Wakina Mama wanaoishi kwenye Kijiji cha Sanga Sanga,Nje kidogo ya Mji wa Morogoro wakionekana wamebeba ndoo za maji huku mmoja akionekana kuelekea Kisimani kuteka Maji na Mwingine anaokena akirudi huku akiwa ni mwenye furaha baada ya kupata maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mie nadhani unatania. Ni Aibu ilioje kuona kwamba ni mafanikio au ni maendeleo
    kuwa na uwezo wa kuchota maji kisimani na kujitwika kichwani halafu kutembea hatua kadhaa kupeleka nyumbani kwa matumizi. Haitakiwi iwe hivo hata kidogo. Hii ni karne ya 21. Tusitafute visingizio. Huo ni Mfano halisi wa sera zilizofeli. Jamani tuamke na tuanze kujiuliza maswali. Hivi ndivo tuna define maendeleo?

    ReplyDelete
  2. Utajiri wote wa mito nchini miaka hamsini ya uhuru bado watu wanakosa maji safi na salama ya bomba??
    Kila siku tunaona eti uzinduzi wa visima?
    Hizo pesa za mafisadi kwanini zisitaifishwe ufanyike mradi mkubwa wa maji nchi nzima??

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na comment ya mdau wa kwanza, hii kero itaisha lini ? matatizo haya yako maeneo mengi ya nchiyetu lakini inaonekana hakuna ufumbuzi wa haraka, haileti maana mtu kutembea umbali mrefu kutafuta maji, ukiuliza wanasema mipango inafanywa kuondoa tatizo lakini hakuna linalofanyika, lakini pesa za kampeni za uchaguzi zinapatikana tena bila shida kabisa

    ReplyDelete
  4. BADALA YA KUTUMIA FEDHA KATIKA SHEREHE, TUZITUMIE KATIKA MIRADI YA KUONDOA MATATIZO YA MSINGI YA JAMII KAMA UPATIKANAJI MAJI, NYUMBA ZA KUISHI NA UMEME.

    ReplyDelete
  5. 80% wanaotoa comments zao humu wametoka vijijini, suala je yeye amekifanyia nini kijijini kwake alikotoka. yeye na wanavijiji wenzake wameshafanya harambee ya kujenga visima au kuchimba visima kwao. Mimi tangu nilipofungua macho nyumbani kwetu kuna kisima huwa kinaboreshwa na kujengewa tu kinapopata athari. Sio kila kitu. Mtu anajenga bonge la jumba mjini, kwao kijijini akienda hawezi kwenda chooni kwa sababu cha shimo, what a shame.

    ReplyDelete
  6. mdau wa pili watu wenye muono kama wewe ndio wanaochangia zaidi kurudisha maendeleo nchini na kuwaruhusu viongozi wachache wajinufaishe midhali wametia barabara nusu lami.

    ReplyDelete
  7. Maji ni kero lakini furaha ya dada aliebeba maji itakuwa inatokana na simu anyoongea nayo

    ReplyDelete
  8. Wewe unaesema tusitumie pesa ktk mambo ya sherehe unasema hivyo kwa sababu wewe ulisha OA mke kwa michango yetu sasa unataka utubanie na sisi?....swala ni budget tu

    ReplyDelete
  9. Mdau wa pili kutoka juu ni kiini cha utendaji mbovu. Tusikubali kamwe the status quo. We should always push the envelope. Ni aibu ilioje kuona uchotaji maji na kujitwika kichwani ni maendeleo.

    ReplyDelete
  10. Tatizo la maji si kero vijijini tu, mjini Dar es salaam hamna maji. Unauliza tumefanya nini kijijini kwetu!? Kwa hela zangu nilitoa bomba toka umbali wa kilomita 10 mpaka kijini kwangu maji yalikuwa yanatoka kwa muda wa mwaka 1 na kijiji kizima kilinufaika. Wengine walivuta bomba kwao toka hapo. Siku hizi maji hayatoki kabisa na idala ya maji wanasema maji hayana nguvu tena. Mabomba ni maonyesho. Na hapo hapo kijijini ni karibu na nyumbani kwa Mbunge na Waziri wa maji, Mwandosya. Na nimewaandikia barua,ongea nao kwa simu, bure. Kwa hiyo wa (Anony wa Tue Mar 20, 12:42:00 PM 2012)acha kuuliza maswali hayo kwa watu kwani hayo ni majukumu ya serikali. Maji ni haki ya kila binadamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...