Mama Sarah Samson (Mama John) wa mbagala Charambe kwa Mbiku Mtaa wa Machinjioni kwa Maharage anayefanya kazi SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA  - MAKAO MAKUU anamtafuta kijana wake aliyepotea njia Ndugu Jofrey William Orondo (PICHANI JUU) . Kijana huyu ni mgeni hapa Dar es salaam akitokea UTEGI RORYA - MUSOMA. 

Kijana huyu alipotelea maeneo ya Kwambiku tangu siku ya Ijumaa 9/03/2012.
Kwa yeyote atakayemuona kijana huyu tunaomba atoe taarifa kituo cha polisi Zansa,Charambe,Maturubai au Maji Matitu au atoe taarifa kwa namba zifuatazo:


PICHA YAKE IMEAMBATANISHWA HAPO JUU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Duhh Poleni kwa mkasa wa kupotelewa!

    Isipokuwa Vijana wengi wa kutoka Mara haswa Wakurya wanajishughulisha maeneo ya Kongowe-Njia ya Kilwa kuendelea, na biashara ya Ufugaji wa Kuku na uuzaji wa jumla wa Mayai.

    Inawezekana Kijana amekutana na Wadau wa Kijijini Rorya na wameanza kumwingiza kwenye mipango mipya ya Maisha!

    ReplyDelete
  2. Ohhh, ametokea Musoma sio?, wala msihangaike yupo salama na afya yake!!!

    Nendeni Kongowe hadi Vinkindu mtamkuta amebeba shehena ya Mayai ktk Baiskeli huku akiendesha spidi moto chini pembeni ya barabara na akipiga miluzi!

    ReplyDelete
  3. Ahhh, Ahhh, Ahhh,

    Wasela wa Kikurya Kongowe ,Vikindu wameshampa msokoto wa Bangi, amepuliza amedata na kazi!!!,,,,wamemkabidhi baiskeli la mzigo wa Mayai anakuja njiani spidi kulelekea Mjini akipitia Mbagala!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...