawa haswa.
HIVYO ZOEZI HALIKUFAA KUWA NI KITU CHA KUWA NA DEADLINE.