ANKAL SALAMALEKO...
NIMERUDI TENA MKUU, SAFARI HII NNA SWALA NATAKA UFAFANUZI WA WADAU WAKO LUKUKI WA LIBENEKE.
SWALA LANGU NI KUHUSU HII MITANDAO YA JAMII (SOCIAL NETWORKS) AMBAYO KWA KWELI IMELETA MABADILIKO MNO KATIKA JAMII - IMEANGUSHA SERIKALI (TUNISIA, MISRI NA LIBYA) NA IMEWEZA HATA KUMPELEKA MTU IKULU (OBAMA), KWA HILO NAIPONGEZA.
SWALA SASA JE NINI KINAFUATA (WHAT NEXT)???
NAHOJI HIVYO SABABU HADI DAKIKA HII SIJAONA MITAMDAO IKILETA MAGEUZI CHANYA (POSITIVE) KATIKA HII JAMIII YETU. SANA SANA IMEKUWA KAMA IMEKUJA KUKOSOA NA KJULETA UJUAJI WA KILA KITU, KWA KUWA TU MTU ANAFUNGUA KOMPYUTA YAKE NA KUMWAGA LAZI. LAKINI UKICHUNGUZA UTAKUTA HAKUNA TIJA KABISA KATIKA HII MITANDAO.
WADAU WA LIBENEKE HILI NAOMBA TUJADILI. NI KWELI KWAMBA MITANDAO YA KIJAMII INA UWEZO WA KUJENGA/KUBOMOA LAKINI HAINA UWEZO WA KULETA MABADILIKO MBADALA WA HAYO WANAYOYASHUPALIA???


NAWASILISHA
MDAU SALAMA LEKO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. huyu jamaa VIPI ?? David V uko wapi ?? hebu mpe vipande vyake, sasa wewe yaani hueleweki unaposema huoni faida yake ,mara wewe huyo huyo unasema imebadili serikali za Misri,Tunisia, Libya,je ? yote hayo hayakutoshi kuziona faida zake? !!! au tu unataka kukera watu humu ndani ya mtandao wetu ?? je ?? bila matunda haya ,tungekujua vipi ndugu salamaleko au ungetuma barua ! ambayo ingemaliza wiki mbili kabla haijamfikia Michuzi,na kama utatumia bahasha kubwa ,basi kuna hatari washikaji posta wakaichana wakifikili kuna chochote (pesa) na hivyo swali lako hata kwa Michuzi halingefika. Amka ndugu yangu wee !! sasa hivi ni touch button au touch screen. Faida yake ni kubwa mno, tena inabidi tumshukuru sana mzungu ambaye mimi binafsi napendekeza kwamba baada ya Mungu anayefuatia ni Mzungu, wengi huenda mtaguna-lakini sote tunajua ukweli unauma. ni mimi Zebedayo mna nasa.

    ReplyDelete
  2. mdau hiyo ni kweli haina maana tunabaki na umaskini tu,umbea mwingi tena kuna hatari watu wa nje wachache wakaharbu nchi kwa uchochezi wakati wa vurugu vifo wao wapo ulaya

    ReplyDelete
  3. Mdau hizi ndio hoja stahiki. Ninakupa pongezi kwa kuiibua. Kuhusu hoja yako ni muhimu utambue kuwa mabadiliko ni mchakato (process) na sio tukio la mara moja au tukio moja. Kwa hivyo ushupaliaji huo unaoushuhudia (km kukosoa, kujiletea ujuaji wa kila kitu, nk) katika mitandao ya kibongo ni sehemu ya mchakato huo. huna budi kuungalia 'ushupaliaji' kwa mtazamo chanya.

    ReplyDelete
  4. Kaka unapo sema huoni faida yake unamaanisha kweli au unataka kuumiza vichwa vyetu.faida moja wapo ni kutoa fikra(thought) zako kwa watu wote wasomao mtandao huo.mfano ni wewe umetoa fikra zako.Ni njia ya mawasiliano na yaharaka,nyepesi,cheap n.k.So ujumbe utakao tuma ni uupendao wewe mtumaji na walengwa ni watu wote watakao weza kusoma.Social Network is the bestiest means of communication ever.Na itaendelea ku improve within sec to sec.

    ReplyDelete
  5. mdau uliyeleta hii hojo mimi nakuunga mkono. maana mimi mwenyewe huwa nafikiria kila siku kuhusu hii social networks
    yani ukiangalia kwenye UMOJA VILLAGE ndo huwa sielewi kabisa maana ni kama watu wanashindana kuandika mambo ya watu tuu(umbea)......hatuandiki mambo ili kutatua matatizo tunaandia kwa ushabiki tuu.kweli na bado Tanzania hali itaendela kuwa ngumu milele maana hata mafisadi wenyewe wameshatujua kama tunalalamika lakini hamna tunachokifanya

    ReplyDelete
  6. Binafsi nazifagilia sana blogs kwa sababu wanakosoa watu hata na serikali na uozo wake. Tatizo l TZ ni ubabe, watu tuseme asilimi kubwa ya walio mjini hawaipendi hii serikali yetu ya sasa na tunataka mageuzi ila tatizo linakuja pale mnapopanga kufanya kitu cha kuleta mageuzi wenzako wanakugeuka kwa uwoga wao. Kukosoa redio zetu bongo, wasanii wa fleva, mpira wa bongo, na uozo kibao wa bongo ni jambo sahihi. We umeona wapi watu ama jamii inashabikia kitu ambacho hakina tija katika jamii yetu? Kwa hiyo watu wanapolalamika juu ya hili ni sawa kabisa kwani mtu huwezi lalamika bila sababu.

    ReplyDelete
  7. DUNIA KWAMWE HAIWEZI KUWA KICHAKA!

    ELEWA UNACHOKIFANYA HAKUNA SIRI(Jitahidi uwe unafanya mazuri daima) KAMA NI KIBAYA KITAANIKWA KWA KUWA HATOKI MTU HAPA KWA ZAMA HIZI!

    Mitandao ya Jamii azma yake ni kutoa uwezekano wa watu walkio sehemu za mbali zilizo tofauti Ki Joigrafia na mida tofauti kufikiana kwa urahisi zaidi na kwa kasi zaidi kwa gharama nafuu!

    Anaeitumia Mitandao ya Jamii ndivyo sivyo ni Mhalifu na inabidi aepukwe!

    Kwa aneyeichukia ujue sio mtu mwema na si mwenzetu! (Ndo wale wale hupenda kuwafanya watu wengine kama Ng'ombe na kuwa Dunia ni kichaka kwa kuwa wengine unaweza kuwafanya wengine kuwa ni wajinga kwa kuwa hawafikiani na kubadilishana mawazo kirahisi kama ilivyo ktk Mitandao ya Jamii)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...