Moja ya Magari Makubwa ya kubeba mizigo mizito likiwa limesimama katikati ya Barabara ya Mandela Road kwa na kusababisha msongamano mkubwa wa magari wakati likielekea kwenye yadi maalum ya kuhifadhia makontena ya mizigo inayotoka bandarini ambayo ipo Tabata AMI-ICT maeneo ya Relini. Hii inakuwa kero kubwa sana kwa watumiaji wa barabara hiyo na wakazi wa maeneo ya jirani na yadi hiyo,kwani kuna kipindi magari hayo yanalazimika kufunga kabisa barabara hiyo ya Mandela kutokana na uzembe wa madereva wa magari hayo kutaka kuingia kwenye yadi hiyo bila ya kufuata utartibu.
Hivi ndivyo namna inavyokuwa pindi magari hayo yanapofunga njia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...