Nimepokea maswali na maoni mbalimbali baada ya kuweka hapa video yenye maelekezo ya jinsi inavyowezekana kufungua sanduku kupitia kwenye zipu bila ya kufungua kufuli.

Wapo walioripoti kuwa vitu vyao viliibwa kutoka masandukuni na makufuli yalikuwa yamefunguliwa au kuonesha dalili ya kuchokonolewa ama hayapo kabisa. Kutokana na shuhuda hizo, wengine walitoa ushauri wa kutumia aina fulani ya makufuli ambayo yamepigwa chapa ya mashirika (agency or department) yanayohusika na usafiri kwa baadhi ya nchi, mfano TSA, ATS n.k. nami nikawafahamisha, hiyo nayo si dawa muafaka kwani hata hayo nayo yanaweza kufunguliwa.

Makufuli yoyote bila kujali aina na muuneo, yaani yawe ni yale ya namba (combination locks) au ya funguo mfano Tri-Cicle, Tri-Cycle, T-lock, Diamond, au ya chapa za TSA, ATS n.k. hayo yote yanaweza kufunguliwa kirahisi.

Video zifuatazo zinaonesha jinsi ya kufungua makufuli hayo bila ya kutumia ufunguo au kujua 'combination' ya kufuli.

USHAURI: Kama nilivyoeleza kwenye ushauri wa jinsi ya kusafiri na vitu kwenye carry-ons, ikiwa umeweka vitu vya thamani katika sanduku, ama (1) lipia waranti ili chochote kikibiwa ulipwe (yapo mashirika mbalimbali yanayotoza waranti kwa kulipia gharama kiasi fulani, bofya hapa kuona mifano) au (2) ulizia kwenye kiwanja cha ndege unakoanzia safari ikiwa wanayo huduma ya kuzungushia nailoni kwenye masanduku yako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. I think this is serious
    Without you intending...
    Unatupa maarifa ya kuwa wizi

    ReplyDelete
  2. Makufuli ya kichina ikiyapiga ngumi tu yanafunguka!!

    ReplyDelete
  3. sasa wewe ndo unazidi kuwapa ujanja watu wa airport Dar, sina hamu walivyoniibia vitu. yaani naanda mpango wa kusafiri na bomu nali-activate sanduku likifika Dar

    ReplyDelete
  4. Kuna kufuri aina ya SHENGLI nawezaje kulifungua paspo kutumia funguo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...