Watu watano wameuwawa na wengi kujeruhiwa kwenye shambulio katika kituo cha basi mjini Nairobi, Kenya.

Inaarifiwa kuwa maguruneti kama mane yalirushwa kutoka kwenye gari dhidi ya kituo cha basi mjini Nairobi - kituo cha Machakos Bus Station, ambacho kilikuwa kimejaa wateja.
Shambulio hilo limetokea Jumamosi saa mbili usiku.
Hadi sasa inajulikana kuwa watu watano wamekufa, na wengi kujeruhiwa.
Mbunge wa jimbo hilo la Kamukunji, Yusuf Hassan, alisema alihisabu majeruhi 40 walipokuwa wakifikishwa hospitali ya taifa, ya Kenyatta.
Wakuu bado hawakueleza nani alihusika na shambulio hilo; wala kama washambuliaji ni wa ndani au kutoka nje ya nchi.
Bwana Hassan alisema kuna majonzi na masikitiko mjini Nairobi kutokana na maafa hayo, lakini alisema safari za magari kwenye kituo zimeanza tena.
Aliwasifu watu wa Nairobu kuwa shupavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. MIRIPUKO au milipuko???
    Unahakika hicho kiswahili ni cha BBC kama unavyodai kuwa source ya taarifa?

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu wacha Upindi..mtu huelewi hakafu mbishi..taarifa kweli ni ya BBC Swahili km huamini si uingie kny web yao uone.Kwani hao BBC ndo wanaojua kiswahili safi?
    Ujanja wakuingia Michuzi unao lkn kuwakufanya simple reseach huna.

    ReplyDelete
  3. huyo mdau wa kwanza ni mpumbavu kweli. Kiswahili cha BBC ni kipi? kakupa link ya hiyo taarifa bonyeza, uone kama hiyo taarifa hautaikuta. au wewe wakati wote unapoaandika kuhusu jambo fulani, haujawahi kufanya makosa, mfano kutumia 'a' badala ya 'ha', au 'r' badala ya 'l'. Jua kuchnganya herufi kunaathiriwa na lugha mama. Mfano: Mkurya hutumia sana 'r' mahali pa 'l'.

    ReplyDelete
  4. Mdau uliyemkosoa Mdau wa Kwanza "ata wewe ni pimbi" hakuna ""Upindi"" najua ulitaka sema UPIMBI

    ReplyDelete
  5. Wala msihangaike!

    Hao ni 'nyoko' Al Shaabab wanajaribu kutupa kete za mwisho baada ya kushindwa vita kwao Somalia.

    Baharini utekaji wa Meli umekuwa mgumu zaidi hakukaliki, hebu nielezeni tokea mwaka 2012 umeingia zimetekwa meli ngapi?, si ndio wamesha shikwa wamekamatwa idara zote wanatapatapa sasa wanakuja lipua Nairobi!

    Ameng'oka Kanali Gaddafi aliyekuwa na Serikali, Idara bomba ya Ujasusi na Majeshi ije kuwa Mgambo wa Al Shaabab?

    ReplyDelete
  6. ahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Nafkr muache malumbano mjadili hoja uiliyoletwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...