Na Deogratius Kilawe
Dunia sasa ni kijiji hamna namna ya kufanya kuepuka,ni uwanja wa kukabiliana na yote hayo mazuri na mabaya,Nimekutana na mikasa mingi hapa kwetu afrika watu wengi wakitumia intaneti pasipo faida ya kiuchumi au kijamii na kuwaletea majanga ya kupoteza rasilimali muda pasipo sababu rasmi.
Mara kadhaa imenitokea wakati nikiwa miaka ya mwishoni mwa 1990’s na mwazoi mwa mwaka 2000’s wakati ndio nilikuwa nipo sekondari nikiingia intaneti café pasipo sababu maalumu,mara nimefungua tovuti hii,ile na kwa kuwa sikuwa najua tovuti mbalimbali nikabaki najua google,yahoo,na baadhi tu,lakini kumbe kulikuwa na tovuti muhimu sana ambazo nilikuwa nakosa kupata taarifa nilizokuwa nazihitaji.
Nimeamua kwa moyo mkunjufu kushirikiana na umma kujua hili jambo,naamini sio wote lakini ni wengi huingia mitandaoni pasipo au hutaka kupata taarifa lakini kwa sababu ya kukosa taarifa ya tovuti gani nzuri na hivyo kuishia kukosa taarifa muhimu.
UKITAKA MAMBO YA BIASHARA:
MIKUTANO NA USAHILI/INTERVIEW YA ONLINE:
TAARIFA YA HABARI ZA TANZANIA, AFRIKA NA DUNIA
MASWALA YA KIROHO ,HALI YA HEWA , UBINADAMU PAMOJA NA KUJITOLEA
www. Beliefnet.com
HABARI ZA BURUDANI DUNIANI NA TANZANIA
KUJUA HABARI ,TAFITI ZA MAMBO NA VITU(MAKTABA YA DUNIA)
PICHA ZA KITAALAMU NA KUNUNUA PICHA:
MITANDAO YA KIJAMII:
KUNUNUA VITU MFANO VITABU NK.
MASWALA YA NDOA
Pangilia unachotaka kufanya kwa intaneti,usifanye tu kwa sababu linatokea,kifalsafa tunasema usipopanga jambo,sio kwamba hujapanga,ila umepanga lolote ambalo litakalo kukuta na likuchuke.Hivyo matumizi ya intanet angalia sana yasiibe sana rasilimali muda yako.
umeanza vizuri ukaendelea kipuuzi.
ReplyDeletesawa tumekusoma ,usihukumu kama unatoa ushauri wa kutumia internet,stick to the point! Asanye lakini kwa kutusaidia japo umetuhukumu!
ReplyDeleteaslaaama alekum/ shalom
ReplyDeletenapenda kutoa maoni kuwa huyu bwana amefanya vizuri sana sana na naomba watu waliojaliwa moyo huu wajitokeze zaidi. kwa mtazamo wangu sikuona kitu chochote kibaya bali amesema ukweli kwa wale wanaoadhirika. the truth hurts poleni. well done and keep it on.
Mdau tunakushukuru kwa kutuongezea elimu kidogo, Mungua akubariki uendelee kutujuza zaidi. Kwa wale wanaolaumu na kujiona wanajua zaidi, basi waonyeshe na kuthibitisha ujuaji wao kwa kuchangia na kuongeza points zaidi katika mada iliyowasilishwa badala ya kulala tu
ReplyDeleteahsante bwana mkubwa ulimwengu unatakiwa uwe na watu wa aina yako tuweze kusogea mbele. Nami naongezea.
ReplyDeletekwa wale wapenzi wa music tv http://www.tmtv.co.tz/
wapenzi wa zilipendwa za kongo
http://soukous.com/
for the geographers
http://www.gomapper.com/
Kazi kwenu,
asante saaana nilikuwa nahitaji sana hii mambo, na wale wenye roho za kwa nini mtajiju, mnabana hadi link mfaidi wenyewe, inahuu?
ReplyDeleteAhsante Mdau Deogratius Kilawe.
ReplyDeleteKwa Uamsho wako kwetu juu ya matumizi endelevu ya Mtandao!
Nilikuwa nafahamu masuala kadha wa kadha lakini hii taarifa yako imenifunua zaidi.