Mama mmoja pichani ambaye jina lake halikutambulika mara moja,akiwa amembeba mtoto mdogo kama umuonavyo pichani huku akiomba msaada kwenye moja ya gari,tukio hili limetokea leo mchana kwenye barabara ya Ally Hassan Mwinyi,jijini Dar.Inaelezwa kuwa kumekuwepo na tabia baadhi ya watu kuwatumia watoto kwa ajili ya kujipatia kitu chochote,jambo ambalo linahatarisha afya na ukuaji wa malezi kupelekea kuwa si mazuri.
Home
Unlabelled
hii ni hatari sana kwa malezi ya wototo wetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Hivi Tanzania kuna Child protective services? Wizara ya kina mama na watoto inafanya nini. Hii ni Child abuse! No way around it. Huyu mama inabidi ashtakiwe na mtoto wake kuchukuliwa. mama apewe mafunzo ya kulea mtoto na asaidiwe kama inawezekana . lakini tabia ya kutumia watoto kuomba kuomba lazima ishtumie hawa wabunge wanaomba posho wako wapi?
ReplyDeleteAnonymous number 1: Mtoto ake akichukuliwa watampeleka wapi? Nchi hii tajiri, mafisadi wanafaidi hela wanaua social services! Kazi ipo!
ReplyDeleteyuko wapi yule mbunge alosema ubunge ni umasikini kabisa? labda angelibadilshana na huyu mama akaona raha za omba omba!
ReplyDeletemdau wa kwanza unajifanya umeishi miaka ming nje ya nchi kiasi umeshau maisha ya nyumbani au? eti child protection!
ReplyDeleteLa kusisitizwa hapa ni vipi Serikali italitatua tatizo la omba omba nchini, tatizo ambalo limekuwepo nchini miaka nenda miaka rudi. Hawa ni ndugu zetu ni watanzania wenzetu na wanahitaji kusaidiwa, hatujui ni sababu gani zilizowapelekea hadi kuanza kuomba omba njiani.
Kuwakamata na kuwapeleka vijijini wanakotoka sio suluhisho, suluhisho ni kuwapatia njia za kuweza kuacha kuomba omba na kujisaidia wenyewe,
Mwalimu alisema kuwa ili tanzania iendelee inahitaji mambo matatu, ardhi, watu na uongozi bora. Tukizingatia hayo basi ni hivi: - Ardhi tunayo tele, watu wamejaa tele ni uongozi unaotuangusha!
Ukiona mtu anaomba jua ana matatizo kwelikweli. Maana ni kazi ya fedheha. Pia hawapati pesa ya maana. Ni Kuganga njaa. Pia nimkosoe mchangiaji wa Tue Mar 13, 10:40:00 PM, mambo si matatu ni MANNE: Watu, Ardhi. Siasa safi na Uongozi bora. Huo ulikuwa ni mtazamo wa Nyerere, lakini kwa sasa mambo hayo si lazima ili kuweza kuendelea. Tunachokihitaji sasa ni WASOMI wenye uwezo wa kubuni MIRADI ambayo itaweza kutupatia HUDUMA zote muhimu, bila kutegemea bidhaa nyingi kutoka nje. Kwa mfano kulianzishwa SIDO, lakini nafananisha SIDO na mtoto ALIYEDUMAA. Maana haipigi hatua MBELE. Kingine ni kupata wawekezaji WAZURI ktk sekta muhimu kama vile kilimo, elimu, umeme na ufugaji, na siyo kwenye BENKI, HOTEL, SIMU, na SOCIAL CLUBS. Kwa sasa nchi yetu inahitaji RAIS DIKTETA, ambaye ataweza kuagiza kutungwa sheria ya mtu aliyetoa/kupokea rushwa kubwa au aliyefuja mali ya umma kuuliwa huku vyombo vya habari vikimwonesha. Adhabu kwa makosa haya iwe ni KIFO cha HADHARANi na si vinginevyo. Hii inaweza kujenga woga, na kumfanya kila mfanyakazi, au kila aliyepewa madaraka kufanya kazi kwa uadilifu. Hapo ndo tutaendelea. Haya ni maoni yangu tu.
