Niliposafiri kwa mara ya kwanza nje ya nchi, nilisahau ufunguo wa sanduku nyumbani. Nilipofika kiwanja cha ndege wakati wa kukaguliwa, nilitakiwa kufungua sanduku ili kupunguza baadhi ya vitu, lakini kwa kuwa sikuwa na ufunguo, ilinilazimu ama niliache sanduku zima lirudi nyumbani au nichane na kuondoa vitu na kulisafirisha likiwa na hitilafu.


Wakati nikiwaza cha kufanya, mfanyakazi mmoja anayeshughulika na mizigo alinihurumia, akaniita pembeni, akaniuliza kama nina kalamu (bahati nzuri nilkuwa nayo), akanielekeza jinsi ya kufungua na kufunga sanduku bila kutumia ufunguo wala kuharibu kufuli. Nilifanikiwa kulifungua na kupunguza mizigo, uzito ukaenea, nikaendelea na safari.


Hivi majuzi ndugu yangu amepoteza laptop iliyoibwa kwenye sanduku alilolisafirisha. Nilijaribu kumwelezea kwenye simu jinsi wizi huu unavyofanyika, ndugu yangu hakunielewa hadi nilipommtumia video inayoonekana hapo chini.


USHAURI wa jinsi ya kuhifadhi vifaa vyako kuepuka udokozi: Unaposafiri na vitu kama vile laptop, tablet, simu, kamera, iPod, mp3 player, au kifaa chochote cha thamani kubwa lakini kinabebeka (portable) kwenye mkoba wa mkononi, tafadhali viweke vifaa hivyo kwenye mkoba huo kwani huo unahesabika kama carry-on na unaruhusiwa kuingia nao kwenye ndege (soma tiketi yako ina maelezo ya idadi na uzito wa carry-ons unazoruhusiwa kuwa nazo) na hivyo utakuwa na uhakika mara zote wa vitu vyako "kibindoni" tangu mwanzo hadi mwisho wa safari.

Kama itakulazimu kuviweka vifaa hivyo ndani ya sanduku litakaloingia kama mzigo hadi mwisho wa safari ndipo ulipokee sehemu ya kuchukulia mizigo, basi hakikisha unavificha vifaa vyako ndani, katikati ya sanduku na kuweka nguo na vitu vingine juu ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote kuona au kuhisi kuwa kuna kifaa kama laptop kwa maana kuacha laptop juu ikachora alama na taswira ya laptop, hii ndiyo wadokozi huiona na kushawishika kufungua na kuiba.

Source: http://www.wavuti.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. wewe ndio unajua leo!

    ReplyDelete
  2. swali langu ni moja tu kuhusu hili maana shemeji yangu aliibiwa laptop yake pale julius nyerere int. airport desemba 2011 akiwa anasafiri kurudi zake sweden, tena walimtime maana walimona yeye ni mzungu.
    1. Je waziri wa usafiri wa anga Tanzania anakubaliana na hili tatizo kuendelea hapo kiwanjani ili na sisi tufuate ushauri huu wa jamaa? au yupo tayari kulitatua haraka saana. maana lilipofikia ni pabaya. mpaka leo hii mimi binafsi nishawalipa wafanyakazi wa ndani ya airport hiyo kunipelelezea nani alimwibia shemeji yangu vitu vyake siku ile, na tayari wameshanipatia majina kamili ya wahusika hao. linalofuatia nataka kumtafuta hitman awafanyizie. silaha mkononi tu kama waziri hatatui hili suala haraka. maana huwezi kukubali kuibiwa vitu vya gharama ya $20000 alafu hakuna solution. wakati kumlipa mtu kati ya hao hao wezi akutafutie aliekuibia kati yao ni laki mbili tu ($100) na ya kumfanyizia mwalifu ni laki tano ($250). Na umeshawakomoa pia.

    Michuzi usinibanie hii comment nipo serious.

    Mdau UK

    ReplyDelete
  3. HII VIDEO MICHUZI UNGEFIKIRIA KABLA KUIWEKA WATAIGA SASA NA KUIBA VITU.

    ReplyDelete
  4. duh dogo ingawa nakupa ahsante kwa kututahadharisha na haya lakini umeshau kuwa umeshawapa funzo zuri watu wa airport. Kumbuka wezi wanachukua chochote kila hata nguo almuradi wataweza kuuza.

    Michuzi ondoa hii kabla vibaka wengi hawajaiona.

    ReplyDelete
  5. Kwa msaada zaidi tu juu ya suala hili ningependa kuongezea kidogo juu ya usalama wa mabegi yetu tunaposafiri. Hii issue ya kufungua begi kwa kutumia peni na kufunga ni pindipo tu aina ya begi lenyewe lilivyo! Ikiwa begi ambalo baada ya kutia kufuli then ikawa ina uwezo wa kufuli yenyewe kuzunguka begi zima hio ni hatari sana ... Tupendelee kutumia mabegi ambayo baada ya kulock zile zeep zisiwe na uwezo wa kutembea. nina maanisha kuwa kuwe na hook ya kuweza kuzizuwia zisitembee au passcode lock. Kama inavyoonesha kwenye clip vipi ameweza kulifunga tena kwa kuwa zip yenyewe imeweza kuzunguka unless asingeweza. Hapo tutakuwa salama na mizigo yetu.

    ReplyDelete
  6. Airport mbona wanajua siku nyingi hiyo maana mie nilishaibiwa sana pale na mmoja wanaobeba mizigo alinielekeza wanavyoiba ni hivyo hivyo

    ReplyDelete
  7. mbona hii njia ipo siku nyingi.mimi mwenyewe nilicargo mizigo toka uk (2003) wakati wa kuichukua kule DAHACO nikagundua nimepoteza funguo za masanduku,wakati wa ukaguzi ikabidi wale wafanyakazi wa pale walifanya hivyo hinyo kutumia kalamu wakasema tunakusaidia tu lakini usimwambie mtu.

    ReplyDelete
  8. mabegi ya siku hizi zip ikishabanwa haitembei, kufuli haitumiki, bali begi lenyew lina lock kwa juu pale, then zip yabanwa...so mtu hawezi kuitembeza, so akishafungua kwa pen lazma aliache begi wazi

    ReplyDelete
  9. Mimi nina hasira na TRA na Airport hawa watu kuna siku nitawakamata tu, vitu vingine vinatia hasira. Huku kwa malkia nilishapoteza simu yangu mara 3 niliiacha University ninaposoma lakini kila nikiisahau napatiwa asubuhi yake kwa reception, Halafu cha ajabu unaiba unampatia mtoto wako, inamaana unamlisha mtoto wako laana. Michu nikiandikaga comment huzitoi cku hizi kulikoni? Tuache tu baba ilimradi hatujapigana

    ReplyDelete
  10. Waziri wa anga anafanya nini, kuwa atahakikisha uizi wa vitu vya abiria, tanzania hali mbaya kwani wale wapi sasa, nchi ina wenyewe. maendeleo yetu yako mbali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...