India inajipanga kuwekeza zaidi nchini Tanzania, kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya India na Tanzania kuyonyesha mafanikio makubwa.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Balozi wa India nchini Tanzania, Bibi Hemalata Bhagirath, wakati alipotembelea mradi matrekta ya Kilimo Kwanza, unatekelezwa na shirika la SUMA JKT, eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Bibi Bhagirathi amesema inchi yake, imeridhishwa sana na utekelezaji wa mradi huo, unaohusisha matrecta 1860 ya Farmtrack kutoka India kutokana na mkopo wa Dola Milioni 40 za Marekani, na matrecta hayo kukopeshwa kwa wakulima wa Tanzania, ili kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia mpango wa Kilimo Kwanza.

Balozi Bagirathi amesema, kufuatia mwitikio mzuri kwa Watanzania kwa matrekta hayo, nchi yake inaweza kuangalia uwezekano wa kufungua kiwanda cha matrekta hayo humu nchini ili kutosheleza kabisa mahitaji ya Kilimo Kwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Suma JKT, Co. Ayoub Mwakang’ata, ameishukuru serikali ya India kuwezesha kupatikana kwa mkopo wa mradi huo na kusisitiza kuusimamia vizuri ili fedha za mkpo huo zirudi na faida.

Balozi Baghirati na Mkurugenzi wa SUMA JKT, Co. Mwakang’ata, wanaeleza zaidi.

Ili kutekeleza sera ya Kilimo Kwanza, serikali imeyapunguza bei matrekta hayo ya SUMA JKT kutoka Shilingi Milioni 26 mpaka Shilingi Milioni 16, Iili wakulima waweze kumudu kuyanunua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...