ReplyDeleteNashauri kuwa omba omba waachiwe mpaka siku zao zikifika kama walivyofanywa miaka ya nyuma, lakini kwa sasa, omba-omba wanaobeba watoto watishwe na waonywe kuwa hivyo si sawa.
ReplyDeleteMdau Ano: Tues march.13 10.33PM.
ReplyDeleteNaona umeshindwa kunielewa. Nothing has to do with kukaa nje ya nchi miaka mingi! LA HASHA.
CHILD PROTECTIVE SERVICES NA SISI TUNAZO! IS MATTER OF IMPLEMENTION! TUNARUDI KULE KULE ULIKOSEMA : WATU ARDHI NA UONGOZI BORA! SASA KUNA TOFAUTI GANI YA WIZARA YA WANAWAKE NA WATOTO? KAZI YAO NINI KAMA SIO KUANGALIA MASLAHI YA WANAWAKE NA WOTOTO, NA MOJA NA MASLAHI YA WATOTO NI KUHAKIKISHA KUWA MTOTO ANA TUNZWA NA KUKUA VIZURI.. HUYO MAMA HAPO HANA MAFUNZO, HANA ELIMU, HANA CHAKULA SIAJABU HAJUI KUWA ANACHOFANYA NI MAKOSA KUMTUMIA MTOTO KUOMBA NA KUMUWEKA MTOTO KWENYE JUA NJAA, MVUA WHO KNOWA WHAT ELSE? THE MAIN GOAL FOR CHILD PROTECTIVE SERVICES IS TO MAKE SURE CHILDREN ARE NOT BEING ABUSE OR NEGLETED. THE BABY HERE IS NOT AONLY BEING ABUSE , IBUT ALSO NEGLETED. HUYO MAMA ANAHITAJI KUFUNZWA NA NANI WA KUMFUNZA NA KUMSAIDIA WATU WA WIZARA YA KINAMAMA NA WATOTO. WE AS TANZANIA WE NEED TO MAKE THESE PEOPLE WALIOWEKWA KUMSAIDIA MTANZANIA RESPONSIBLE NA ACCOUNTABLE! HATUWEZI KUENDELEA TU KUSEMA OHH WEWE HAUJI , HAUKO TANZANIA, MOST SERVICES ZILIZO NJE YA NCHI ZIPO TANZANIA KUINA SHERIA NA WIZARA ZIMEUNDWA ILA HAKUNA UTEKELEZAJI. IS ABOUT TIME THE GOVERNMENT INAKUWA FOR PEOPLE AND NOT FOR FEW MAFISADI. IT SAD TO SEE PICTURE LIKE THESE. SO SAD.
After all, where is the child's father? i do blame men to some extent!!!!!
ReplyDeletefalsafa nyiiingi, mwisho wa siku pale pale SIASA SAFI NA UONGOZI BORA!
