Mh Zitto Kabwe akiwasili eneo la tukio.
Godbless Lema amekuwa kivutio kikubwa alipowasili jana hapa Usa river majira ya saa saba na nusu mchana kutokea Arusha.alikuwa na maandamano makubwa ya magari,pikipiki,na waenda kwa miguu.Alipokaribia tu kufika vijana wa hapa walimbeba juu wakati wote na kufunga barabara kwa muda mpaka walipompeleka sehemu ambako wageni wanafikia. Baadaye  maandamano makubwa ya kupokea viongozi watakaozindua kampeni yakafuata
Umati wa watu ukiwa unaelekea eneo la mkutano katika viwanja vya shule ya Msingi Leganza.
Waendesha pikipiki hawako nyuma kama wanavyoonekana katika picha hii.
Barabara za kutokea Moshi na Arusha zimefurika watu wakija kwenye uzinduzi wa CHADEMA.
Picha na Habari na Mdau Maalum Wa Maggid Mjengwa-Arumeru

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. People's Power in Action!

    ReplyDelete
  2. kaskazini kumekucha wazee ccm ishakufa kitambo arusha

    ReplyDelete
  3. Sio arusha tu mpaka Kigoma

    ReplyDelete
  4. Angalau blog ya jamii huwa inacover vyama vyote vya siasa,siyo kama TBC.Tunachotaka kusikia hapo ni uchaguzi huru na haki.Rushwa ni adui wa haki.

    David V

    ReplyDelete
  5. masikin wadanganyika!ewe michuzi usibanie comment hii,wadanganyika licha ya kuelekea miaka 51 ya uhuru,wanaarumeru wanaoonekana pichani wana nyuso zilizokata tamaa ya maisha wanadhan kimbilio lao ni chadema kumbe ni wale wale tu!watu wanataka sera unawafanyia nini ndani ya miaka 3,Mwenyekiti anautangazia uma ujiandae kwa shoo ya helikopta ambayo mara tu inaporuka inaacha vumbi si kawaida wana inji wanabaki na kifua kwa vumbi la shoo ya helikopta,dj mbowe na stage shows wake wanakula maziwa yenye cream halisi!nadhan badala kupoteza mamilion kwa kuziba nafasi ya wanaokufa,nafas iende kwa mshindi wa 2,si kutumia visent vya wadanganyika,jaman Tanganyika sirudi,watawala hawana mapenz na raia,tazama nao polis wamejaza magar ya kunyanyasa wasio na hatia arumeru hata yale washawasha nayo!pesa za kufanya uchaguz zitmike kwa miundombinu km brabra,zahanat,shule nk

    ReplyDelete
  6. chama cha magamba na chama cha wanamuzik wa dansi vyote tabia sawa!CCM inachagua kindugu katoka baba anakuja mtoto,wakati chama cha madensa amestaafu baba mkwe kaja mkwe! Ah tnadanganyana tu!watu wanangoja afe mtu waje kuwadanganya wananchi.EWE MWANANCHI AMKA NA USIKUBALI KUDANGANYWA NA HELIKOPTA,KANGA,FULANA NA MIA 5!HAKUNA LOLOTE.DAINI ZAHANATI,SHULE NA MAJI BANA?

    ReplyDelete
  7. pablo escaborMarch 11, 2012

    The nature of politics is like the human nature...meaning its complex, complicated, hurts and heals...at the end of the day we are losers...no winners in politics...no hard feelings 255 its all for love n better future...yep we need long view here.

    ReplyDelete
  8. Sio mchezo Mhe.Zito Kabwe akiwa chini ya wazee wa kazi akina Ras Makunja?! aka wazee wa bongo tambarare,

    ReplyDelete
  9. Very nice one,but haki itakuwepo au ndo hesabu ya kujumisha itakuwa ya kutoa na ya kutoa ya kujumlisha, vijana Arumeru msikubali wala msisikilize ya chuma chako mapema. Ss tulioko nje ya nchi turuhusiwe kupiga kura

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...