Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC wakiwa na Mwanamuziki Maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania Flora Mbasha na mumewe. Kutoka kushoto, Emmanuel Mbasha, Ms. Maganga, Flora Mbasha, Mindi kasiga na Alex Kassuwi 
Mwimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini Tanzania, Flora Mbasha atembelea Ubalozi wa Tanzania katikati ya jiji la Washington DC, Marekani. Mtumishi huyu wa Mungu kupitia muziki wa injili alipata nafasi kuwa mgeni wa Mh. balozi Mwanaidi Sinare Maajar siku hiyo, ambapo Mhe, balozi huyo alizungumzia fursa mbalimbali zipatikanazo nchini Marekani na Tanzania. Aidha Flora Mbasha alimmwagia sifa Mhe, balozi kwa mafanikio makubwa ya kuwaunganisha watanzania walioko huku ughaibuni. Pamoja na hayo Flora Mbasha alimshukuru Mheshimiwa balozi kwa kazi yake nzuri hapa nchini Marekani. Zaidi ya hayo Flora alitoa shukrani za kipekee kwa watanzania waishio nchini Marekanina kwa ukarimu wao, upendo na mshikamano miongoni mwao.Mwisho Flora alitoa shukrani za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya M. Kikwete kwa kuweza kuendeleza amani na mshikamano nchini Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Florah Mbasha, kwakweli mi ni huyo mumewe ndo ameniacha mdomo mwaa, he is so handsome na mapose sio mchezo. waooh Mungu anendelee kubariki hio ndoa yenu na angalia wanawake wengine wasikunyang'anye mmeo, maana ni bonge la hand.

    ReplyDelete
  2. Mindi umependeza sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...