ReplyDeleteWATANZANIA LAZIME TUJUE KWAMBA USTAWI WA JAMII WIZARA BADO IPO KAMA KWA NA NDIO IDARA HUSIKA NA M,ATATIZO KAMA HAYO, KWA KWELI NI AIBU JAPOKUWA HAKUNA JINSI HAO KINA MAMA NA WOTOTO LAZIMA WAKAOMBE MITAANI NA WANAIJUA MITAA IPI YA KUSIMAMA NA KUOMBA NI HUKO HUKO ALLY HASSAN MWINYI ROAD AMBAKO KUNA PITA MAFISADI WALIOTEULIWA NA NDIUGU RAIS MH. JAKKAYA KIKWETE. WIZARA IPO NA INA KIFUNGU KIKUBWA TU CHA KUWEZA SOLVE THESE PROBLEMS LAKINI NDIO HIVYO UTAWALA BORA HAKUNA NA TUNACHANGIWA PESA NYINGI TU KUTOKA KWA WASAMARIA WEMA AMBAO MUNGU KISHA WAWEKA WAO NDIO WATAKUWA WA KWANZA KWENDA PEPONI SIKO HIYO KUU YA UMLI KIAM (SIKU YA MWISHO) HIO NI PAMOJA NA WATOTO OMBA OMBA . LAKINI KAMA UTAWALA UMEFUNIKWA NA RUSHWA NA UFISADI MNAFIKIRI LINI TANZANIA ITAPEVUKA? UONGOZI HAKUNA KUANZIA RAIS MPAKA MAWAZIRI NA WABUNGE AMBAO TAYARI WAMEISHA ZEEKA LAKINI BADO TU WAKO MAKAZINI HAKUNA HOJA YOYOTE WANAYOITOA ZAIDI YA KWENDA KULALA KWENYE NYUMBA YA BUNGE AMBAYO NDIO SISI TUNAIHESHIMU KAMA MUNGU, RAIS HATAKI TOA AJIRA KWA VIJANA AMBAO WANGEFANYA KAZI HIO KWA MOYO NA KULETA MAENDELEO KWA KILA MTANZANIA LAKINI KAFUNGA MACHO ATI KANA KWANBA HAJUI KINACHOENDELEA NCHINI KWAKE ILA SAFARI TU ZA ULAYA NA MAREKANI ILI KUOMBA MISAADA YA KUJINUFAISHA WAO NA VIONGOZI WAKE . TANGU LINI MSAFARA WA RAIS WA AFRIKA, NA WAFUASI 30 NA MALAYA 7 HUMOHUMO? hATA MANTIKI YOYOTE BADALA YA KUWAITA WATU KAMA HAO KINA MAMA WALIOKUWA NA WATOTO AMBAO HAWAJUI WATAWAENDELEZA VIPI KI MAISHA YEYE ANAITA MIKUTANO NA WAZEE AMBAO WAMELALA USINGIZI NA KUMPIGIA MAKOFI,ILI AONEKANE ANAFANYA KAZI KUMBE POROJO TUPU! HAPOA TANZANIA KUNA NGO`S NYINGI TU AMBAZO ZINAHUSIKA NA WATU KAMA HAO WANAOKAA BARABARANI NA KUOMBA PESA NDOGO NDOGO KWA AJILI YA KUPATA ANGALAU SHS 1000 WAKALE NA MISAAADA WANAPEWA MINGI TU LAKINI HAKUNA ANEJALI ZAIDI YA KUDANGANYA NA KUJENGA MANYUMBA YA KIFAHARI KWA KUTUMIA PICCHA KAMA HIZO ZA WAOMBAJI WA BARABARANI. WE NEED A CHANGE IN SOCIAL POLITIC, AND GOVERNANCE
ReplyDeletemdau Belini , West Germany
MDAU Wed Mar 14, 02:59:00 am 2012 UKITYPE KWA KIINGEREZA unakuwa na jazba sana kiasi kwamba unafanya ERROR zisizokuwa za msingi,jaribu kupunguza jazba
ReplyDeleteWadau, huyo dada hapo juu akifyagia barabara kama wale akina mama wazee wenye wajukuu wa kusomesha, achilia mbali yeye huyu ni mwanae, atapungukiwa nini? Kubwa ni kwamba anahaarisha maisha ya huyo mtoto ama pengine si wake amemkodi kwa kiasi fulani. Tusilee huuu ujinga maana kama ni wa kuomba, basi angalu awe na ulemavu unaomfanya asiweze kujipatia kipato kwa namna yeyote ile. Huyu dada hapo juu ni msanii tu. Asipopewa hela siku 3 ataacha kuomba.
ReplyDelete