Mwimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini Tanzania, Flora Mbasha atembelea Ubalozi wa Tanzania katikati ya jiji la Washington DC, Marekani. Mtumishi huyu wa Mungu kupitia muziki wa injili alipata nafasi kuwa mgeni wa Mh. balozi Mwanaidi Sinare Maajar siku hiyo, ambapo Mhe, balozi huyo alizungumzia fursa mbalimbali zipatikanazo nchini Marekani na Tanzania. Aidha Flora Mbasha alimmwagia sifa Mhe, balozi kwa mafanikio makubwa ya kuwaunganisha watanzania walioko huku ughaibuni. Pamoja na hayo Flora Mbasha alimshukuru Mheshimiwa balozi kwa kazi yake nzuri hapa nchini Marekani. Zaidi ya hayo Flora alitoa shukrani za kipekee kwa watanzania waishio nchini Marekanina kwa ukarimu wao, upendo na mshikamano miongoni mwao.Mwisho Flora alitoa shukrani za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya M. Kikwete kwa kuweza kuendeleza amani na mshikamano nchini Tanzania.
Home
Unlabelled
Flora Mbasha atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Florah Mbasha, kwakweli mi ni huyo mumewe ndo ameniacha mdomo mwaa, he is so handsome na mapose sio mchezo. waooh Mungu anendelee kubariki hio ndoa yenu na angalia wanawake wengine wasikunyang'anye mmeo, maana ni bonge la hand.
ReplyDeleteMindi umependeza sana.
ReplyDelete